Elections 2010 Ombi kwa professors na wasomi wa Tanzania

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Wapendwa Maprofessor na Wasomi wa Vyuo Vikuu

Acheni kugombea kwa tiketi ya CCM. Iga mfano wa Professor Baregu, Dr.Mbassa, Professor Kahigi, Profeesor Mlambiti na wengine wenye mapenzi kwa mabadiliko. Mungu atawalipa zaidi mkiwakomboa watanzania walio wengi kuliko kujali ubinafsi.

Tukipata vichwa safi katika upinzani, hakika CCM itang'oka kwa asilimia 75% mwaka 2015.

Tuanze sasa.

Nami nahitaji kadi ya CHADEMA.
 
wanaJF nahitaji kadi ya uanachama chadema. naomba maelekezo ya namna mimi natokea Ilala, ofisi ziko wapi?
 
wanajf nahitaji kadi ya uanachama chadema. Naomba maelekezo ya namna mimi natokea ilala, ofisi ziko wapi?

download katiba ya chadema futa taratibu za kuanzisha tawi fungua tawi ulipo na uwasiliane na uongozi wa eneo husika mtapata kadi.
 
Nakubaliana na wewe kwa 100%. Mimi ni miongoni mwao na nitaanza maandalizi mapema ya kwende kugombea huko Mbinga 2015.
 
Mie natoa onyo kali kwa Mbunge mteule wa Kigamboni. Mungu anipe uhai, tuko sambamba 2015.
 
Hata mimi nasema Kigwangala ajiandae kuzolewa na mafuriko 2015 huko Nzega. Kama hatafunga buti kutatua kero za wananchi ajue itakula kwake 2015.
 
saa ya mabadiliko ni sasa, vita ya kuingoa ccm madarakani inaanzia sasa, awastaili awastaili awastaili wanaichafua ofisi yetu kubwa ya magogoni kwa kundi lao la waganga, mahawala n.k
 
CCM kwa ushauri tu, chukueni kila mnachoona kinawafaa kwa miaka hii mi5. 2015 hamna chenu...
 
download katiba ya chadema futa taratibu za kuanzisha tawi fungua tawi ulipo na uwasiliane na uongozi wa eneo husika mtapata kadi.

Aisee hebu niambie katiba ya CHADEMA tunaidownload kutoka website gani? Maana tunamachungu sana na tunataka kuimarisha chama:israel:
 
wanaJF nahitaji kadi ya uanachama chadema. naomba maelekezo ya namna mimi natokea Ilala, ofisi ziko wapi?

Nakuombea uzima ufanikiwe lengo lako mkuu..

download katiba ya chadema futa taratibu za kuanzisha tawi fungua tawi ulipo na uwasiliane na uongozi wa eneo husika mtapata kadi.

Hata mimi nimekupata mkuu

Nakubaliana na wewe kwa 100%. Mimi ni miongoni mwao na nitaanza maandalizi mapema ya kwende kugombea huko Mbinga 2015.

Naam

Mie natoa onyo kali kwa Mbunge mteule wa Kigamboni. Mungu anipe uhai, tuko sambamba 2015.

Hilo nalo neno mkuu, good luck

Hata mimi nasema Kigwangala ajiandae kuzolewa na mafuriko 2015 huko Nzega. Kama hatafunga buti kutatua kero za wananchi ajue itakula kwake 2015.

Kabisa.
 
Jamani naomba utaratibu wa kuipata kadi ya CCM. Chama hiki kimenifurahisha sana. Kimewagaragaza wapinzani. WanaJamii forums sasa wamefura kwa hasira baada ya ndoto zao kuyeyuka. Niambieni jamani nitapata wapi kadi ya CCM?
 
Mimi niko serious na mikakati hii ya kuing'oa CCM 2015. Naomba wana JF wenye mapenzi mema na nchi yetu na wanaotaka kuimarisha upinzani kupitia CHADEMA tuandae kikao ambapo tutakutana na kufahamiana ili tuunde timu ya operation Nyangumi itakayoanza kazi mapema kabisa mara tu baada ya uchaguzi huu. Nawasilisha hoja hii kwa uchungu usioelezeka kwa maneno tu.
 
Silas karibu Nzega 2015 kama uko tayari kushindana na mimi!na mimi natangazA nia ya kugombea ubunge nzega 2015! Kwa miradi ya maendeleo niliyokusudia, kwa uwezo wangu wa kufuatilia utekelezaji wa sera za chama changu sidhani kama utafua dafu labda utafute jimbo lingine legelege! Nzega itakuwa ngumu sana kwako ndg yangu!

Nakushauri u-track my record ili ujue Kigwangala ni mtu wa aina gani ndipo uanze mkakati wako usije ukapoteza muda wako bure tu!

Matokeo ya sasa ya uchaguzi ni kaburi la CCM 2015
 
Silas karibu Nzega 2015 kama uko tayari kushindana na mimi!na mimi natangazA nia ya kugombea ubunge nzega 2015! Kwa miradi ya maendeleo niliyokusudia, kwa uwezo wangu wa kufuatilia utekelezaji wa sera za chama changu sidhani kama utafua dafu labda utafute jimbo lingine legelege! Nzega itakuwa ngumu sana kwako ndg yangu!

