Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 3,985
- 2,770
Watu maskini huwa wanaongea mengi sana juu ya waliofanikiwa. Hivi mwajiriwa kama ana sifa na anaweza kazi kuna haja gani ya kumfanyia categorization ya uliyoyataja hapo juu? Nchi zilizoendelea maoni ya kugawa kama haya hakuna. Marekani Bush baba Rais tena alichaguliwa, akaja Bush mtoto rais tena wa kuchaguliwa, Bush mtoto Gavana wa kuchaguliwa haya maneno ya ukanda, ukabila, udini, familia wenzetu hawajali wanajali uwezo wako tuu! Mama Clinton naye mke wa Rais wa Zamani naye alipigiwa kura nyingi tu awe rais pamoja na kwamba mumewe alishawahi kuwa rais. Hakukosa kura eti kwa vile ni Clinton wife. Mimi naona ifike mahali watu waajiriwe kwa sifa na uwezo wao siyo kuwanyima kwa ukabila,Undugu, ukanda, udini. Tuache kugawanyika kwa misemo hii. Halafu hivi kama mimi nina wadhifa sehemu kuna fursa ndugu, mtoto ana sifa kwa nini nisimpe? Wakose kwa kuwa nina mahusiano nao? Faida yangu kwao ni nini kama siyo kuwabeba? Ila kama hana sifa simpi!Uozo wa namna hii upo kwenye public/ government institutions nyingi.
Nenda kila mahali kupo ivyo ivyo
Undugu, ukanda, ukabila, udini kwenye ajira ni janga kubwa.