Ombi: Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi: Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fasta fasta, Apr 29, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu wanajf ninawasalimia wote kwa ujumla,
  Ndugu zangu sio nia yangu kueleza kilichotokea ila inanibidi kutokana na maana ya neno kaka jinsi lilivyo na maana kubwa katika kiswahili. Hili neno kaka lina maana nzuri sana kwa kiswahili na katika kufikisha ujumbe, lakini kutokana na media ilivyopanuka na kufanya dunia kama kijiji ikiwa na maana kila mtu anataka kusikiliza lugha ya mtu mwingine, unakuta ujumbe unawakwaza wengine kutokana na wengine kutumia neno hilo kama linavyotamkwa na linavyoandikwa ili kufikisha ujumbe wao pia. Na lugha ya kiswahili inapambana na lugha nyingine ili na wao waweze kuonja utamu wa lugha yetu ya kiswahili.

  Hili neno kaka siku moja lilileta mzozo mkumbwa sana kati ya mwitaliano na mtanzania, ikiwa na maana matanzania alimwita huyu jamaa wa kitaliano kaka yangu. Mtaliano alikuja juu kwa hasira kwa sababu kaka kitaliano halina maana nzuri. Kwa wale wenzangu wanaojua maana ya hili neno kitaliano wanaweza kutujuza zaidi ili kushauri hili neno libadilishwe. Na maana ya hili neno kutumika kwa kila mtu bila uoga au kumuudhi mtu yeyote. Samahani sana ndugu zangu kwa wale watakao nielewa vibaya lakini nina maana nzuri.
   
 2. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kaka ni Mavi kwa kitaliano,
  lakini tusihangaike sana hata wahindi majina kama **** na kila lugha iende kivyake.
   
 3. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kutokana na maana ya hilo neno hainishawishi kuendelea na nalo. Kumbuka kutokana na media ya leo na ukaribu wa maana ya neno kaka katika jamii litakufa lenyewe. Sio waitaliano wenyewe wanaitumia hiyo lugha ya kitaliano ni watu wengi wanaisoma. Tukumbuke mtu kama anaanza kujifunza lugha maneno ya kwanza kukumbana nayo ni kama kaka, dada, mama nk. Sasa litampa ugumu mtu anaejua kitaliano kutumia hilo neno kaka, ni tofauti na jina la mtu. Kaka linawakilisha jamii na sio jina la mtu ndugu yangu. Ninadhani kila atakayeona maana ya hili neno hataridhika, na kuliunga mkono kuliunga mkono. Hata kulitamka sasa linakuwa ngumu.
   
 4. Analogia Malenga

  Analogia Malenga JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2015
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,093
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  ooh! Ashakumu si matusi.
  Nadhani neno K*MA lina maana nzuri kikongo, je tulisanifishe?
   
Loading...