Ombi - Asasi za kiraia ( NGO'S ) jengeni shule kusaidia watoto wa kike wa Tanzania

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,343
217,371
Natuma ombi hili kwa Mashirika yote yasiyo ya kiserikali , ambayo mara zote yamekuwa mstari wa mbele kulinda utu wa mwanadamu na kutetea haki za mwanamke , Jengeni shule kwa ajili ya watoto wa kike ambao kwa bahati mbaya walipata mimba wakiwa shuleni lakini bado wanayo ndoto ya kusoma .

Serikali ya Tanzania kupitia Mh Rais imekwishaweka wazi msimamo wake juu ya watoto hawa , ambao ushahidi unaonyesha kwamba wengi wao hupata mimba kwa kubakwa ama kurubuniwa kwa vitu vidogo sana kama lift za magari na bodaboda , ama hata chips kavu kutokana na umri wao kuwa mdogo kiasi cha kushindwa kujitetea wanapobakwa au kushindwa kuchanganua pale wanaporubuniwa .

Ninao ushahidi wa mtoto wa Dada yangu , ambaye alipata ujauzito akiwa kidato cha kwanza na hivyo kufukuzwa shule , lakini alikuwa anataka kuendelea na masomo , ambapo ndugu tukamsaidia na akaja kufanya mtihani kama Private candidate , yaliyoendeleaa ni historia , lakini kwa ufupi niseme tu kwamba binti huyu kwa sasa ni msaada mkubwa sana kwa familia yake .

Hakuna haja ya kutia shaka , maana Mh Rais asichokitaka ni watoto hawa kusoma kwenye shule zake tu , kwahiyo tukijenga shule zingine NECTA watatoa ushirikiano kama watoavyo kwenye shule zingine .

Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa , tuwape nafasi nyingine mabinti zetu .

Natanguliza shukrani .
 
Mnachowajengea watoto ni kitu cha hatari na ajabu sana.That they can do anything and go away with it.Hayo sio malezi mema ya watoto kabisa.Consequence ya maamuzi ya namna hiyo ni very far reaching.
 
Naunga mkono hoja, lakini pamoja na hayo, tuendelee kuibana serikali iwaruhusu kuendelea na masomo. Tatizo wabongo tunapenda kuongea bila takwimu, tujiulize tu ni watoto wa maeneo gani ambao ni wahanga wa mimba za utotoni(credit: Msando)?

Kuna mtoto wa rais au waziri amewahi kupata mimba akiwa shule? Kati ya mijini na vijijini, ni wapi hasa mimba za utotoni ni nyingi? Mikoa ipi inaongoza kwa mimba za utotoni na kwanini? Kuna ushahidi wowote kuwa walio na watoto wakirudishwa shulen hawawezi kufanya vizuri kwenye masomo? Kama aliyepata mimba akiwa shuleni anakomeshwa kwa kunyimwa fursa ya kuendelea, je na yule anayeeendelea na shule lakin mwisho wa siku anapata zero wana tofauti gani?

Serikali isikwepe jukumu lake la kutoa huduma za kijamii. Kesho tutaambiwa ukipata ajali wakati unaendesha kwa spidi kubwa hupati matibabu hospitali za serikali-uende private. Kama serikali inaona wanafunzi wenye watoto watasababisha na wengine waone kuwa na watoto ni kawaida (panahitaji utafiti, sio hisia) basi serikali yenyewe ijenge shule maalum kila wilaya kwa ajili ya wanafunzi wenye watoto. Isisakizie jukumu la elimu kwa private sector maana mtoto wa maskini anayehitaji ukombozi wa elimu hana uwezo wa kumudu gharama za private.
 
Mimi naona ile kauli ya jana ya mkulu ilikuwa yakukumbusha tu mtoto kupata mimba na kufukuzwa shule haijaanzia kwa Magu hii imekuwepo miaka nenda rudi ushahidi wa kuwepo kwake nimesoma na wadada wengi tu tokea s/primary na sec, ambao walipata mimba na wakafukuzwa shule, sasa jana mkulu kuongea, kila mtu ameshika bango na kuwa mchambuzi.
 
mimi suing mkono hoja ya kuwajengea shule yao waliopata mimba, kwa kufanya hivo utawaharibu kisaikolojia. hii ni sawa na isolation, watajiona hawana maana katika inch! naunga mkono wanafunzi waliopata mimba kuendelea na masomo katika shule za mchanganyiko na wengine!
 
Wakati mwingine ni vigumu kuwaelewa wanasiasa kwa kiwa vinavyotoka vinywani mwao.....ni vigumu kuvitaza katika ulimwengu halisi....
 
