Ombi kwa Kikwete: Kabla hujatoka madarakani ipe Kahama,Masasi na Ifakara Mikoa

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,630
3,577
Hizi wilaya zimekamilika kila kitu milishangaa sana uliulipounda mikoa kama njombe katavi,simiyu wakati haijazifikia wilaya tajwa kila sekata.
Pia nashauri kuongeza ufanisi wilaya za kibaha bagamoyo zizihamishiwe katika mkoa wa dar es salaam, mkoa wa pwani ubaki na rufiji,mkuranga mafia na kisarawe kwani kwa salsa inaleta mkanganyiko,
 
Kwa maoni yangu hakuna sababu za msingi na zenye tija kwa wananchi kugawagawa mikoa na kuanzisha urasimu mpya wa mikoa mipya. Ni kuongeza ulaji wa watu fulani usio na manufaa ya kweli kwa wananchi. Mikoa iliyopo inatosha, na pengine ni mingi mno.
 
Kuanzisha mkoa ni gharama sana hata hiyo mikoa 4 iliyoanzishwa ilipita miaka miwili bila kuwa na bajeti ikitegemea bajeti ya mikoa mama.
 
Tembelea wilaya mpya zilizoundwa, uone balaa lake, hawana hata pesa ya kununulia magari mafuta.
 
Sasa uanzishwe mkakati wa kupunguza idadi ya Wilaya na Mikoa ili kubana gharama za uendeshaji ambazo sasa zimeilemea sana hii Serikali.
 
Nashauri tuwe na majimbo tu za kikanda tupunguze utitiri wa mikoa mf. Kanda ya pwan:(DAR,PWANI,MORO),Kanda ya Kaskazini(ARUSHA,,KILIMANJARO.MANYARA,TANGA)KANDA YA ZIWA(MWANZA,MARA,SHY,KAGERA,GEITA NA SIMIYU) kanda ya kati(DOM,SINGIDA,TABORA) ETC.
 
Wakati wengine tunapigania bajeti ya utawala ipunguzwe na matumizi yasiyo na tija yasiwepo, wengine mnatamani wilaya na mikoa iongezwe!

Maana yako mleta hoja ni kuwa Wakuu wa Mikoa waongezwe, Wilaya ziongezwe, Wakuu wa polisi mikoa na wilaya waongezwe! Pole zako.
 
Kweli imekizi vigezo? Pengine kahama ila masasi no naijua vema bado kidogo.
 
Kahama ina hadhi gani ya kuwa mkoa, hizo barabara 3 za lami au?wilaya zake ziwe zipi?
 
Hizi wilaya zimekamilika kila kitu milishangaa sana uliulipounda mikoa kama njombe katavi,simiyu wakati haijazifikia wilaya tajwa kila sekata.
Pia nashauri kuongeza ufanisi wilaya za kibaha bagamoyo zizihamishiwe katika mkoa wa dar es salaam, mkoa wa pwani ubaki na rufiji,mkuranga mafia na kisarawe kwani kwa salsa inaleta mkanganyiko,

Nipe sifa za Masasi kuwa mkoa.
 
Back
Top Bottom