Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu

Mfutakamba kesho Naye anaita press conference kukanusha tuhuma za Nundu! Wonders shall never end

Alichosema Nundu ni aibu katika mfumo wa utendaji kazi serikalini. He has to go. Ila kama Mfutakamba naye akianza kushindana naye, hatutaona tofauti kati yao, bali anatakiwa kuwa na busara zaidi.
 
Ana matatizo mengine kabisa ambayo nina uhakika hakuzungumzia. Je amezungumzia dhulma aliyotaka kuifanya KIA? _
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Nundu ameluzungumza la Kia alipokuwa EA amefight wamejenga hanger ya service ya ndege kubwa na nyumba kadhaa za wafanyakazi, tangu alipoondoka waliobaki waka abandon ili service zikafanywe nje, watu wale miposho ya dola!.

Uwanja umekondishwa kwa mwekezaji anayelipa peanut serikalini!. He had to stop that nonsense!. Amedai angekuwepo yeye ATCL isingekufa, angeiingilia mpaka chooni!.

Kama cost ya mradi ni US $ less than 200 milions kwa nini wakope 600?. Approach yake ni kutumia PPP!.
 
Alichosema Nundu ni aibu katika mfumo wa utendaji kazi serikalini. He has to go. Ila kama Mfutakamba naye akianza kushindana naye, hatutaona tofauti kati yao, bali anatakiwa kuwa na busara zaidi.

Ha ha ha ha ha ha ha! Halafu kwa hali hii eti mawaziri hawatajiuzulu! Kweli? Mnataka kitokee nini ndipo wajiuzulu au wafukuzwe? Kweli mfumo wa serikali yetu uko ICU kuliko tunavyodhani. Halafu kesho Waziri na Naibu wake wote watakuwa ofisini na kufanya kazi kwa pamoja? Ha ha ha ha ha. Kinyaa!
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Nundu ameluzungumza la Kia alipokuwa EA amefight wamejenga hanger ya service ya ndege kubwa na nyumba kadhaa za wafanyakazi, tangu alipoondoka waliobaki waka abandon ili service zikafanywe nje, watu wale miposho ya dola!.

Uwanja umekondishwa kwa mwekezaji anayelipa peanut serikalini!. He had to stop that nonsense!. Amedai angekuwepo yeye ATCL isingekufa, angeiingilia mpaka chooni!.

Kama cost ya mradi ni US $ less than 200 milions kwa nini wakope 600?. Approach yake ni kutumia PPP!.

Kweli hii nchi imefika sipo. Hapana this is too much.
 
Kwenye press conference nilikuwepo, kiukweli, upepo haumwendei vizuri waziri Nundu ila luwalo na liwe, kausema ukweli wa moyoni mwake na kuna uthibitisho beyond reasonable doubt, Nundu sio fisadi ila amezubgukwa na mafisadi left right and centre, hivyo kuishia kuonekana an enemy of the people!.

...Inawezekana kabisa hapa kuwa "wezi" wamemuwahi Nundu na kujivika vazi la "uzalendo" na kumtupia yeye "uchafu" wote kabla hajawavurugiwa deal yao...

...Nundu nenda lakini kama ulitenda kwa uaminifu katu usikae kimya, zuia deal hilo kwa namna yoyote ata kama hautakuwa waziri, kama sio basi kesho Watanzania wataujua ukweli...


...Kweli siasa ni mchezo mchafu , na watu wachafu ndio wanaoweza kuucheza vizuri zaidi....
 
Siku hizi Press Conf waandishi wanakwenda kusikiliza, wachache sana wanafanya utafiti na kuuliza maswali magumu bila ya kuwa na maslahi nayo. Ukiona wanaouliza maswali magumu wana maslahi na jambo husika na si kwa kufanya utafiti. Kama waandishi wangekwenda kwa Nundu wakiwa na taarifa kamili, nadhani Waziri angeanza kumwaga matusi.Bahati mbaya hata mipaka na majukumu ya Waziri watu wanakua hawamuulizi. Tusubiri tuone na wenye mapenzi mema na nchi hii watamwaga humu nyaraka. Sekta ya uchukuzi ni nyeti sana na ikiangaliwa vyema inaweza kubeba uchumi wetu.

....Mzalendo yoyote hawezi kukubali wala kuuunga mkono makataba kama huu, hakika Nundu anastahili pongezi na wala sio kejeli kwa kuupiga stop mwelekeo wa mkataba wa muktadha huu...

...Ili tutoke hapa tulipo kama taifa, tunahitaji viongozi wengi zaidi wasioweza kuulembalemba uozo wa wazi kama huu eti kwa jina la "mwendelezo wa makubaliano yaliyokwisha fanyika", no way, ujinga kama huu haukubaliki kwa viwango vyovyote....

...Ni mtu aliyekula 10% tu au asiye mzalendo ndiye anayeweza kuutetea ujinga kama huu, atleast kwa hili hongera sana Nundu...

Wanabodi,
Niko hapa mjini Dodoma, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Omar Nundu, anafanya Press Conference saa hizi hapa Dodoma Hotel na amefunguka vilivyo ikiwemo hoja ya kujuizulu!.

1. Ujenzi wa Gati No 12 na 14.
TPA wanaipigia chapuo kampuni CCC ya Uchina kujenga kwa gharama za mkopo wa dola appx 600 toka Exim Bank ya China. Waziri Nundu amekiri kuingilia kati sio mpaka sebulen bali hadi chooni kwenye uchafu wenyewe!.

Hiyo kampuni ya CCC ilipatikanaje?.
Waliofanya feasibility study ni hao hao CCC wanaotaka kujenga ni hao hao CCC na mkopo walioomba toka benki ya Exim ya China ni hao hao CCC. Waziri amepinga kwa kutaka ushindani wa wazi!. Wenzetu Mombasa wamejenga gati kama hizo kwa less than 200 millions, kwa nini sisi tujenge kwa dola milioni 600 tena bila ushindani wa wazi, why?.
2.2. Baada ya kuona waziri anawakwamisha CCC wakaamua kuyapitishia madudu yao kwa Naibu waziri. wakampa paid trips kutembelea miradi mbalimbali ya CCC duniani pote, Naibu waziri yeye hana bei, akaingia kichwa kichwa kuwa kuwadi wao. Alianza kupigwa trips za nje ya nchi bila kibali cha waziri wake, kwa lugha nyingine ni uwezekano wa Ikulu kuhusika kwa Naibu Waziri huyo kusafiri nje ya nchi bila waziri kujua. Mazingira ya safari hizo za naibu waziri zina viashiria vyote vya rushwa ya "free bees" under pretex ya "facility visit" under transparency lazima Naibu Waziri aseme amelipwa shin ngapi amesafirishwa tiketi za ndege za daraja gani na alifikia hoteli za nyota ngapi?.

Wachini huwa hawasafiri 1st Class, hawalipani per diem nono wala hawakai hoteli ya nyota 5!, ila makampuni yamayo sololea tenda, huwalipa maofisa wa nchi per diem nene, kuwasafirisha kwa 1st class na kuwalaza hoteli za nyota 5!.
 
Alichosema Nundu ni aibu katika mfumo wa utendaji kazi serikalini. He has to go. Ila kama Mfutakamba naye akianza kushindana naye, hatutaona tofauti kati yao, bali anatakiwa kuwa na busara zaidi.
Mkuu Halisi, myonge mnyongeni, haki yake mpeni!. Kosa kubwa la Nundu ni kuleta uzalendo kwenye kichuguu cha nchwa!, au kutaka kuzuia wezi kwenye shamba la bibi ambalo limezungukwa na mijizi!. Nakubaliana na wewe he has to go!. Kama mafisadi nchwa wametamalaki kumzunguka, yeye anayetaka kuzuia mijizi isituibie tena sasa ndio adui!.

Namhurumia sana Nundu, kama ninavyomgurunia Nape kupiga vuvuzela la anti ufisadi kumbe mifisadi iliyokubuhu ndio hiyo hiyo inayokula meza kuu na mkuu and you never know hiyo CCCC ni wale wale chini ya pretex ya Mchina!.
 
