Ombi kwa Ras Magufuli: BRELA imeshindikana, iweke chini yako

businesslink

Senior Member
Mar 20, 2019
129
113
Mheshimiwa Rais.

Unahangaika kutaka kuifikisha nchi hii kwenye uchumi wa kati na wa viwanda kutimiza mipango ya maendeleo tuliyojiwekea kama taifa.

Moja kati ya sekta ambayo ni muhim kutekeleza hayo ni BRELA lakini kwa bahati mbaya sana wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwenye kusajili na pia kufanya malipo.

Kwa kifupi mtandao wa BRELA hauruhusu u yoyote yule kufanya yafuatayo:

1. Ku search jina la biashara au kampuni (Name search)....hii wanataka ufanye manually and it takes 2 weeks kupata majibu

2. Kujua wamiliki wa hizo kampuni ni akina nani na wanamiliki asilimia ngapi (shareholding structure)

3. Kufanya malipo kwa njia ya Simu au benki kupitia kwenye mtandao wa e-payment wa Serikali

4. Kufanya returns online

Mheshimiwa Rais, Waziri husika na viongozi husika watakwambia hayo yote yapo lakini sio kweli. Mhehsimiwa Rais, naomba uingie kwenye mtandao wa Brela kisha jaribu kutafuta jina la kampuni yoyote kwa kifupi hutopata hizo taarifa.

Kwa kumalizia na kukufanyia wepesi hawa ndio wahusika wakuu BRELA:

Waziri wa Biashara, Ndugu: Joseph Kakunda
Naibu Waziri wa Biashara, Ndugu Stella Manyanya
Katibu Mkuu wizara ya Biashara, Ndugu JosephBuchweishaija
Waziri wa Uwekezaji ,Ndugu Angelina Kairuku
Mkurugenzi Mkuu BRELLA ...................

Ushauri. Mheshimiwa naomba kama imeshindikana ichukue hii uiweke chini yako maana hao uliowapa majuku wameshindwa

ushahidi wa haya ninayosema huy hapa:

BRELA ORS
 
Naunga mkono hoja; kwa makampuni yaliyoanzishwa kabla ya March 2018 ni kama kila kitu kimesimama; hakuna unachoweza kufanya kwa sasa wakati returns zote za mwaka na mabadiliko mbalimbali wanazo wao BRELA.

Ni vizuri Mh. Raisi aingilie kwani kwa sasa huwezifanya chochote kwenye huo mtandao wao; na hata ukifanya kwa maelekezo yao bado wanarudisha na maelekezo mapya ili mradi hii kazi ya kuhuisha taarifa kwenye mtandao wao isifikie mwisho. Kwa uhakika mapato mengi ya Serikali yamecheleweshwa sana na huu mfumo wa kuhuisha taarifa usiokamilika
 
Brela wanamatatizo mengi sana hasa upande wa makampuni na ule wa leseni jamaa wanafanya kazi wanavyotaka na muda mwingine ukiwa mgeni usipopitia kwa kishoka wao basi utasubiri sana, kitengo kinachojitahidi ni wale wa trade mark jamaa wako vizuri hata ukipiga simu unapata msaada wa kueleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kna mtu analindwa pale
Mupe muruke.....angekuwa mtu ambaye yuko pale alafu mzee baba hamsomi zamani sana angeshamninginiza mbele ya makamera

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la BRELA ni ukosefu wa utaalamu wa mambo ya kutoa huduma kwa kutumia mtandao. Mwanzoni kabisa walianza kwa matumaini, kwa kutumia "Software" ambayo uliweza kujihudumia na mambo yalienda vizuri, Tangu walipobadilisha "Software" hiyo ya awali na kuanza kutumia hii iliyopo sasa, mambo yameharibika kabisa hasa kwa watu waliokwisha sajiriwa siku za nyuma.

Mfano; Mimi nilifanya mabadiliko kwenye jina na umiliki wa biashara, niliweza kurekebisha jina tu, baada ya hapo mtandao wao umegoma kabisa kuendelea na mchakato mzima na kutoa taarifa ya "error" kila ninapotaka kuanza upya. Niliwafuata kwenye ofisi zao pale Lumumba, kwanza wakabisha kwamba haiwezekani, lakini baada ya kurudia zoezi kwa maelekezo yao, Iliposhindikana wakanitaka nipige picha hiyo "error" niwapelekee watalaamu wa ICT ghorofa ya saba.. Kufika pale ...Kappa!... Mzee mmoja akanitonya kuwa ndio kwanza wanasoma, kila siku mchana wanaingia darasani hadi kwenye saa kumi jioni, nibahatishe kesho yake ila nifike mapema... Saa moja asubuhi!.

Mpaka leo nimekwama na "error" yangu ambayo siwezi kuondoa pasipokuwa na mkono wao!...Najipanga kwende kukabiliana nao hivi karibuni, lakini ni kweli kuwa, badala ya kurahisisha mambo; BRELA wamefanya mambo kuwa magumu. Pamoja na kusomesha wataalamu, waangalie utaratibu wa kupata "Software" yenye uwezo mkubwa.
 
Back
Top Bottom