Ombi kwa Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Uongozi Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi kwa Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Uongozi Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Jan 28, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi siamini kama kuna uwezekano wa kiongozi mzuri kutoka CCM. JK alikuwa chaguo la wengi na wengi tulimpenda ila baada ya JK kutuangusha kwa jinsi tulivyoweka matumaini kwake sioni kama kuna mtu mwingine ndani ya ccm anaweza kuibadili ccm kiwe chama kizuri. Nakiri, nampenda sana Dr Slaa kwa kuwa namwona kama ni mkombozi, mtu asiyeweka maslahi yake binafsi mbele lakini hata Dr Slaa akigombea kwa tiketi ya ccm sitampa kura kwa vile tatizo ni chama si mtu au watu.

  Maombi yangu kwa uongozi wa chadema ni kwamba kwa kuwa watanzania tunaiona chadema kama chama mbadala, kizogezeni zaidi chama kwa watu ili kiwe chama cha watu na si cha viongozi. Naomba mzingatie yafuatayo, ni maoni yangu tu yapo subject to criticism ila nayatoa kwa nia njema ya kujenga chama chetu.
  (i) Kwanza, tutenge siku moja kwa mwaka, nadhani siku ya kumbukizi ya kuzaliwa chama, tufanye mikutano nchi nzima, lakini badala ya kuhutubia tuwape wananchi nafasi wao wazungumze. Ni ukweli kwamba Tz tuna brains nyingi sana na ufumbuzi wa matatizo yetu tunayo ila tatizo ni kukosa uongozi wa kuyaweka mawazo yetu pamoja na kuyatekeleza. katika mikutano hiyo ya wananchi wa kada mbalimbali na makundi mbalimbali, tuwaulize wana matatizo gani na wanataka matatizo yao watatuliwe vipi. Tukiyakusanya maoni ya watanzania kwa miaka minne, tunaya summarize na kuyatumia kutengeneza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015.

  Hapa tutakuwa na mawazo na maoni yanayohusu jimbo kwa mfano wananchi wa ubungo wanaweza kutoa maoni kuhusu jimbo lao na nini kifanyike kuwakomboa, hapa tutatengeneza ilani ya mgombea ubunge na udiwani, yale ya kitaifa basi yanatumika kujenga ilani ya mgombea urais. Kwa kuwa watu wanapigia kura ilani za vyama na kwa kuwa ilani ya chadema itakuwa si imposed bali imetoka kwa watu basi si rahisi watu waipinge.

  Kikubwa zaidi ni kwamba sidhani kama malengo yetu ni kushinda uchaguzi tu bali kuisukuma Tz mbele. Kama ilani itatokana na wananchi wenyewe basi itakuwa yao na itatekelezeka. Fuatilia kwa mfano mijadala kuhusu umeme, watu wana mawazo makubwa mno namna ya kuondoa tatizo hili, kama tukichukua mawazo haya na kushirikiana na wananchi wenyewe hakika tutashinda. tatizio la ccm ni kwamba mambo hayatoki kwa watu bali yanatoka juu. Mfano mwingine, tatizo la ajira ya vijana lina ufumbuzi unaotokana na vijana wenyewe, kaa na vijana wasomi, wamachinga, mama ntilie waulize nini kifanyike watakupa mawazo makubwa hadi utashangaa. Tukitumia mawazo yao na kuwatumia wao kutekeleza tutashinda hakika.

  (ii) Pili nashauri chama kiajiri on part time basis washauri rasmi wa chama. Watafutwe watu makini na waliobobea katika fani mbalimbali walipwe vizuri kazi yao iwe kufikiri na kufanya utafiti kuhusu mambo ya chama. Naomba tuanze na washauri wanne, wa uchumi, siasa, mambo ya nje na gender. hawa washauri wasiwe wajumbe wa kamati kuu bali wawe watu huru na hata si lazima wawe wanachama ila wanaweza kuhudhuria vikao kama observers tu. natoa tu mfano, ukimchukua Jenerali ulimwengu kama mshauri wa siasa, unamlipa vizuri, kazi yake iwe ni kutafiti, kufuatilia siasa ya nje na ndani na kushauri nini kisemwe wakati gani na chama ki react vipi kuhusu mambo mbalimbali, tuwe na ilani ya jinsi gani, hatuba zibebe nini nk tutapata advantage sana. hata mambo kama maandamano ,kutoka nje bungeni nk lazima mtu huyu ashauri political implication.

  Week end njema, tupo pamoja kwa mapambano.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Akhasante kwa maoni yako tutayafanyia kazi.
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Suala uliloshauri ni la msingi sana .Nadhani wanaoitakia tz mema wapo humu yale ya muhimu watayachukua.

  Nakutakia weekend njema.
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Pengine hujui ulisemalo au unajua unalolisema ila unataka kusikia kama sisi wote ni MBUMBUMBU kama wewe. wewe unaonekana hujui tofauti kati ya ilani ya chama na matatzo ya wananchi, huwezi kuunda ilani ya chama kwa kusikia anataka nini. wananchi wote wakisema hawataki kufanya kazi utafanyaje?

  Lakini pia umesahau kuwa mawazo ya wananchi kuwakilishwa na viongozi kama wabunge, madiwani na wengine siyo sera ya CCM, duniani kote wanafanya hivyo. Unanishangaza sana unaponiambia CDM iajiri washauri ambao siyo lazima wawe wanachama, Thehe thehe thehe, sijui umelala au unaota. Kama wafanyakazi wa Media mbali mbali za Vyama tayari wameegemea kwenye vyama hivyo iweje hao washauri wasiwe wananchama.

  Sitaki nikutajie watu kama akina Prof. Baregu walivyoingia kwenye siasa kimya kimya ila tu nikupe mifano kama wafanyakazi wa Tz Daima na uhuru walivyo wakereketwa wa vyama vyao. achilia hao kwa sababu kula watoto wao wanakwenda chooni kwa sababu ya vyama hivyo, vipi akina Said kubenea na wengine wengi?

  Mbona unajificha sana unaposema tatizo nini CCM na siyo mtu, kwa nini usisema CCM ni kama timu ya mpira ya ARSENAL yenye umaarufu wa kuzalisha wachezaji bora ila hawezi kushinda makombe? Akina SLAA wametokea wapi?

  Sisi tuliosoma siyo miaka ya siku nyingi kwani mwaka 1990 mimi bado kijana mbichi ulikuwa ukiingia sekondari unakutana na kadi ya umoja wa vijana wa CCM unataka akina SLAA, MBOWE ZITTO na wengine walipikwa wapi kama siyo CCM?

  Labda ungeomba msamaha kwa kusahihishusemi wako na kusema tatizo siyo CCM bali watu ningekuelewa. Pole sana kama nimekuudhi mkuu siegemei kokote ila siasa za Tz na hasa za CDM ni kijicho tu wala hakuna nafuu yoyote itakayopatikana kwa wao kuingia madaraakani sana tu labda hali itazidi kuwa mbaya. Serikali ya akina SUGU, LEMA MDEE SLAA, MBOWE , LISSU? labada kama ni kikundi cha Cinema.
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Sugu 1 sasa hao unaowatetea wana miaka 50 sasa badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma. Bila kukubali mabadiliko hali zetu zitakuwa duni. Sasa itakuwaje msafi ndani ya nyumba chafu, kwamba chama sio tatizo tatizo ni watu sasa kama chama kinalea ubovu hakiwezi kuwa bora.
   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe haya maoni ni kwa ajili ya CDM. Ukiyapeleka CCM yatazidi kukiua.

