Ombaomba huyu ashughulikiwe

buguruni

Member
Feb 5, 2010
22
2
Kuna ombaomba mmoja kijana ambaye hupenda kuombea katika taa za salender, peugeot house na mktaba anakera kwa staili yake ya kufunua kidonda kikubwa kwenye paja lake la kushoto akidai anataka msaada wa matibabu.

Kidonda hicho ni kikubwa sana kilicho fresh na bila kujua watu wengi hawapaendi kuona damu.

Kwa kumbu kumbu zangu huyu bwana ana kidonda hicho miaka mitano anacho na sijui anakifanya nini kisipone.

Kidonda kageuza mtaji.

Vyombo vya dola hamlioni hilo?
 
Ungekuwa unasoma threads usingeirusha hii!!
 
Ni kweli huyo jamaa hata mie nimemuona kwa muda mrefu. Kwa kweli kidonda chake kinatisha. Kuna siku nilimwambia aende akatibiwe badala ya kuendelea kukifanya kidonda kuwa dili ya kupatia pesa.
 
Kwanini hujapeleka malalamiko yako polisi?
Mi naona kama unaitwisha jf jukumu ambalo si lake.

Hivi wewe umeshawahi kuendaga vituo vya polisi kutoa malalamiko ukaona mambo yalivyo. Kwa taarifa yako kuna siku nimesharipoti hapo jirani tu na anapoombea Salender Bridge na wakasema watashughulikia na mpaka leo yupo.

Unaposema naitwisha JF mzigo si wake una maana gani? mizogo yake ni ipi? nafikiri si kila tread unatakiwa utoe maoni kama huna cha kusema kuhusu hilo ipotezee.
 
Ni kweli huyo jamaa hata mie nimemuona kwa muda mrefu. Kwa kweli kidonda chake kinatisha. Kuna siku nilimwambia aende akatibiwe badala ya kuendelea kukifanya kidonda kuwa dili ya kupatia pesa.

Mpelekeni Hospital
 
Hii inanikumbusha kuna kijana alikuwa anakuja chuo(enzi hizo tupo pale mlimani) na barua yake ya mwenyekiti akiomba asaidiwe ada ya kujiunga na form one ..cha ajabu tangu nippo 1st yr hadi nafika 4th yr kijana anakuja kuniomba ada ya kuingia form II!...

Huyo Omba omba aende makanisani kule kuna watu wanatoa sadaka..watamjumlisha na yeye pia atapata na maombi!
 
he he he he hizi style za ombaomba hizi kwanza ni kero kama ile manyoyaaaaaaaa,lakini pia hiii ya mavidonda hawa dawa yao ni kukicharaza bakora kidond chenyewe kama anakitumiaa kupata hela ili kiwe mbichi kila siku apate zaidi
 
Hii inanikumbusha jamaa mmoja Arusha nae analikidonda upande wa kushoto wa ubavu wake ni kama vile utumbo uko nje huwa anafunika na mfuko wa plastiki kwa madai kuwa kinyesi kinatokea hapo. Lakini cha ajabu ni muda mrefu tangu nimuone na hilo tatizo akiombaomba mpaka nilimuuliza kuwa tangu anze kuomba hajapata tu pesa ya matibabu? Tena huyu mpaka ananuka...hata kama ndio mradi sidhani kama una maslahi....mh!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom