Ombi kwa Serikali: Futa salamu ya shikamoo

kiwiko

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
1,307
2,063
Kwanza maana ya shikamoo ni ipi? Marahaba ni kiarabu sijui ni nini?

Maneno hayaeleweki. Salamu haieleweki ni kwa ajili ya watu gani? Unajuaje umri wa mtu wa kumpa hio salamu maana sijui unatumia kipimo gani kujua aliekuzidi umri.

Hii ni salamu inayoleta mkanganyiko usio wa lazma kwa jamii.

Ni bora kutumia salamu moja inayoeleweka kwa watu wa rika zote mfano "Habari". Hio haitamaanisha ni ukosefu wa adabu na heshima.

Ombi kwa serikali na Bakita kufuta hii salama mbona nchi nyingine salamu ni moja tu na maisha yanaenda vizuri.

Nawasilisha.
 
ni mawazo yako tusikushangae.... umeitumia shikamoo miaka yote hiyo, leo hii umeota sharubu huitaki tena shikamoo?

Wazungu wanakitamani hichi kiswahili.....SHIKAMONJI yako tafakari upya hilo wazo lako
 
HII NDIYO HISTORIA HALISI YA MANENO "SHIKAMOO" NA "MARAHABA."

kuna idadi kubwa ya watu wanatumia neno shikamoo kama sehemu ya kuonyesha heshima au salamu kwa mtu aliyekuzidi umri.

Ila ni muhimu sana tukaelewa maana na historia ya na maneno “Shikamioo” na “Marahaba”. Kama ifahamikavyo kuwa kila jambo huwa na mwanzo na mwanzo huwa na sababu za kufanya hilo jambo kuibuka. Ni hivi kabla ya miaka ya 600 BK au BM, Wabantu walikuwa wameshafika Pwani ya Afrika mashariki. Na ukweli ni kwamba Wabantu walishapata kuishi hapo na hata wageni waliofika walikiri suala hilo. Na kwa kuwa Wabantu walipata kuishi hapo walikuwa na mitindo yao wa maisha na walikuwa wakiheshimiana.

Kikubwa zaidi Wabantu walikuwa na salamu zao. Kwa mfano Wazaramo (historia yao itaandikwa) walikuwa na salamu yao kama ifuatavyo, aliyekuwa akiamkia alionyoosha mikono mbele na kusema “simbamwenee” na kisha anayeamkia huitikia “utwaaa”. Na kila mtu alikuwa akifurahia salamu hiyo, iliyokuwa nzuri kuitamka mdomoni.

Lakini mambo yalibadilika pale walipokuja Waarabu na kuanzisha biashara ya utumwa. Na hapo tukapata makundi mawili yaani “mtumwa” na “bwana” na mtumwa alipaswa kumuamkia Bwana kwa neno la “Nashika Miuu” akiwa na maana ya “Nashika Miguu”. Na kila mtumwa alipaswa kujua na kutambua salamu hii.

Na mtumwa alipaswa kutoa salamu hii hata mara 100 kwa siku moja. Lengo la salamu hii ilikuwa ni kutenganisha kati ya mtumwa na bwana wake.

Kuanzia miaka ya 600-1700, salamu hii ilikuwa ikitumika maeneo ya Pwani tu. Na kuanzia miaka ya 1700 mwishoni na 1800 mwanzoni Waarabu walianza kuingia maeneo ya ndani ya Afrika mashariki. Na kila walipofika salamu hii waliitumia na baadhi ya machifu waliipenda sana salamu hii. Na kujikuta wakiwa na matamshi tofauti juu ya salamu hiyo. Na kwa wakati wote huo ilikuwa ni salamu ilikuwa ni "Nashika Miuu" na sio "Shikamoo" kama ilivyo sasa.

Kutokana na watu tofauti kutumia salamu hii, wapo waliotamka "Shikamuu" kama neno moja. Na mpaka miaka ya 1930, kipindi ambacho Kiswahili kinafanyiwa usanifishaji ndipo tukapata neno "shikamoo."

Na kuhusu neno "Marahaba", lina maana ya "asante". Na neno hili huitikiwa na Yule anaeamkiwa (Bwana) ambaye miguu yake imeshikwa na mtumwa. Na mpaka sasa salamu hii inatumiwa sana na Watanzania wengi licha ya kuwa na salamu zao za kikabila.

Hii ndio historia fupi ya neno "Shikamoo" na "Marahaba".

Shukrani za pakee ziwafikie "Historia ya Afrika"

Je wewe mpendwa una maoni yapi juu ya salamu hii?, JE inafaa kuendelea kuenziwa au haifai?
 
Hata mimi salamu hii siiungi mkono japo inaonekana hatuna mbadala. Inanikumbusha madhila ya utumwa
 
Kumbe!
 
h

hii salamu siipendi basi tu kweli haina maana yeyote
 
Back
Top Bottom