Tutumie nguvu nyingi kuwaeleza watoto madhara ya kufanya ngono kabla ya ndoa na hasa wakiwa mwanafunzi. Tuwaambie ukweli kuwa ukifanya ngono utapata mimba na utafukuzwa shule na sisi hatuna cha kufanya juu ya hilo. Tusiwalee watoto na wadogo zetu kujifariji kuwa kupata mimba ni bahati mbaya. Tuwaambie ukweli tuwasaidie.
 
Leo ukaongea madini kabisa hapa. Ila kwa navyofahamu NGOs zetu ni za kukosoa tu na hazina hata msaada wa pini ya kushonea nguo kwa wananchi.

Kule Nigeria, kumeanzishwa kitu kama hiki kwa wale walikosa shule kwasababu ya Boko Haram. Lakini ile ina support kubwa sana katika halihalisi.

Kwetu huku naona serikali inapata ukakasi wa nini tunaenda kukifanya. Shida ni kuwa unapolegeza sheria ndo wengi wanafanya kama wanavyotaka. Ndo kinachotofautisha kati ya uarabuni na huku kwetu.

Hii inatokana na umasikini wetu.
 
Mtu anangozwa anakubali
Anaenda Nae mpaka analala naye
Huku anaelewa kuwa ni mwanafunzi

Ukipanda mihogo
Usitarajie Kuvuna mahindi
 
Hiyo ni Fursa mpya ya kuanzisha shule maalumu, sasa zitajengwa kila sehemu, subiri uone watanzania walivyochangamka,
 
Naunga mkono hoja, lakini pamoja na hayo, tuendelee kuibana serikali iwaruhusu kuendelea na masomo. Tatizo wabongo tunapenda kuongea bila takwimu, tujiulize tu ni watoto wa maeneo gani ambao ni wahanga wa mimba za utotoni(credit: Msando)?

Kuna mtoto wa rais au waziri amewahi kupata mimba akiwa shule? Kati ya mijini na vijijini, ni wapi hasa mimba za utotoni ni nyingi? Mikoa ipi inaongoza kwa mimba za utotoni na kwanini? Kuna ushahidi wowote kuwa walio na watoto wakirudishwa shulen hawawezi kufanya vizuri kwenye masomo? Kama aliyepata mimba akiwa shuleni anakomeshwa kwa kunyimwa fursa ya kuendelea, je na yule anayeeendelea na shule lakin mwisho wa siku anapata zero wana tofauti gani?

Serikali isikwepe jukumu lake la kutoa huduma za kijamii. Kesho tutaambiwa ukipata ajali wakati unaendesha kwa spidi kubwa hupati matibabu hospitali za serikali-uende private. Kama serikali inaona wanafunzi wenye watoto watasababisha na wengine waone kuwa na watoto ni kawaida (panahitaji utafiti, sio hisia) basi serikali yenyewe ijenge shule maalum kila wilaya kwa ajili ya wanafunzi wenye watoto. Isisakizie jukumu la elimu kwa private sector maana mtoto wa maskini anayehitaji ukombozi wa elimu hana uwezo wa kumudu gharama za private.
Hilo LA kuendelea kuibana serikali waruhusu wanafunzi kuendelea na masomo akiwa amejifungua
Nikuwajengea watoto wet mazingira yakufanya ngono

Wakiruhusu Hilo
Serikali iondoe adhabu ya kwenda jela
Aliyempa mimba mwanafunzi
 
Mnachowajengea watoto ni kitu cha hatari na ajabu sana.That they can do anything and go away with it.Hayo sio malezi mema ya watoto kabisa.Consequence ya maamuzi ya namna hiyo ni very far reaching.
Hujui mleta mada alilelewaje na wazazi wake humu jamii forums kuna watu wamelelewa wengine hovyo tu. Hawajakulia mikononi mwa familia zenye maadili
 
Mnachowajengea watoto ni kitu cha hatari na ajabu sana.That they can do anything and go away with it.Hayo sio malezi mema ya watoto kabisa.Consequence ya maamuzi ya namna hiyo ni very far reaching.

Mkuu unaonaje tukipitisha sheria ya kuharalisha utoaji mimba kwa watoto na wanafunzi watakao amua au Yoyote atakaye mpa mimba mtoto/mwanafunzi auawe maana kusibitisha ni rahisi siku hizi aonewi mtu ni DNA tu.

Maana wapatao mimba sio wote wametaka kwa hiyari yao. wengine wamebakwa na kutishwa.
 
