Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Ufuatao ni mpango wa ushindi baada ya kuona Watanzania hatuna lengo la kufanya vizuri na tumekuwa wasindikizaji kila olympiki na tumebakia kukumbukia ushindi wa 1980.
NADHARIA INAAYOONGOZA: Kwa Taifa lolote kuweza kuchukua nafasi yake katika ulimwengu wa siasa na kiuchumi, Taifa hilo halina budi pia kuonesha kuwa lina nguvu na uwezo katika michezo. Ni michezo ambayo ndiyo siasa ya kweli inaonekana na ni siasa ya urafiki zaidi kuliko uadui. Ni kwa sababu hiyo utaonaa nchi kama Marekani, Urusi, Uingereza, China, Ujerumani, Australia na Ufaransa wanafanya jitihada kubwa sana kujiandaa kwa michezo hususan Olympic kwa sababu wanaamini it is the biggest political venue ya kuonesha mafanikio yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Tanzania nayo ikitaka kuonesha kweli imeanza kufanikiwa kiuchumi na kijamii haina budi kuonesha hilo kupitia kwenye michezo.
LENGO: Kupata medali zisizopungua 20 kwenye Olympiki ya London 2012. Za rangi yoyote ile.
IDADI YA WANARIADHA: Kuanzia sasa tutaandaa wanariadha wapatao wasiopungua 100 katika sekta zote kubwa za michezo, Soka, riadha, Uogeleaji, riadha na michezo mingine. Kati ya hao timu yetu itaundwa na wanariadha 50. Itaitwa Timu ya Ushindi (Victory Team)
MIKAKATI:
Yote haya yatawezekana endapo tu kuna NIA na UAMUZI wa makusudi wa KISIASA YA KUFANYA VIZURI KATIKA MICHEZO. Hadi pale wanasiasa wetu watakapoona haja ya kuinua Tanzania katika michezo ndipo tutaweza kufanya vizuri. Lakini kwa kadiri wanavyosubiri watu wafanye vizuri ndio watoe pongezi ndivyo watakavyoendelea kusubiri kuvuna wasichopanda! Vinginevyo wataendelea kusubiri kulia kivulini bila kuchumia juani.

- 0. Kuunda Kamati ya Ushindi ambayo itasimamia maandalizi haya ya Olympiki. Kamati hiyo itaundwa na watu wote ambao hawajawahi kusimamia maandalizi ya Olympiki kabla! Iundwe na wataalamu wa chakula, wataalamu wa afya, wanamichezo, conditional pyschologists, na iwekwe chini ya mtaalamu wa riadha kutoka China. Huyo Mchina na timu ya wasaidizi wapewe uwezo wote wa kusaka, kutambua, na kukusanya vipaji vya vijana wa Kitanzania na itakapofika 2010 awe tayari na timu ya vijana wasiopungua 100 kuwaandaa kwa Olympiki.
- 1. Kuanza kusaka vipaji vya wanamichezo kuanzia wenye umri wa miaka 12 sasahivi hadi wenye miaka 16 sasa hivi ili ifikapo 2010 wale wenye miaka 12 watakuwa na miaka 16 ambao ni umri wa chini wa kushiriki Olympiki na wale wenye miaka 16 sasa hivi watakuwa na miaka 20. Lengo letu ni kupeleka timu ya vijana zaidi katika Olympiki. Kwenye timu yetu ya Ushindi mwenye miaka 21 ndiyo atakuwa "mzee" kwenye timu hiyo.
- Katika hili jitihada ya pekee ifanywe pia ya kuwahusisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi hasa nchi zenye vifaa na zana za kisasa za ushindani kama Marekani, Uingereza, Ujerumani n.k na kuwaambia kuwa kama wana watoto wao walio kati ya umri huo hapo juu watoto hao wanaweza kushiriki timu ya Taifa ya Tanzania endapo wataandikishwa na watakuwa tayari kushiriki mashindano ya Tanzania. Msisitizo upewe kwa Watanzania pia watakaokuwa katika vyuo vikuu mbalimbali vya Marekani kuwa wajihusishe na michezo katika vyuo hivyo na watapata nafasi ya kushirki mashindano ya TAnzania ya Taifa kupata timu kwa kadiri ya kipengele cha 2 hapo juu.
- 2. Miaka hii miwili ya mwanzo kuwa na mashindano ya michezo kila mwezi katika wilaya na mikoa mbalimbali ya kutafuta vipaji. Kuanzia kwenye mashule ya msingi, mitaani n.k Mashindano ya wilaya ya riadha, mashindano ya kijiji ya riadha ili kuibua vipaji mbalimbali. Haya mambo ya kupoteza muda na "umiss wherever" na kucheza "chandimu" peke yake yaanze kuzaa matunda kwani hakuna Olympiki ya urembo! Vijana wetu waanze kutiwa moyo kuwa na wao wanaweza kuwa wanariadha maarufu zaidi duniani kupitia mashindano ya Olympiki.
