binti wa kirombo
JF-Expert Member
- May 17, 2016
- 847
- 959
Waungwana natumaini mnaendelea vyema na majukumu yenu ya ujenzi wa Taifa na wale mlioko mapumziko mkisherekea sikukuu ya Muungano hongereni.
Hebu fikiri umeachishwa kazi ghafla bi vu yaani siunajua makampuni mengi yalijinadi yanapunguza watu kazini kwasababu ya hali mbaya ya kiuchumi hapo una kamkopo SACCOSS labda kalikuwa kaishe julai hivi na ulikopa kwa ajili ya kumalizia kaujenzi kako ili angalau huu mwaka ukiisha uende kwako.
Hapo umepata kabarua kutoka kwa wale maafisa waajiri bwana au bibi Fulani wewe ni miongoni mwa ile asilimia kadhaa aliyoisema baba mwenye mbwa kila stahiki yako itafanyika kulingana na sharia ya ajira kwa tabasamu pana unawajibu sawa.
Mbali na hapo upo kwenye mahusiano na jamaa yako ukifikiria atakuwa faraja kwako lakini inakuwa kinyume chake unampigia simu ili umuelezee yale yaliyojiri wala hapokei wala kukutafuta hukati tamaa siku inayofuata unamtafuta unaongea lakini hapo unakuwa na hasira unachofanya ni uamuzi wako.
Hapo unaamua kujitoa mbuzi wa kafara uishi wewe kama wewe Maana Mungu akiwa upande wako ni nani aliye juu yako?
Hapo unamshukuru Mungu kwa nanmna ya kipekee wakati ule unaajiriwa ulikutana na vijana wenye maono ya maisha ..wakakutonya kuwa hawa wenye mbwa hawaeleki kulingana na mkataba wao kimini hapa ni kuwa na akili wekeza nje ya kazi…hapo swali linakuja nitapata wapi mtaji? Wanakujibu tuna mshikaji wetu anakopesha ila ana riba kidogo hata wew unaweza rejesha..kwanza hakikisha unakopa ukiwa na wazo la biashara gani unataka kufanya ..Baada ya miezi mitatu nikajifunga nikakopa nikafungua biashara ya kwanza huku nikiwa na hofu ila vijana wenye vision walinitoa hofu baadae niliona faida yake nikafungua la pili…na mafanikio mengine mengi.
Sasa hao wenye mbwa kunipunguza mimi wakifikiria labda ningdondosha chozi kama wengine wala leo sura ni ya kutabasamu naenda kusimamia miradi yangu……
Usije kubweteka pale unapopata ajira halafu ajira yenyewe inasema mkataba wako ni kimini (temporal or renew after one or two years) hata wale wa mkataba wa milele (permanent) fungua kitu kingine kikuingizie kipato mbali na mshahara.
Ni hayo tu kwa leo