Hilo LA kuendelea kuibana serikali waruhusu wanafunzi kuendelea na masomo akiwa amejifungua
Nikuwajengea watoto wet mazingira yakufanya ngono

Wakiruhusu Hilo
Serikali iondoe adhabu ya kwenda jela
Aliyempa mimba mwanafunzi
Kwani huwa hawafanyi ngono? Wabunge na mawaziri wana wake zao nyumbani, lakini bado wanachepuka, tena na machangudoa-sembuse watoto ambao hawajakomaa kiakili? Tutunge na sheria kuwa mbunge akizini asiendelee na ubunge.
 
Natuma ombi hili kwa Mashirika yote yasiyo ya kiserikali , ambayo mara zote yamekuwa mstari wa mbele kulinda utu wa mwanadamu na kutetea haki za mwanamke , Jengeni shule kwa ajili ya watoto wa kike ambao kwa bahati mbaya walipata mimba wakiwa shuleni lakini bado wanayo ndoto ya kusoma .

Serikali ya Tanzania kupitia Mh Rais imekwishaweka wazi msimamo wake juu ya watoto hawa , ambao ushahidi unaonyesha kwamba wengi wao hupata mimba kwa kubakwa ama kurubuniwa kwa vitu vidogo sana kama lift za magari na bodaboda , ama hata chips kavu kutokana na umri wao kuwa mdogo kiasi cha kushindwa kujitetea wanapobakwa au kushindwa kuchanganua pale wanaporubuniwa .

Ninao ushahidi wa mtoto wa Dada yangu , ambaye alipata ujauzito akiwa kidato cha kwanza na hivyo kufukuzwa shule , lakini alikuwa anataka kuendelea na masomo , ambapo ndugu tukamsaidia na akaja kufanya mtihani kama Private candidate , yaliyoendeleaa ni historia , lakini kwa ufupi niseme tu kwamba binti huyu kwa sasa ni msaada mkubwa sana kwa familia yake .

Hakuna haja ya kutia shaka , maana Mh Rais asichokitaka ni watoto hawa kusoma kwenye shule zake tu , kwahiyo tukijenga shule zingine NECTA watatoa ushirikiano kama watoavyo kwenye shule zingine .

Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa , tuwape nafasi nyingine mabinti zetu .

Natanguliza shukrani .
Kwa nini chadema na Lowassa msijenge kwanza ili muweze kumkosoa vizuri Magufuli na hivyo kupata fursa ya kumletea mtikisiko mwaka 2020?
Nadhani hii ndiyo golden chance kwa chadema na Lowassa kumuonesha Magufuli wka vitendo kwamba mnaweza na hivyo kuwashawishi wapiga kura 2020.
 
Hiyo ni Fursa mpya ya kuanzisha shule maalumu, sasa zitajengwa kila sehemu, subiri uone watanzania walivyochangamka,
Hiyo fursa labda mikoa ya pwani ambako wali kibao hupata mimba kuliko eneo lolote la nchi. Tatizo hata wakijenga hawatakuwa na wateja wengi kwani hao wali hujipatisha mimba kwa kuwa hawataki shule. Kwa hiyo hata wajenge watakosa wanafunzi wa kutosha.
 
Mkuu unaonaje tukipitisha sheria ya kuharalisha utoaji mimba kwa watoto na wanafunzi watakao amua au Yoyote atakaye mpa mimba mtoto/mwanafunzi auawe maana kusibitisha ni rahisi siku hizi aonewi mtu ni DNA tu.

Maana wapatao mimba sio wote wametaka kwa hiyari yao. wengine wamebakwa na kutishwa.
From bad to worse,kutoa mimba tena!Binti akishapata mimba akubali consequences za umalaya wake.Aibebe mpaka azae.Akiitoa,akikamatwa,sheria itachukua mkono wake.Hatuwezi kuruhusu murder.Na kosa la kupachika mimba lina adhabu yake kisheria,why should we beat around the bush.It is thirty years if convicted by a court of law.

Halafu hili swala la oh, wamebakwa,oh,sio hiari yao,mbona mnapenda kulitumia sana kuhalalisha 'en masse' upuuzi huu.Jamani ni wangapi wanabakwa?Such cases if proved,can be dealt on a case to case basis,sio shida,ila hatuwezi kuhalalisha upuuzi kwa sababu hiyo.Halafu swala la oh,sio hiari yao, is nonsense.Hivi mtu anatongozwa,anaongoza mwenyewe kwenda,porini,ghetto au gesti, halafu mnasema eti sio hiari yake?!Haingii akilini.Tunaomba msiwasemee hawa wasichana kwa nia mbaya ya kuhalalisha uovu.
 
Back
Top Bottom