- 3. Ndani ya mwaka mmoja wa maandalizi (2008/2009) tushiriki mashindano ya dunia ya riadha na tuhakikishe vijana wetu wanafanya vizuri huko. Wakianza kupata ile fedha ya ushindi (kwenye mashindano ya dunia mita mia moja mshindi anapata karibu dola milioni moja!). Itaanza kuchochea wengine kuelekea 2009/2010.
- 4. Ili kuweza kufanikisha hilo la (3) hapo juu Serikali (ya Muungano na ya Zanzibar) zitenge kiuiwiano Shs. Bilioni moja kila mwaka kwa ajili ya kujiandaa kwa Olympiki kila mwaka. Kwa hiyo hizo bilioni moja za mwaka huu zitumike kuandaa ofisi, makazi ya makocha, na vitendea kazi vya mwanzo vya "Kamati ya Ushindi na kuandaa mchakato wa awali wa kusaka vipaji na kuanza kuviendeleza mikoani.
- 5. Mojawapo ya michezo ambayo tunattaka kuushangaza ulimwengu ni kuogelea. Huu ni mchezo ambao naamini tuna nafasi kubwa zaidi kuliko nchi nyingi za kiafrika. Tukiwa tumezungukwa na maziwa makubwa matatu na bahari ya Hindi kuogelea kuko ndani ya damu yetu. Hivyo, tujenge vituo viwili ifikapo 2010 Tanzania National Aquatic Centers. Lengo la vitu hivyo ni kuwapa watoto na vijana na mtu mwingine yoyote nafasi ya kuogelea kitaalamu. Lakini msisitizo mkubwa ni vituo hivyo kutumika kama sehemu za mashindano ya kuogelea. Vituo viwe ni vya kiwango cha Olympiki. Nani tumuombe ajenge kwa fedha zetu wenyewe, you guessed it China. Ifikapo 2010 tuandae mashindano ya kwanza ya Kimataifa ya Afrika ya Kuogelea tunaweza kuyaita TanzaniaaOpen Swimming Competition; na kwa mbwembwe zetu tunatangaza mshindi wa kwanza kupata medali ya Tanzanite!! or something of sort!
- 6. Ifikapo 2010, kambi ya Olympiki itengenezwe na mchuo ufanyike hadi kufikia kiwango cha kuwa na wachezaji 50 tu ambao wote wawe wawe wamefikia kiwango cha olympiki. Vijana hao 50 na labda 20 ambao ni substitutes ndio wataunda timu ya Olympiki ya Taifa kuelekea London 2010. Watakuwa kwenye kambi ya eneo moja, kama walikuwa kwenye shule nyingine watahamia karibu na kambi hiyo kwa gharama za serikali. Nidhamu itakuwa ni msingi wa ushindi, na uzalendo kwa Taifa iwe ni chachu ya wao kujituma.
- 7. Ifikapo 2011, timu yetu lazima iwe inashikilia rekodi kadhaa za dunia katika maeneo mbalimbali na hivyo tunapojiandaa kwenda Olympiki 2012 jina la Tanzania linatangulia kuwa ni "washindi wa dunia". Mashindano ya Taifa ya 2011 yatakuwa ni pamoja na kuwaleta wale vijana wa Kitanzania walioko nje kwa mujibu wa kipengele (cha pili) ambao watashinda kupata tiketi ya kushiriki Olympiki na kambi ya Taifa ya Olympiki of a Unified Team itawekwa rasmi. Kabla ya mashindano ya 2012, timu hiyo ya Olympiki ipewe ofa ya nguvu kutembelea sehemu mbalimbali duniani kwa mapumziko ya angalau wiki mbili kuwashukuru kwa muda wote wa kujiandaa na olympiki na wanaporudi wanakuwa kwenye "Lock Down" hadi Olympiki iishe.
- 8. Timu ya Tanzania ikiwa na wanaridha 50 na rekodi kadhaa za dunia itapita mbele ya jukwaa la wageni siku ya ufunguzi kama tishio la ushindi. Mashindano ya kwanza ya kuogelea, Michael Phelps anaangushwa na kijana wa Kitanzania na kumnyang'anya dhahabu yake ya kwanza kwenye Relay! Tanzania itakuwa imefika.
- 9. Mwisho wa Olympiki London Tanzania ni nchi ya Afrika iliyofanya vizuri zaidi kwenye Olympiki na kwenye dunia ikiwa ni miongoni mwa nchi 10 bora. Wakati huo mtajua hatukushinda kwa bahati!!!