OMARILYAS na Baraza la Mawaziri la JK Vs Matumizi

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,970
Ndugu wanJF,
Jana katika kipindi cha tuongee asubuhi cha startv, kulikuwa na mjadala kuhusu baraza la mawaziri lililoundwa na Rais JK hivi karibuni.
Kulikuwa na wachangiaji watatu studio ya mwanza akiwemo Singo Kigaila wa cdm, Kerebe Lutele kada wa ccm na mwingine wa tatu.Studio ya Dsm walikuwepo mwanaharakati Bw. Marcus Albano na mwanaJF Omarilyas.

Kwa ujumla watu wote walikubaliana kwamba baraza la mawaziri la JK ni kubwa sana na uendeshaji wake utachukua karibia takribani 80% ya bajeti, wakati bajeti ya maendeleo inakuwa ni takribani 20%. Bw. Omarilyas na mwenzake Kerebe pamoja na kukubaliana na hoja ya ukubwa wa baraza wao wakasema inatokana na mahitaji ya wakati huu kitu ambacho walishindwa kukithibitisha.

Jambo moja ambalo binafsi lilinishangaza ni pale bwana Omarilyas alipodai kwamba baraza la mawaziri linaweza kuwa kubwa lakini matumizi yakawa madogo, akitolea mfano kwamba kunaweza kuwa na baraza la mawaziri lenye watu 100 wakawa na matumizi madogo sawa na baraza la watu 50.

Swali ambalo nilikuwa najiuliza na ambalo ningependa wanajamvi wenzangu tushirikishane kufahamishana ni hili; kwamba inawezekanaje kuwa na baraza kubwa la mawaziri lakini tukatumia fedha kidogo kwa shughuli za uendeshaji katika nchi kama yetu ambayo tumeelezwa kwamba magari waliyokabidhiwa juzi mawaziri baada ya kuapishwa yameigharimu serikali kiasi cha Tsh. 9.3 bilioni. Je ni kweli kwamba chini ya serikali ya JK na ccm tunaweza kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha? Je chini ya serikali ya JK na ccm wanaweza kuelekeza fedha nyingi za bajeti katika maendeleo kwamfano 50% ikaenda kwenye miradi ya maendeleo?

Wadau naomba mawazo yenu.
 
ndugu wanjf,
jana katika kipindi cha tuongee asubuhi cha startv, kulikuwa na mjadala kuhusu baraza la mawaziri lililoundwa na rais jk hivi karibuni.
Kulikuwa na wachangiaji watatu studio ya mwanza akiwemo singo kigaila wa cdm, kerebe lutele kada wa ccm na mwingine wa tatu.studio ya dsm walikuwepo mwanaharakati bw. Marcus albano na mwanajf omarilyas.

Kwa ujumla watu wote walikubaliana kwamba baraza la mawaziri la jk ni kubwa sana na uendeshaji wake utachukua karibia takribani 80% ya bajeti, wakati bajeti ya maendeleo inakuwa ni takribani 20%. Bw. Omarilyas na mwenzake kerebe pamoja na kukubaliana na hoja ya ukubwa wa baraza wao wakasema inatokana na mahitaji ya wakati huu kitu ambacho walishindwa kukithibitisha.

Jambo moja ambalo binafsi lilinishangaza ni pale bwana omarilyas alipodai kwamba baraza la mawaziri linaweza kuwa kubwa lakini matumizi yakawa madogo, akitolea mfano kwamba kunaweza kuwa na baraza la mawaziri lenye watu 100 wakawa na matumizi madogo sawa na baraza la watu 50.

Swali ambalo nilikuwa najiuliza na ambalo ningependa wanajamvi wenzangu tushirikishane kufahamishana ni hili; kwamba inawezekanaje kuwa na baraza kubwa la mawaziri lakini tukatumia fedha kidogo kwa shughuli za uendeshaji katika nchi kama yetu ambayo tumeelezwa kwamba magari waliyokabidhiwa juzi mawaziri baada ya kuapishwa yameigharimu serikali kiasi cha tsh. 9.3 bilioni. Je ni kweli kwamba chini ya serikali ya jk na ccm tunaweza kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha? Je chini ya serikali ya jk na ccm wanaweza kuelekeza fedha nyingi za bajeti katika maendeleo kwamfano 50% ikaenda kwenye miradi ya maendeleo?

Wadau naomba mawazo yenu.

mmh sidhani
 
Hii nchi kuna kuna watu wanapiga pesa sana...........................
 
Kama Omarilyas hakuweka ufafanuzi wowote runingani basi hapa ndo jukwaa la kutuletea huo uyakinifu wa baraza kubwa na matumizi madogo.
Kuna watu nchi hii hawajui nini maana ya neno shida
 
The man is serios with his appointment. He knows exactly what to do. That is his life. OMAR ILYAS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kama Omarilyas hakuweka ufafanuzi wowote runingani basi hapa ndo jukwaa la kutuletea huo uyakinifu wa baraza kubwa na matumizi madogo.
Kuna watu nchi hii hawajui nini maana ya neno shida

Kweli kabisa kamanda, hapa anweza kufafanua ni namna gani serikali kubwa ya JK inavyoweza kuwa na matumizi madogo ili bajeti kubwa ielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom