Ombi: Kabla hujamaliza uongozi wako mhe. Rais, tunaomba utupatie azimio mbadala wa Azimio la Arusha

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
1,159
Points
2,000

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
1,159 2,000
Mara baada ya kumaliza kusikiliza mazungumzo uliyofanya na baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania 07/06/2019 na kuona malalamiko mengi ya serikali kwa wafanyabiashara, na ya wafanyabishara kwa mamlaka ya serikali yalionesha kuna ombwe kubwa la utendaji, nidhamu na uwajibikaji hapo ndipo nikawaza kusoma tena azimio la Arusha.

Katika kusoma huko nikaweza pia kusoma maoni ya Mwalimu Nyerere juu ya azimio la Arusha. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa namnukuu’ nimelisoma na kulisoma azimio la Arusha na sikuona mahali popote palipo na tatizo juu ya Azimio hilo. Tatizo pekee ambalo ninaweza kulisema ni la kanuni la uandishi na kukosea kuweka nukta na alama nyingine mahali panapohitajika’. Maneno hayo yalisemwa zamani sana ila mpaka leo bado yanaishi na azimio la Arusha kuendelea kuwa ni azimio bora la wakati wote la misingi, maadili na nidhamu.

Azimio la Arusha nina hakika kama lingeendelea kuwepo mpaka leo lingetibu hiyo kansa ya nidhamu, maadili na misingi ambayo imekuwa ikiendelea kulitafuna taifa na kuwa kikwazo cha wewe Mhe.Rais kuwatumikia wananchi. Kutokana na mahitaji ya muda na wakati, tunaona kuwa azimio la Arusha la wakati ule haliwezi kutumika mpaka sasa ila nina amini kutokana na azimio lile tunaweza kupata azimio mbadala la kudumu hata miaka 100.

Ombi

Mhe.rais tunaomba kabla ya kumaliza uongozi wako utuachie mbadala wa azimio la Arusha ambalo litakuwa na kazi ya kuendeleza kwa juhudi ileile misingi, nidhamu na maadili yaliyokuwepo kwenye azimio la Arusha na ambayo kwa bidi kubwa unatamani irudi.

Nina imani kwamba kwa kushirikiana na wajamaa kama mzee Mangula na Katibu mkuu wa CCM taifa Ndgu Dkt. Bashiru Ally mkawa ni njia ya kufikia adhma ya nchi kurudi katika misingi iliyokuwepo.

Maoni ya wanazuoni wengi wakubwa na wewe mwenyewe mara nyingi nimekuwa nikiwasikia wakilala mkitaka azimio la Arusha lirudi liwe ni tiba ya uongozi, maadili na nidhamu. Kwa kushirikiana nao, ninayo imani utapatikana mbadala wa Azimio la Arusha.

Faida za Azimio mbadala
  • Azimio mbadala litakuwa ni tiba ya kujenga uzalendo mzuri kwa watu, kwa nchi na Rasilimali zake

  • Azimio mbadala litakuwa ni chachu ya kuzalisha, kukuza na kudumisha uzalendo na utaifa

  • Azimio mbadala litaonesha njia na dira ya maendeleo yetu kwa miaka na miaka mingi ijayo
Hitimisho

Tuwe na azimio mbadala wa lile la Arusha ili maadili, nidhamu na misingi yarudi ambayo itakuwa msaada katika kujenga nchi ya uchumi wa kati.
 

Forum statistics

Threads 1,379,930
Members 525,627
Posts 33,761,374
Top