Ombi kwa Mwenyekiti wa NICOL na Bodi yake

wade adams

Senior Member
Dec 2, 2011
160
47
Tumefurahi sana kwa kazi kubwa uliyofanya kuokoa NICOL kutoka kwenye meno ya mafisadi. Tumesoma taarifa yako kwa kina na tumegundua madudu mengi sana yaliyofanyika ikiwa ni pomaja na kufanya NICOL kuwa ya mtu binafsi. Inaonekanika maamuzi yote yalikuwa yanafanywa na mtu mmoja, wengine walikuwa wana "endose".

Tumeona upotevu wa 10btzs ni fedha nyingi sana haswa ukizingatia ni mchango wa makabwela.
Tumeona vision na mission ya NICOL ni superb hii ndiyo ndoto yetu tulio nayo wengi.

Kile kiwanda cha nyama na samaki kipo au ndiyo danganya toto. Tupate taarifa iliyoshipa kuhusu hivi viwanda hata kama itakuwa special audit. Tunaomba kama itawezekana kwa kutumia sheria zilizopo tumtumie CAG. Jitahidi kutumia gharama ndogo za uendeshaji walau 0.5% ya mtaji au chini zaidi. Tufuate style ya Raisi ya kubana matumizi.

Maombi yetu:
Pamoja na hiyo mission,hebu tuangalie matatizo ya Mtz. Tatizo kubwa hapo Bongo sasa hivi ni ajira kwa vijana. Ni vizuri basi miradi yetu hiyo itakayobuniwa ikawa ya kutengenexa mazingira ya ajira na faida ya kutosha
Wanahisa tunaomba ukuwaji wa mtaji ukuwe na sisi (yaani hisa zetu zikuwe) lazima huo utaratibu uwepo. Mgao wa dividend uwe tofauti na ukuaji wa mtaji, kama mwahisa atapenda kuuza sehemu yake kubakia na principal hiari yake. Itakuwa siyo haki nilipie share mwaka 2003 kwa million moja, mwaka 2016 mtaji ubakie million moja ile ile.

Gharama za mashauri ya kumng'oa Felic Mosha ni nani anabeba!
Nini mpango wa NICOL miaka mitano IJAYO, tunaomba isiwe kununua stocks/share bali ilenge vile vile kujenga viwanda vya kati ambavyo ni rahisi kuendesha na kutengeneza ajira faida ya kutosha, kuleta maendeleo ya nchi na kutengeneza kodi.

Tunaomba NICOL ianzishe microfinance company ili kuwezesha watz kukopa.
Hebu NICOL iwe mkombozi wa watz siyo mzingo na kichocheo cha ugomvi na sehemu ya kupiga dili CHONDE CHONDE
 
NICOL ni nini?
Ni compuni ya wananch ya uwekezaji. Iliunda na kusajiliwa brela na jamaa fulani wakiongozwa na felix mosha. Miaka ya 2000 -2003 ilichangisha mitaji kwa wanamchi wa kawaida kama wewe na mimi. Walikusanya hela nyingi kutoka kwa wananchi na serikali ikachangia. Sasa hivi imesajiliwa Dar Stock Exchange. Ni kampuni ya wananchi. Hapa nyuma ilihujumiwahujumiwa lakini sasa hivi inaelekea kuzuri. Mwenyekiti mwazilishi.alikuwa Felix Mosha, wajumbe walikuwa Idd Simba, Mama Masasi Signs, Reginald Mengi. Sasa hivi Mwenyekiti wa Muda ni Dr Kaunda msomi mzuri mwenye umri wa kiuwenyekiti, aliyetembea na kufanya kazi kwenye mashirika mengi nje na ndani yanchi,wajumbe ni eng salewi na joyce ambaye ni mhasibu. Dr kaunda sijui ni mdogo wake keneth kaunda raisi wa zamani wa zambia. Huyu raisi ndiye walianzisha sadc na baba taifa na bado yuko hai.
Mkuu umeshiba au bado
 
Nmeshiba mkuu
 
Back
Top Bottom