Ufisadi hapa Tanzania ni mfumo, dawa yake ni kuung'oa huo mfumo na kuweka mfumo mpya ambao utakuja na sheria mpya na kanuni mpya ambazo zitaziba mianya yote ya rushwa.

Ufisadi hapa ulindwa na "utatu usio mtakakatifu" (unholy trinity):
Kwa juu ipo Ikulu ambayo imekuwa ikiteua mafisadi na wakigundulika ama inapata kigugumizi cha kuwatema au kuwasafisha kiaina.

Upande wa mwingine wapo Wabunge wa CCM ambao wamekuwa wakiingia kifua Ikulu ili isisulubiwe na Bunge. Kwa kuwa wabunge wa CCM ni wengi, wanatumia wingi wao kuilinda Ikulu ili isitekeleze maagizo/maazimio/mapendekezo ya Bunge. Hapa tuna mifano mingi. Lakini hawa nao ni wanufaika kwani Ikulu kwa kutumia UWT, Polisi na hata JWTZ huwa inatishia raia na wakati mwingi hukusanya taarifa za kuzipeleka kwenye chama ili zifanyiwe kazi. Pia Tume ya Taifa ya Uchakachuaji (NEC) hufanya kazi ya kuchakachua matokeo kwenye baadhi ya majimbo ambako hakuna ulinzi wa kutosha wa kura.

Chama cha Mapinduzi kwa upande mwingine hufanya kazi ya kutishia kuwashughulikia wabunge wa CCM ambao wanaonekana wana kiherehere na ndio maana kukiwa na issue huwa wanaitana chemba kwenda kuwekana sawa. Wakitoka huko huja na approach ambayo humpa Rais discretion ya kutekeleza ama kutotekeleza maazimio/maagizo/mapendekezo ya Bunge.

Kwa hiyo hizi pande tatu zote zinalindana ili kuhakikisha kwamba mfumo wa ufisadi unaendelea kuwepo. Mwaka 2008, Kamati Teule ya Mwakyembe ilionyesha sheria kibao ambazo zina mapungufu yanayosababisha ufisadi, na ilipendekezwa sheria hizo zipitiwe upya, leo ni mwaka wa 4, hakuna hata sheria moja iliyofanyiwa marekebisho. Kamati ya Sakata la Jairo iligudnua kasoro nyingi sana kwenye Financial Regulations za mashirika na za Idara Kuu ya Utumishi na wakaagiza zifanyiwe kazi, mpaka leo ni zaidi ya miezi 6, hakuna kilichofanyika.

Serikali haitaki kufanya hayo marekebisho, Bunge halitaki kufanya hayo marekebisho, halafu akitokea mbunge wa Upinzani akapelaka hoja ya kubana mianya hiyo, wabunge wa CCM wanakuwa wa kwanza kugoma kuunga mkono halafu baadaye wanajifanya wanachukizwa sana ufisadi, yaani ni usanii kwa kwenda mbele!
 
Pasco wewe ni mchumia 2mbo,othertim we don undestand u..aneitishaje press kama hana hoja wakati nchi ipo ktk tension..hoja angeachia ngazi..na Ester Bulaya je?
Dalai Lama, the press co was full pack nondo!. Kwa Ester ninepata uthibitisho narudi pale muda sii mrefu!.
 
....Mzalendo yoyote hawezi kukubali wala kuuunga mkono makataba kama huu, hakika Nundu anastahili pongezi na wala sio kejeli kwa kuupiga stop mwelekeo wa mkataba wa muktadha huu...

...Ili tutoke hapa tulipo kama taifa, tunahitaji viongozi wengi zaidi wasioweza kuulembalemba uozo wa wazi kama huu eti kwa jina la "mwendelezo wa makubaliano yaliyokwisha fanyika", no way, ujinga kama huu haukubaliki kwa viwango vyovyote....

...Ni mtu aliyekula 10% tu au asiye mzalendo ndiye anayeweza kuutetea ujinga kama huu, atleast kwa hili hongera sana Nundu...
Mkuu Butola, kiukweli namhurumia sana Nundu, hisia zangu game yote inachezwa kule juu kwenywe kunako!, yeye ataishia kufanywa bangusilo!. Ili asivuruge deal, mtashuhudia akitolewa kondoo wa kafara apishe njia wenye meno wajilie vyao!.
 
sasa Nundu anafanyaje kazi na naibu ambae hawaelewani.!!!
Mkuu, mbona serikali yote iko hivyo hata JK analijua na akalizungumzia ktk sakata la mgomo wa madaktari kuwa hakuna kuaminiana baina ya ngazi za uongozi wa juu. Kwa kifupi ni kwamba hakuna maelewano baina ya Waziri na Naibu W, katibu mkuu na naibu wake, ma- DG na Deputy wao na hali hiyo ni ktk Wizara na Taasisi zote za govt kwa sasa, ni hatari sana!
 
Mkuu Pasco,
Unajua watu wengi hawafahamu kilichoendelea Bandari. Hili deal lilisha chezwa siku nyingi sana yaani CCC walipofanya feasibility study walikua namba zao ambazo sizijui ila waliambiwa waweke Usd 600 maana mkopo utatoka. Sasa yawezekana kabisa ujenzi wake ni Usd 200mil au 300 jamaa wakaongezea zao kufika 600. Alipokuja Nondo na kuona kwamba hapakuwepo na tender kisha gharama yenyewe sawa kabisa na mkopo wakati CCC haikueleza kwa kila kpengele cha mradi kita cost kiasi gani akaishtukia deal..

Hii imewaumiza wengi waliokuwa wakitegemea deal hili na Nondo amekuwa kizuizi kikubwa sana kiasi kwamba lazima aondolewe kama yule Katibu mkuu wa Tanesco enzi za Richmond ambaye nadhani yuko Ardhi sasa hivi. Tuweni makini sana na hizi tuhuma na naomba Mungu JK awashtukie hao viongozi wa Bandari, na wizara hii ambao wameisha jiweka mkao wa kula.
 
Pasco mbona unawatetea sana wezi na wabadirifu wa mali ya umma wanakupa nini kaka?
Waandishi kama nyie ambao hamko objective ni tatizo kwa tanzania tuitakayo
Mkuu Mungi, hivi kwenye hii issue ya Nundu kumbe wengi hawajagundua nani mwizi na nani anazuia tusiibiwe!. Waadilifu ndio wanaotokewa kondoo wa kafara, na mijizi na mifisadi ndio inaonekana safi!.

Safari halisi ya truthfullness, objectivity na impartiality bado ni ndefu!.
 
Katika Wizara zenye matatizo hii ya Nundu ni mzigo mkubwa,hyu jamaa namfahamu ni mzuri ila ataharibiwa na mfumo wa Chama,amepokea idara zote zenye matatizo,Reli ovyo,Bandari ovyo,ATCL ndio usiseme af mbaya walomzunguka pia wanamzunguka ki-ukweli so ana wakati mgumu sn af ikizingatiwa ni mgeni ktk system.Hata Zitto anamfahamu huyu jamaa ndiyo mana alithubutu kumtetea juzi.
 
Mh Nundu amesema haoni sababu ya yeye kujiuzulu na haelewi jinsi kampuni ya CCC ilivyoibuka . Mkanganyiko mkali. Source TBC.
 
Agoma kijiuzulu adai hajaambiwa ajiuzulu ila atafakari na anedai tatizo ni naibu wake sio yeye. Adai naibu wake kapewa rushwa kibao na wachina na safari za kutosha ili wapewe tender ya kujenga bandari.

Adai CCC ni kampuni na wanaoijua ni Naibu wake na TPA na ndio wanaotaka serikali ikope then iipe kampuni hiyo ya CCC ndo ijenge gati namba 13 & 14 zaidi wao ndo wanapanga bei na serikali iridhie bila discussion
 
Back
Top Bottom