Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 583
Kwanza nianze na pongezi kwa Mh Rais na serikali yake aliyokwisha kuiunda na kuanza kazi rasmi na hata kutimiza siku 100 ikiwa madarakani. Sasa nijielekeze kwa hoja ya ombi langu ya kuwa kutokana na awamu za uongozi zilizo kwisha kupita zimekuwa na tamaduni / Taratibu za kuongea na wazee wa Dar es salaam jambo ambalo limekuwa adhimu sana na muhimu sana kwa wazee wa Dar es salaam.
Ombi langu ni kuwa utaratibu huu ni mzuri sana kwani unakufanya Mh Rais kuwa karibu na wananchi wako kupitia mazungumzo hayo unayo yafanya na wazee wa Dar es salaam kwakua unapata kueleza muelekeo wa serikali yako ili wazee nao wapate kufahamu nini kinaendelea kwenye Taifa lao, lakini sasa ingependeza utaratibu huu wa kuongea na wazee wa Dar es salaam sasa ukabadilika na uwe kwenye mikoa mingine kama mkoa wa Mwanza , Pemba na hata Mtwala n.k na hii italifanya Taifa kuwa na wazee wenye hadhi moja na si kwamba wazee wa Dar es salaam kuwa wao ndio wanahadhi ya kuzungumza na Mh Rais na wa mikoa mingine hawana hadhi ya kuzungumza na Mh Rais. Katika kutimiza jambo hili nakuomba Mh Rais uanze kuzungumza na wazee wa Mwanza pale BOT ambapo naamini watakupa mawazo ya hekima na busara na hivyo kukufanya uendelee na shughuli zako za Kuliongoza Taifa hili adhimu barani Afrika naomba Mh Rais ukubali ombi hili ambalo shahiri dhahiri unafahamu kuwa ni muhimu sana kwakua Mwanza Mh, Rais tunajiandaa sasa kuwa Jiji kubwa kama la GENEVA kwa niaba ya wazee wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla karibu Mwanza Mh Rais JOHN POMBE MAGUFULI.