Ombi kwa Rais Mwinyi: Wakumbuke Masheikh wa Uamsho ambao wanateseka huku familia zao zikiishi kwa shida

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Namshukuru M/Mungu , kwa kutupa utulivu na amani, mhe ris mwinyi , uchaguzi umekwisha na umefanikiwa kuanzisha furaha na upendo uliokuwa umeanza kutoweka hususani mara baada ya uchaguzi mkuu kuisha.

Ombi langu kwako (Mungu amrehemu Maalim Seif) na viongozi wengine uliowaalika kurejesha Serikali ya umoja wa kitaifa. Ni kuwakumbuka masheikh wa uamsho ambao naamini kabisa familia zao zinaishi kwa taabu na mateso na pengine kuna baadhi ya watoto wao wamekosa huduma muhimu hata ya masomi kwa kutokuwepo kwao.

Nakuomba Rais uwakumbuke binaadamu hawa ikiwa kama chachu ya ubinaadamu wako ulionza kuonekana na ambao umekusukuma kuhuisha upya Serikali ya umoja wa kitaifa.

Tukio hili liwe ni moja ya kumkumbuka almaruhuum Maalim Seif Sharif Hamad, kama kiongozi mlioketi pamoja na yeye kufuta machungu ya madhira yaliyotokana na uchaguzi mkuu uliopita 2020. Namuomba Mungu
 
Usiseme wakumbuke mashehe wa uamsho maana hawajashitakiwa Kama mashehe Bali wameshitakiwa kama raia wanaotuhumiwa kwa uhalifu fulani!
Sema wakumbuke watuhumiwa wa ..............
Uharifu gani mpaka leo hakuna kesi mahakamani? ingekuwa baba ako yupo ndani mpk leo bila kufungwa wala kufikishwa mahakani ungejisikiaje mpuuzi wewe? mimi siyo muislam lakini nachukia sn waislam kuonewa
 
Usiseme wakumbuke mashehe wa uamsho maana hawajashitakiwa Kama mashehe Bali wameshitakiwa kama raia wanaotuhumiwa kwa uhalifu fulani!
Sema wakumbuke watuhumiwa wa ..............kwe
Kweli walushtakiwa kama wahalifu lakini kwa sasa wanashijuliwa kama masheikh bila kuoelekwa mahakamani wala kusomewa kesi yeyote Yaani wanateswa kuliko maelezo kweli jiwe ni kafiri
 
Si wapo bara? Hilo jambo lilishabadilishwa na kufanywa la kimuungano. Muambieni nanihiii ndio alishughulikie
 
Sio maneno Ndio yanawafanya wakae jela isipokua wao na mheshimiwa wapo dini tofauti....
Sasa kwani yeye ndio aliwakamata hadi uanze kuzushia tuhuma za kidini, hao si walikamatwa na ndugu yao wenyewe kwenye imani, sasa magufuli yeye kwenye hizo dini kaingiaje hapo? Kuna mkono wa Magu ulihusika wakati wa kukamatwa kwao?

Ni kweli ana mapungufu ila haya mengine mnazidisha sasa.
 
Mkuu wewe una ushahidi gani kuwa walienda kumuomba hilo au unataka tuamini tu kwasababu wewe umesema kuwa walienda kumuomba akakataa?....
Mkuu kwenye vikao vya ndani vya ACT moja ya agenda ni kuhusu masheikh wa uamsho na serikali ya Umoja wa kitaifa. Na viongozi waandamizi Walisema swala hili lazima wawili hao wakaonane nae uso kwa uso ikiwezekana wampigie magoti maana ndugu na jamaa wanawapa pressure akina mwinyi kule Zanzibar.

Na kweli walienda na jamaa kwa kua na chuki na waislamu kwa macho makavu kakataa. Sasa hao viongozi wakuu walienda chato kutalii?
Vitu vingine sio lazima uwe na PhD kuelewa
 
Sasa kwani yeye ndio aliwakamata hadi uanze kuzushia tuhuma za kidini, hao si walikamatwa na ndugu yao wenyewe kwenye imani, sasa magufuli yeye kwenye hizo dini kaingiaje hapo? Kuna mkono wa Magu ulihusika wakati wa kukamatwa kwao?

Ni kweli ana mapungufu ila haya mengine mnazidisha sasa.
 
Sasa kwani yeye ndio aliwakamata hadi uanze kuzushia tuhuma za kidini, hao si walikamatwa na ndugu yao wenyewe kwenye imani, sasa magufuli yeye kwenye hizo dini kaingiaje hapo? Kuna mkono wa Magu ulihusika wakati wa kukamatwa kwao?

Ni kweli ana mapungufu ila haya mengine mnazidisha sasa.
Mkuu baadhi ya hawa masheikh walikamatwa na SMZ kabla ya yeye kua Rais lakini walikua wanapelekwa mahakamani kujibu kesi zao na ilikua wapo katika hatua za mwisho kufikia uamuzi.

Sasa jiwe alipoingia akaamrisha kesi zote ziache kusikilizwa na kila kukicha kuna viongozi wa kiislamu wanakamatwa kwa tuhuma za ugaidi kuanzia arusha. Mbeya. Tanga. Mwanza nk.

Anyways hakuna mtu anasema waachiwe lakini kwa sababu nchi hii Kuna mahakama je kwa nini hawapekekwi mahakamani?
Huyu mtu katili sana.
 
Mkuu kwenye vikao vya ndani vya ACT moja ya agenda ni kuhusu masheikh wa uamsho na serikali ya Umoja wa kitaifa...
Ninachotaka mimi hapa utoe ushahidi wa hicho unachoseme na si porojo poroja na hisia zako binafsi, hao viongozi kuenda chato sio ushahidi wa kuwa eti ndio walikwenda kuleka hilo ombi.

Sitaki umbea hapa wa kuishi kwa hisia hisia huku tukiwapachikiza watu matuhuma yasio na uhakika.

Unanambia habari za vikao vya ACT kwahiyo wewe ni mjumbe wa kamati kuu ya ACT au? Kwahiyo walipo toka huko walipokataliwa ndio wakaja kuwapa habari kuwa walikataliwa
 
Back
Top Bottom