Nakushauri u-track my record ili ujue Kigwangala ni mtu wa aina gani ndipo uanze mkakati wako usije ukapoteza muda wako bure tu!

Mwenye kufanya mambo huwa hajisifu bali husifiwa kwani unapomdharau mwezio hujui atakuja na nini litakalokushinda wewe. La msingi wewe ni bora ukafanya kazi ya maana huko Nzega ili akija jamaa asifue dafu. Ni ushauri tu Mh. Hamisi
 
Wapendwa Maprofessor na Wasomi wa Vyuo Vikuu

Acheni kugombea kwa tiketi ya CCM. Iga mfano wa Professor Baregu, Dr.Mbassa, Professor Kahigi, Profeesor Mlambiti na wengine wenye mapenzi kwa mabadiliko. Mungu atawalipa zaidi mkiwakomboa watanzania walio wengi kuliko kujali ubinafsi.

Tukipata vichwa safi katika upinzani, hakika CCM itang'oka kwa asilimia 75% mwaka 2015.

Tuanze sasa.

Nami nahitaji kadi ya CHADEMA.

Wasomi hawaihitaji kujiunga na chama na siasa kwani itikadi za kisomi ni kuwa unasimamia principles za fairness and truth. Kujiunga na chama fulani cha siasa ni kuhama kutoka kuwa msomi na kuwa mwanasiasa. Kuna msemo mmoja maarufu unasema " A Politician is a failed academician" . Hivyo sidhani Tanzania inahitaji wasomi kujiunga na chama fulani cha siasa bali ni suala la Watanzania kujitoa katika limbi la ujinga na kuelewa nini kinaendelea. Kwani tukiwa na taifa lenye kujua nini kinaendelea nadhani changes will come otherwise hata wasomi wote wakijiunga na chadema hakuna changes zozote zitatokea Tanzania. Kumbuka wanaopiga kura tanzania si wasomi pekee bali watanzania wenye kujua na wasiojua kusoma.
 
Jamani naomba utaratibu wa kuipata kadi ya CCM. Chama hiki kimenifurahisha sana. Kimewagaragaza wapinzani. WanaJamii forums sasa wamefura kwa hasira baada ya ndoto zao kuyeyuka. Niambieni jamani nitapata wapi kadi ya CCM?

zinapatikana kwa shekhe yahaya
 
Wasomi hawaihitaji kujiunga na chama na siasa kwani itikadi za kisomi ni kuwa unasimamia principles za fairness and truth. Kujiunga na chama fulani cha siasa ni kuhama kutoka kuwa msomi na kuwa mwanasiasa. Kuna msemo mmoja maarufu unasema " A Politician is a failed academician" . Hivyo sidhani Tanzania inahitaji wasomi kujiunga na chama fulani cha siasa bali ni suala la Watanzania kujitoa katika limbi la ujinga na kuelewa nini kinaendelea. Kwani tukiwa na taifa lenye kujua nini kinaendelea nadhani changes will come otherwise hata wasomi wote wakijiunga na chadema hakuna changes zozote zitatokea Tanzania. Kumbuka wanaopiga kura tanzania si wasomi pekee bali watanzania wenye kujua na wasiojua kusoma.

mkuu,
kukopi mawazo ya watu wengine na kuyachukuli kuwa ni final ni mbaya, na wewe ukiwa ni msomi unakubariana na huo msemo
wenye mapungufu ya fikra hapo
kwenye bold red?
 
Mkuu ni mtazamo wa kwangu sijasema kuwa ni final but huo msemo unasemwa sana na wasomi wengi. Huwezi kuwa msomi unafata principles za kisomi halafu ukawa unakuwa mwanasiasa, lazima utakuwa unapindisha pindisha maneno tu kutetea hoja zako.
 
Wasomi hawaihitaji kujiunga na chama na siasa kwani itikadi za kisomi ni kuwa unasimamia principles za fairness and truth. Kujiunga na chama fulani cha siasa ni kuhama kutoka kuwa msomi na kuwa mwanasiasa. Kuna msemo mmoja maarufu unasema " A Politician is a failed academician" . Hivyo sidhani Tanzania inahitaji wasomi kujiunga na chama fulani cha siasa bali ni suala la Watanzania kujitoa katika limbi la ujinga na kuelewa nini kinaendelea. Kwani tukiwa na taifa lenye kujua nini kinaendelea nadhani changes will come otherwise hata wasomi wote wakijiunga na chadema hakuna changes zozote zitatokea Tanzania. Kumbuka wanaopiga kura tanzania si wasomi pekee bali watanzania wenye kujua na wasiojua kusoma.
Kitu kikubwa ambacho wanaweza kusaidia kwa mtazamo wangu ni kuzungumzia mapungufu ya katiba tunayo tumia kwa sasa na kuunga mkono
watu wote wanaopigania usawa katika medani za siasa. Naamini wanaweza kuanzisha motion ya mabadiliko ya katiba kwa manufaa ya taifa na siyo chama fulani, kwani TZ ni yetu wote. Kama inakufever sasa hivi ujue kuna wanaoumia na ipo siku itakugeuka kama sio wewe basi kizazi chako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom