Omari Nundu, TIC, Pinda...nendeni Lamu Kenya muone

Pinda na Nundu waende Lamu kujifunza?? thubutu

Ingekuwa safari ya kwenda Uholanzi kuangalia Land areclamation scheme wangeenda fasta japokuwa haina uhusiano wowote na maendeleo ya Tanzania. Bandari ya Dsm congestion, wizi, innefficiency ya hali juu hapo bandarini ukiachilia rushwa na uzembe.

Mungu ibariki Tanza-near
 
Ni wakati muafaka sasa wabongo kujikubari na kuona fursa zilizoko kwetu kuliko kuona yanayookea Kenya ndio mazuri zaidi kuliko kwetu. Sie mbona tunampango mkubwa kuliko huo banadari ya bagamoyo na mtwara mbona utekelezaji ushaanza na Kigamboni city.

Mie nmeona barabara ya namtumbo kuunganisha bandari ya mtwara na malawi/zambia na mozambique huko mbele, Congo inaunganishwa kupitia sumbawanga badala ya kupita kapwili/Kitwe mpaka kasumbalesa ili kupunguza umbali na congo.

Construction works ya Namtumbo nimewakubali jamaa wanamitambo ya ukweli sio magumashi kwa hiyo wako fasta na quality. Lamu ndio wanatakiwa kujifunza kutoka kwetu labda tu bongo watu hawatoi taarifa nzuri, kuna bandari lake Tanganyika ya ukweli ijapokuwa mtoto wa mkulima kajipigia ndefu lakini tutafaidika wote
 
sitegemei mabadiliko ya maana kupitia ccm, hata kenya KANU walipigwa chini kwanza
 
Wataunda tume ya kufanyia kazi madai yako then wataingia kwenye mchakato kisha wataleta taarifa ndo mfumo wa kutenda kazi nchi hii ila ACTION hatuwezi tunachoweza ni maneno ya kuwadanganya watz basiiiiii
 
Back
Top Bottom