Ombi - Kamanda Sirro wasaidie wakazi wa Keko - Machungwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,562
217,900
Naomba kuweka wazi kwamba mimi ni Mkazi wa Tandika Mwembe Yanga lakini nina nyumba kwenye kijiji hiki cha Keko Machungwa , ni nyumba yenye wapangaji wawili.

Kwa miaka yote tangu nipate akili kijiji hiki kimezungukwa kwa karibu pande zote na kambi ya polisi ( POLICE BARRACKS ) , Hii ni kuanzia Shule ya msingi Mgulani , Mchomba line hadi Police Signal, maeneo ya Keko Akida kuelekea Kurasini Mivinjeni.

Njia pekee ya kupita ili ufike Kituo cha Daladala cha karibu (CHA POLISI UFUNDI) kwenye barabara ya Kilwa ni kupita katikati ya Kambi hii , hii ndio njia pekee iliyo salama na rahisi kwa wakazi wa eneo hili kuweza kufika kwenye maeneo yao ya kazi na yenye kuwapatia riziki , Ikiwa ni pamoja na wanafunzi.

Taarifa za hivi sasa zinasema kwamba Njia hiyo sasa imewekewa Masharti mazito sana ili kupita.

Kwamba hairuhusiwi tena kupita baada ya saa 4 usiku na kwa asubuhi ruksa ya kupita hapo ni baada ya saa 1 asubuhi, hii ni kazi ngumu sana kwa wakazi wa eneo hilo ambao kiukweli ni wa kipato cha chini kinachopatikana kwa kuvuja jasho, wengi ni wauza nyanya, wauza chips, mama lishe, ambao huondoka kwao alfajiri na kurudi usiku wa manane, sasa wakichelewa kurudi dhahama wanayokutana nayo ndani ya kambi ni nzito mno, Kamanda wasaidie watu hawa njia ya kupita kwenye kambi hii maana ndio njia pekee na kwa miaka yote wameitumia bila madhara yoyote yale (wasaidizi wako wanalijua hili)

Mateso wanayoyapata watu hawa tangu utaratibu huu uwekwe si madogo , Natambua umuhimu wa kudumisha usalama ndani ya kambi lakini kwa watu wa Keko Machungwa ambao kwa miaka mingi wamekuwa walezi na walinzi shirikishi wa kambi , Ustaarabu wako unahitajika sana.

Natanguliza shukrani.
 
Kamilisha habari, weka hayo masharti. Isije kuwa ni masharti ya kawaida tu ya kupita kwa mtu.
 
Nimeikamilisha mkuu .
Kumbe sharti lenyewe moja tu....muda wa kutumia njia. Anyway tuombe wasikie kilio chao, ila hata mimi kama ningekuachia njia katikati ya kiwanja changu nisingekuruhusu upite muda wowote kwasababu za kiusalama.
 
Serikali ivunje nyumba za watu njia mbadala ipatikane. Wakulaumiwa ni wananchi mliojenga eneo ambalo halijapimwa na mna serikali za mtaa zimewaachia muendelee kujenga tuu. Na maeneo hayo ndio kuna group za vibaka kama ukoko wa chai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole mno mtoa hoja wewe na waathirika wengine,binafsi nimeshaitumia sana hiyo njia;please waombe serikali ya mtaa wakawaone makamanda wa kile kituo cha polisi na waongee how to resolve that issue,mkimshirikisha mbunge wenu itakuwa bora zaidi,ikishindikana fungueni kesi mahakamani dhidi ya kituo hicho maana ni wajibu wao kisheria kulinda raia na mali zao sasa kama wao wanaogopa au kuona maisha yao yapo hatarini kuruhusu raia kupita hapo saa 8usiku what about citizens?lini tutafikia maisha ya polisi kukusindikiza hadi nyumbani kwako?kukusaidia kuendesha gari hadi kwako ?maana ni wajibu wa polisi wote kuwa na driving licences,tanzania hili tumeliweka chini ya zuria,unapoomba kazi ya upolisi lazima uwe na driving licence.good luck
 
Asante sana mkuu .
 
Back
Top Bottom