Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,563
- 217,866
Natuma ombi hili kwa Mashirika yote yasiyo ya kiserikali , ambayo mara zote yamekuwa mstari wa mbele kulinda utu wa mwanadamu na kutetea haki za mwanamke , Jengeni shule kwa ajili ya watoto wa kike ambao kwa bahati mbaya walipata mimba wakiwa shuleni lakini bado wanayo ndoto ya kusoma .
Serikali ya Tanzania kupitia Mh Rais imekwishaweka wazi msimamo wake juu ya watoto hawa , ambao ushahidi unaonyesha kwamba wengi wao hupata mimba kwa kubakwa ama kurubuniwa kwa vitu vidogo sana kama lift za magari na bodaboda , ama hata chips kavu kutokana na umri wao kuwa mdogo kiasi cha kushindwa kujitetea wanapobakwa au kushindwa kuchanganua pale wanaporubuniwa .
Ninao ushahidi wa mtoto wa Dada yangu , ambaye alipata ujauzito akiwa kidato cha kwanza na hivyo kufukuzwa shule , lakini alikuwa anataka kuendelea na masomo , ambapo ndugu tukamsaidia na akaja kufanya mtihani kama Private candidate , yaliyoendeleaa ni historia , lakini kwa ufupi niseme tu kwamba binti huyu kwa sasa ni msaada mkubwa sana kwa familia yake .
Hakuna haja ya kutia shaka , maana Mh Rais asichokitaka ni watoto hawa kusoma kwenye shule zake tu , kwahiyo tukijenga shule zingine NECTA watatoa ushirikiano kama watoavyo kwenye shule zingine .
Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa , tuwape nafasi nyingine mabinti zetu .
Natanguliza shukrani .