Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,312
Pamekucha wakuu, nami naianza siku kwa hili.
Inafahamika wazi watumiaji wakuu wa barabara ni sisi wenyewe (binadamu/watu).
Kati yetu wapo wanaotumia magari, wapo wanaotumia pikipiki, wapo wanaotumia baiskeli, wapo wanaotumia miguu tuliyoumbwa nayo, wapo pia vilema wanaotambaa ama kwa magoti au hata makalio yao.
Sasa ukiangalia huu ujenzi unaoendelea wa hii barabara ya ubungo hadi kibaha na hatimaye chalinze, kuna kundi moja la watumia barabara limeachwa nyuma, kundi la waenda kwa miguu, waendesha baiskeli na vilema (PEDESTRIANS)
Haiwezekani katika dunia ya sasa ujenge barabara kuu (highway) iliyo katikati ya jiji bila kuwawekea waenda kwa miguu kinjia chao. Ingekuwa ni nje ya mji hapo sawa, kwa maana huko ni machakani hamna watu wengi wanaotembea kwa miguu.
Nimeamua kuweka hili ombi mapema kabisa kabla ujenzi haujamalizika ili kuondoa dhana ya kukosoa kila kitu, sitaki kusubiri ujenzi umalizike ndipo tuanze kutaja mapungufu yake wakati tunaweza kutoa ushauri angali mapema.
Hapa ni mjini, waenda kwa miguu ni wengi sana huwezi kusema watakuwa wanatumia barabara moja pamoja na magari. Ukizingatia itakuwa ni barabara 3 kwa 3 kwa 2 haitawezekana kabisa raia pia wajichanganye humohumo kwenye highway.
Kingine cha muhimu ni afya. Sote tunajua siku hizi magonjwa yasiyoambukiza yameongezeka kwa kasi sana. Moja ya sababu ni watu kuishi aina ya maisha yasiyo rafiki kwa afya zetu. Sasa kama ujenzi wa miundombinu hauko rafiki kwa ajili ya kubadili lifestyle zetu na hatimaye kupunguza haya maradhi hamuoni mnazidi kuipa serikali mzigo?
Wekeni barabara za watembea kwa miguu, jioni watu wafanye jogging za hapa na pale, mwenye kibaiskeli chake naye apate hamu ya kukiendesha. Unakuta mtu anatoka kimara mwisho kwenda kimara suka eti anapanda gari, like seriously? Hii yote inasababishwa na miundombinu kujengwa kwa ajili ya magari peke yake huku kundi la waenda kwa miguu(pedestrians) likisahaulika.