   
 7. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hakika kuna watu ndani ya Jf wana uzalendo wa kuliwezesha taifa letu kusonga mbele, ndg yangu huu ushauri wako tutauchukuwa na kuufikisha panapostahili, tunazidi kukutia moyo kwamba utajibiwa na msemaji wa chama siku yoyote kwa jinsi ulivyopendekeza. Ninajua matumaini ya watu wanyonge yako Chadema, hivyo toeni mawazo yenu kadili mtakavyoweza. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU SIMAMA Na watu wako
   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  We pakashume nini
   
 9. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  duh masihara haya sasa
   
 10. i

  ibange JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naomba nikujibu kwa ufupi.
  (i) Ilani ni sera za chama ambazo kimsingi zinaelezea ni jinsi gani kitakavyotatua matatizo ya watu. Kwa mfano ni jinsi gani ya kutatua tatizo la umeme, ajira, kuanzisha viwanda nk. Mimi naamini kwa dhati wananchi wana solution ya matatizo yao ila tu wapate viongozi bora. Sasa unavyobisha kuwa ilani haipaswi kutoka kwa watu inashangaza. Pia tatizo la ilani ya vyama vyetu hasa ccm ni kwamba haitokani na watu. kwa kuwa nguvu ya watu haohao ndio itategemewa kutumika kutekeleza ilani, kama ni alien kwao ni vigumu kuiunga mkono.

  (ii) Narudia, tatizo la CCM ni mfumo wake ambao umejenga matabaka ya wakubwa na wadogo. Watu wanateuliwa kwa vile ni watotot wa wakubwa si kwa vile wanaweza. matokeo yake mambo hayaendi. Hii ndiyo iliyotokea Zambia na malawi. kwamba viongozi hao walishindwa kutekeleza sera zao hadi walivyohama vyama vyao. CCM kinaweza kuwa chama kizuri kwa maana ya sera na muundo ila kamwe hakitaweza kuwa chama kizuri kwa maendeleo kwa maana mfumo wake hauruhusu mapinduzi ya kifikra na kuondoa rushwa na matatizo mengine ya jamii. They are always out to maintain status quo.
   
 11. cheze

  cheze JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  Nimependa sana HONI/PENDEKEZO la kwanza, ni lazima ili walichukuwe kama wapo makini..chama lazima kiwe na kumbukumbu ya kuundwa..lakini wasije tumia fedha nyingi katika hizo kumbukumbu za kuzaliwa chama.
   
 12. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kazi ipo duh
   
 13. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono maoni.. chama makini kinakuwa karibu na wananchi na kusikiliza matatizo ya msingi... na kuyafanyia kazi....
   
 14. mzee wa miba

  mzee wa miba JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 763
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inavyoonekana wewe umetumwa na mafisadi kuyaongea hayo na sidhani kama unafikiria kwa ubongo ama kwa mgomgo.
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Good job Ibange, we need people like you with forward thinking entrepreneurship.
  kwa kuongezea tu ni kuwa wanahutajika wataalam kwenye sekta zote kukishauri chama kuanzia uchumi, sayansi na technologia
  na mengineyo mengi na siyo lazima watu hawa waajiriwe na chama bali wanaweza kufanya kazi kwa kujitolea na endapo chama kitachukua nchi basi wao ndio wanakuwa wa kwanza kufikiriwa kwa nafasi mbalimbali.

  pili ili chama kionekane serious lazima majibu yao yazingatie utaalamu na siyo ushabiki wa kisiasa. ndiyo maana siku za nyuma nilipendekeza chadema kuwa data base ya wanachama wake wote nchi nzima na profile zao ili kujua ni wangapi na utaalamu wa nyanja zipi ili kama ikiwezekana wawe wanapata msaada kutoka kwa wanachama wao kwa ajili ya maendeleo ya chama.
  chadema inashindwa kugema kwenye resources ilizonazo ambazo ni nyingi sana hii inanipa wasiwasi ili tusije kuwa kama CCM kushindwa kutumia rasimali tulizonazo iili kujiletea maendeleo badala ya kuzunguka dunia nzima kuomba omba.
   
 16. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zetu wa Burundi wanakitu kinaitwa Accountability day siku hii wananchi huitumia kuikosoa serikali yao kwa kuyataja mapungufu na kutoa mapendekezo hii inaweza kutumika pia hapa kwetu na serikali na ikishindikana serikalini basi chama makini kama CHADEMA wanaweza itumia hii ili kuleta uhalisia wa nguvu ya umma. Naunga mkono hoja kwa asilimia 88.
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Thanks. Mchele utachukuliwa, pumba zitaachwa.
   
 18. S

  Stany JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Good !ndg una mawazo mazuri sana God bless u
   
Loading...