Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 816
Asalaam alykum,
Ndugu zangu, kwa huzuni nawapa taarifa kuwa ndugu yetu,kaka yetu na mwenzetu Omari Lambi alifariki jana hapa London katika hospitali ya university College Hospital -Euston kutona na cancer ya kichwa "Nasopharyngeal Carlinoma" .

mipango ya mazishi inafanywa, punde mipango itakapokamilika tutawatangazia.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na:
Almas Kassongo 079830 73526.
Adam Mgoyi 07817290269.
Mhando 00447863138725.
mazishi ya ndg yetu Bw. Omari Lambi yatafanyika leo kwenye makaburi yaliyopo; Gardens of Peace,Elmbridge Road, Hainault, Ilford, Essex, IG6 3SW.
Kituo cha Treni cha Karibu ni Hainault Station, Central Line.
Wanaume wanaombwa kwenda makaburini moja kwa moja ambako pia ndipo atakaposwaliwa marehemu.
Wanawake watakuwa na kisomo kitakachofanyika kuanzia saa 5 Asubuhi; 266-268 High Street North, Manor Park, London, E12 6SB.
Taarifa hii Imetolewa na kamati ya Msiba
Akiwa hapa Uingereza, Marehemu alikuwa na Master ya Strategic Management na mwezi wa tisa mwaka huu alikuwa yupo mbioni kuchukua PHD.
Wakati wa uhai wake alikuwa ni kiongozi wa mfano na aliyejitolea muda wake kwa ajilio ya kufanikisha masuala mbalinmbali yenye faida kwa Watanzania wenzake na Taifa kwa ujumla.
Wana JF tumemempoteza mwanachama mTanzania mzalendo ambae alikuwa na mchango mkubwa kwenye kwenye mijadala mbali mbali humu ndani.
Ili kufanikisha mazishi ya marehemu, tunaomba michango yenu ya hali na mali, kwa kuweka michango katika akaunti:
Account No: 13258960
Sort Code: 30-84-12
Jina/Name: Mr. Said S. Surur
Bank: Lloyds TSB
Wabillahi Taufiq
Innaa Lilahi wa Inna Illahi Raajuun