Ole wetu sisi! Hata sisi saa zetu zaja

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,766
18,620
Taifa limepata msiba mkubwa Sana, limepoteza mkuu wa nchi, amirijeshi mkuu, mkuu wa serikali na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi!

Kama ilivyo kawaida wa wanadamu, tupo tunaohuzunishwa na ukomo wa maisha yake hapa duniani, wapo pia waliongojea kifo chake Kama siku ya furaha, wengine wanajitokeza hadharani na kudai bado wanakesha baani wakilewa na kufurahisha nafsi zao.

Tunamhukumu Sana John Pombe tukimnyooshea vidole kuwa alikuwa muovu na mtenda mabaya dhidi ya wengine.
Tunasahau kuwa hata sisi hatuishi vizuri na majirani, ndugu na hata familia zetu.

John Magufuli amelala milele, na wengine tunaamini maisha yetu yatakuwa marefu na tutafurahi Sana hapa duniani. Ila hatujui lolote ambalo Mwenyezi Mungu aliamua katika sekunde ya mwisho ya kupokea roho ya Magufuli.

Inawezekana Mungu anatutizama kwa huruma sana tunaoendelea kufurahishwa na kifo Cha huyu mtu tunayeamini alitunyima maisha Bora na raha.

Ndugu zangu! Sisi Ni wadhambi sana, hatuna tofauti na wale tunaosherehekea mauti yao, hatujui Ni lini tutaitwa hukumuni, hatujui tutakuwa baani tukila na kunywa! Mwisho wetu utakuwaje?

Kama Mungu Muumbaji alivyonena ya kuwa tumetokana na mavumbi, hakika mavumbini tutarejea!

Mungu atupe hekima na busara, tuache kuhukumu ambao tayari Bwana ameshahukumu tayari!

Pumzika unapostahili Ndugu John Pombe Magufuli, mema yako yatalinufaisha taifa, nasi tu karibu kuingia hukumuni mwa Bwana.
 
57:20



Know that the life of this world is but amusement and diversion and adornment and boasting to one another and competition in increase of wealth and children - like the example of a rain whose [resulting] plant growth pleases the tillers; then it dries and you see it turned yellow; then it becomes [scattered] debris. And in the Hereafter is severe punishment and forgiveness from Allah and approval. And what is the worldly life except the enjoyment of delusion.

QUR AN 57:20

Tunatakiwa tuyajue haya kabla ya siku kufika. Naiusia nafsi yangu na nafsi yako wewe mleta uzi juu ya maisha haya. Itoshe kusema Mungu atuongoze.

Samahani kama ntakuwa nimekukwaza mkuu!
 
Back
Top Bottom