Ombi kwa Serikali yetu kwenye Sheria za Uchaguzi

APA CHICAGO

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
259
293
Ninaombi kwenye sheria zetu za uchaguzi kipengele kimoja tu kibadilishwe au kiongezwe.

Kwa maoni yangu ningependa iwe hivi Mbunge yeyote " Akijihudhuru au kuhama chama" basi aliyekuwa anafuatia kwenye kura wakati wa uchaguzi Mkuu yaani wa pili aapishwe ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi.

Nimependekeza marekebisho haya ili kuepuka gharama kubwa zisizo za lazima kama taifa tunazopata.Turudie uchaguzi tu pale bahati mbaya Mbunge anapoteza maisha.

Tumeshuhudia taifa likiingia gharama za kurudia uchaguzi katika majimbo kadhaa kwa kutaja kwa uchache majimbo yafuatayo: jimbo la 1.Nyarandu 2.Paulina Gekul 3.Chacha Ryoba na wengine wengi kibao.Kwenye upande wa udiwani huko penyewe usiseme wao ni wengi mno na penyewe kipengele hiki kiwe hivi hivi.

Kama kweli tuna nia ya dhati ya kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele kiuchumi basi hatuna budi kuchukua hatua mbali mbali kuthibiti mianya ya upotevu wa rasilimali fedha.Wanaharakati na watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii tuombe hili.

Wanasiasa kwenye hili awe ACT,CHADEMA, CCM,NCCR na Hata CUF hawawezi kuwa upande wa mawazo haya.
 
Ukihama chama huruhusiwi kugombea mpaka ipite miaka miwili kwa uelewa wangu (kama nakosea nisahihishwe). Hata hao wanaohama sasa au baada ya Bunge kuvunjwa hawataweza kugombea iwe ubunge au urais hadi watimize miaka miwili katika vyama vyao vipya.
 
Kama hili jambo lina maslahi na CCM basi watafanya hivyo haraka mno lakini kama litakuwa mwiba kwao tusitarajie chochote

Jr
 
Naunga mkono hoja
P
Kaka Paschal nikiwaza fedha zilizopotea kwenye chaguzi za marudio 2015-2020 hapo kati kati wakati kuna shule huko maeneo mbalimbali zina miundo mbinu mibovu.Wakati huo huo kuna fedha zinatumika kurudia uchaguzi ili mtu fulani tu ameamua kuhama chama hii ni too personal
 
Ukihama chama huruhusiwi kugombea mpaka ipite miaka miwili kwa uelewa wangu (kama nakosea nisahihishwe). Hata hao wanaohama sasa au baada ya Bunge kuvunjwa hawataweza kugombea iwe ubunge au urais hadi watimize miaka miwili katika vyama vyao vipya.
Kwa hiyo 2020 -2025 tusitegemee chaguzi za marudio za kama zile za 2015-2020
 
Back
Top Bottom