Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,760
- 730,014
Ni kitu cha kusikitisha unakutana na mtoto mdogo anaomba hela au bibi kizee aliyejichokea kabisa...unaingiwa na imani unazama mfukoni unampa ulichonacho huku ukitafakari kuwa aliyekupa wewe ndie kamnyima yeye...hii ni roho ya upendo mkuu.
Lakini nyuma ya pazia kuna kitu kibaya kabisa kuhusu habari nzima ya omba omba......Omba Omba ni kazi rasmi inayowaingizia watu kipato kikubwa tuu...wale watoto ni chambo tuu wanatumikishwa na wakubwa kwa ujira hafifu....na hata wale watu wazima ni watu wenye uwezo tu huko wanakotoka!hii inakufanya ujiulize hivi hii ni mila?
Cha kushangaza zaidi ni baadhi tu ya mikoa na maeneo ndiko ambako hutoka Omba Omba wengi..vigumu sana na pengine hakuna mchaga mpare au mhaya Omba Omba.
Tunaliangalia hili kwa jicho la ndani ya nchi lakini kama taifa pia tumevizwa na tabia hii mbaya ya kuwa omba omba kimataifa...tuna kila kitu kinachoweza kutufanya tusitegemee misaada ya wahisani, lakini kila leo tunanyenyekea na kupewa misaada ya masharti magumu! Huu ni utumwa mbaya kabisa..hivi kama taifa tuna tofauti gani na Matson ya RIP yule Omba Omba maarufu aliyekuwa na mali za kutosha tu huko kwake Dodoma?
Ukiishi kutegemea misaada hutakaa ukomboke kamwe utalemazwa akili na hutakaa uwaze kupata chako kwa akili na juhudi zako...utakuwa mtumwa milele.
Kampeni ya kuwaondoa Omba Omba kwenye viunga vya jiji la Dar inapokaribia nasi kama taifa tujitathmini kama ilikuwa ni sahihi kulilia pesa za MCC na likafanywa ni jambo kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.
TUMETIA AIBU KUBWA