Ombi kwa MO: Ongezeni Mzumbe kwenye kuwapa mikopo

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Nianze kuwakumpongeza MO kwa kuamua kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji kwa watakaochaguliwa UDSM na SUA. Nadhani amechagua vyuo hivi kwa kigezo cha sifa nzuri kwa vyuo hivi lakini pia kwa kuwa ni vyuo vya kitaifa. Ila naomba niwashauri waongeze na chuo cha Mzumbe kwani pia kina sifa nzuri na ni cha kitaifa pia. Sababu zangu ni kuwa:

1. Chuo cha mzumbe kinatoa kozi nyingi ambazo hazijapewa kipaumbele na bodi ya mikopo tofauti na SUA, hata UDSM. Hivi vyuo viwili walivyovichagua wanafunzi wake wengi hupewa mikopo na bodi. Kwa hiyo wao MO wangejikita mahali ambapo bodi haifadhili wanafunzi wengi. Kwa mfano kozi karibu zote za SUA zina kipaumbele kwenye mikopo, kwa hiyo haileti maana kwa MO nao kukimbilia kufadhili wanafunzi ambao wana uwezekano mkubwa wa kupewa mikopo na bodi.

2. Haileti logic kusaidia mahali ambapo tayari kuna msaada, vinginevyo italeta picha kuwa hawakuwa serious kusaidia wahitaji.

Lakini pia, MO angewaomba Heslb wamsaidie kumpatia wanafunzi wanaostahili kupewa mkopo lakini haikuweza kuwapa mikopo maana tayari Heslb wana maombi na taarifa za kuwawezesha kuchambua mikopo hiyo.
 
Mo sidia watanzania /wanafunzi wenye uhitaji kwa vyuo vyote kulingana na uhitaji nasio jina LA.chuo itakuwa umefanya something amazing
 
Back
Top Bottom