Ombi kwa Mh. Lukuvi; Tunaomba umshughulikie MKurugenzi mtendaji wa Muheza

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,357
73,935
Tunakuomba uingilie kati utaratibu unaotumiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Muheza katika kugawa mashamba kwa wananchi. Mashamba hayo ni Azimio na Kibaranga.

1. Kinachoonekana ni kuwa kuna mbinu chafu wanayotaka kuitumia kuwa kama huna nyumba pale huna haki ya kuwa na ardhi pale, wakati watu wamelima na kuwa na ardhi hiyo miaka zaidi ya 10, 20 etc.

Usingeliweza kujenga nyumba au kuweka mazao ya kudumu sehemu ambayo ina migogoro kwani Rais alikuwa hajatengua umiliki.

2. Mashamba mengine yalikuwa mapori na hivyo watu walitumia hela kubwa kuyafyeka, kung'oa visiki. Haikubaliki uchukue ardhi kama hiyo umgawie mtu bila fidia ya gharama za uendelezaji wa mashamba hayo kama mfyekeji visiki, kulima etc.

3. Wanataka kupachika watu wao ambao mpaka rais anatengua umiliki wa mashamba hayo, walikuwa hawa ardhi pale. Kama kupewa wapewa ambayo ni mapori hayana watu wanaokaa mle.
 
toa pendekezo lako! na maoni, fikra zako zinakutuma vipi juu ya ugawaji wa mashamba hayo?
 
Back
Top Bottom