Ombi: Ajira TANESCO zipitie Public Sec. Recruitmnent, wengi wameingia kwa kubebwa

Tanesco wakitangaza ajira,ukienda unaambiwa nafasi zimeshajaa wakati ata 48 hrs haijaisha tokea watangaze.. ! Sadly
Ni kujuana mwanzo mwisho..ushaidi uko wazi kwa wenye macho
siyo kweli! Mimi niliitwa kwenye usaili na nikashindwa mwenyewe.Wewe toa ushahidi hapa
 
Mfumo wa kuajiri watumuishi katika shirika la umeme Tanzania(TANESCO) ni mbovu, usiofuata misingi wala utaratibu maalum. Tanesco kupewa uwezo wa kuajiri wenyewe imekuwa shida kwao kwani watu wengi wameajiriwa kwa mashinikizo ya wakubwa katika shirika. Naomba serikali ipeleke ajira zote za TANESCO Katika sekretarieti ya ajira ya Taifa. Unakuta shirika linaajiri watu ili kufanya kazi flani lakini hawana uwezo hasa katika kazi za kiufundi.

Taarifa zinasema huko mokoani ndo uozo umejaa, kwani unaweza kukuta meneja ameajiri familia yake nzima na ni watumishi wa eneo husika , jambo kama hili linapunguza ufanisi wa kazi.

Pia promotion za TANESCO Nyingi zimekuwa ni za kujuana, unakuta mtu ana masters , ana PHD lakini hapandi cheo. Matokeo yake mameneja wengi hasa wa mikoani na wilayani wana elimu ya diploma tu, Serikali iangalie sana suala hili, kwani linaleta kuvunjana moyo mtu ana mdegree, masters na ni mtendaji mzuri, inakuaje mtu mwenye elimu ya diploma ndo apewe umeneja. Mambo ya TANESCO ni ya ajabu sana.
Ushauri huu ni mzuri sana. Ni kweli serikali inapaswa
kuangalia swala la ajira TANESCO upya,pameoza kabisa.Hii itasaidia kuongeza ufanisi.Hata hivyo tatizo hili lipo katika Institutions zingine na itakuwa busara kama litaangaliwa kiundani kila mahali. Previous governments were very lousy.
 
Back
Top Bottom