Ole wenu watanzania, wanachokisema wanamaanisha

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
1,853
2,000
Amani iwe kwenu wazalendo wa nchi hii. Natumaini mungu yupo pamoja nasi katika maisha yetu ya kila siku. Mungu anatupenda sote bila kujali tofauti zozote tulizonazo kwa kuwa sisi sote ni watoto wake na tumeumbwa na yeye.

Ningependa kuwa niwapongeze Watanzania wote kwa kuendelea kulijenga taifa letu kila mtu kwa nafasi yake yaani kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kadhalika. Kwa mfano wachumi wetu wamekuwa wakituelimisha na kutupa mawazo namna gani ya kujenga uchumi wetu pia wanasheria nao wamekua wakitupa tafsiri za kisheria zinazotusaidia katika maisha yetu, wote mbarikiwe sana. Nami leo nimekuja kutoa mchango wangu mdogo kuhusu lugha mbalimbali zinazotolewa na viongozi wetu.

Tumekua tukishuhudia lugha mbalimbali zisizo na staha zikitolewa na viongozi wetu. Hebu jaribu kutafakari lugha kama wapinzani ni wapumbavu na malofa, watakaoshindwa kumudu nauli wapige mbizi, ninaposimama mimi ni Mungu amesimama, Tuko radhi watanzania wale nyasi kwa vyovyote ndege ya Rais lazima inunuliwe, wapigwe tu nk.

Baada ya kusikia lugha mbalimbali zenye uhaba wa staha nikajikuta narejea nadharia iitwayo SPEECH ACT THEORY. Speech Act ni sayansi ya lugha na falsafa ya lugha ambayo imeelezea dhana kwamba kauli kazi yake ni kutenda. Kwa wataalamu wa lugha yaani watu wa tasnia ya "Linguistics" wanajua ukweli kwamba katika mambo haya ya "Speech Act" siku zote ni kwamba kauli ukiitoa inapelekea tendo litendeke. Kwa hiyo siyo kwamba maneno au kauli zinapotolewa na mtu zinabeba taarifa pekee bali zinabeba matendo ndani yake. Kusema ni kutenda kwa kua maneno huumba kwa hiyo chunga kauli yako. Once you speek, you can't take it back. Neno ukishalitamka halirudi tena mdomoni, hivyo basi mdomo unaweza kukiponza kichwa kama sio mwli kabisa.

Kama ilivyopata kuandikwa na mwanafalsafa wa Oxford J. L Austin ( How To Do Things With Words) na baadaye kuendelezwa na mwanafalsa wa kimarekani J. R. Searle ni kwamba kauli inaweza kuwekwa katika hatua tatu za utendaji au vitendo kama ifuatavyo

(1) Kauli yenyewe inayotolewa na yenye maana mfano nikiingia madarakani watu watalimia meno.
(2) Lengo la kauli hiyo...... hapa inabidi ujiulize swali kwamba huyu aliyeitoa kauli husika alikua na maana gani mfano kutisha watu, kufurahisha, kuelimisha, kuburudisha nk
(3) Matokeo ya kauli yake- kwa mtoaji, mlengwa mfano watu kuogopa, kuteseka, kutajirika nk

Nimejaribu kufanya upembuzi wa kauli zifuatazo kwa muongozo wa wanafalsafa niliowazungumzia kama ifuatavyo

Nataka watu waishi kama mashetani, yaani hii inatia ukakasi kabisa. Katika hali ya kawaida ni kwamba katika jamii zetu yaani nyumbani, shuleni, mitaani na pia katika nyumba za ibada tumefundishwa kwamba shetani ni kiumbe mbaya sana kwa hiyo unabidi tumwogope sana na pia tusimwabudu. Tumefunzwa kwamba shetani ndiye aliyeileta dhambi duniani pia ndiye aliyesababisha kuwepo na kifo duniani, magonjwa, mafuriko, matetemeko, ugaidi, njaa, vita, ukame. Kiongozi huyo alipotamka maneno hayo ni kweli alimaanisha na lengo lake la kuigeuza Tanzania kuwa Jehanamu imewezekana. Nchi ya viwanda haipo ndo hao akina Ndangote wanaondoka, hapa kazi tu haijawezekana hakuna kazi wala ajira zozote mpaka sasa. Elimu hakuna ndo hivyo wanavyuo vikuu wanalia coz mikopo ni majanga.

Watu watalimia meno, hii kauli ni ile inayopatikana katika kitabu cha Luka 13:28 inayosema "Hapo ndipo mtalia na KUSAGA MENO YENU, wakati mtakapomwona Abrahamu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa mungu, lakini ninyi wenyewe mkiwa mmetupwa nje". Jamani watanzania tuwe wakweli, hivi huyu mtu alimaanisha nini hasa? Kweli alimaanisha tutaumia kweli kweli kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa hili alimaanisha na ndio maana sasa tinasagia meno na kulimia pia na kauli yake imetimia, maneno huumba na aliongea kwa vitendo. Kwa mfano wanyonge tumetupwa nje ya mikopo ya elimu ya juu, hakuna kazi kwa vijana wahitimu wa taaluma mbalimbali, kwa wafanyakazi serikalini hakuna ongezeko la mishahara, kupanda madaraja, uhamisho vilevile kwa wanafunzi hakuna elimu bora ya ukipanga bali ya ukilaza ndio imetawala.

Msinidrive, hii kauli ya msinidrive asili yake ni ubabe na udikteta ndani yake. Kauli hii inamaanisha huyo anayeitoa hataki umjaribu kwa sababu anaweza akakufanya kitu mbaya ukajajutia maisha yako yote. Ukileta ujinga anaweza hata kukupasua au akufanye kitu kinachofanana na hicho. Kwa WABONGO wengi tumezoea mtu akisema "usinidrive" tunaelewa kwamba huyu mtu anamaanisha "usiniendeshe", "usinipelekeshe" "usinitumikishe". Je kweli huyu kiongozi hatukumchangua ili atutumikie? Basi MAJANGA. Je hawa wanavyuo kudai haki yao ya kupatiwa mikopo ni kumpelekesha au kumuendesha huyu kiongozi?. Baada ya tafakuri yangu ya hii kauli kwa muktadha wa Kitanzaniatanzania nikaamua kurejea kamusi yangu ya "Oxford Advanced Learner's Dictionary- New 8th Edition" imetoa maana ya neno "drive" kwa muktadha wa lilivyotumika kwa tafsiri zisizo rasmi
>To make somebody very angry, crazy. Kauli hii ikimaanisha kumfanya mtu awe na hasira na achanganyikiwe. Kwa hiyo watoto wanyonge wa Kimaskini Tanzania kudai haki yao ya kupatiwa mikopo inamfanya mheshimiwa awe na hasira na achanganyikiwe. Hili limetimia mpaka sasa na ndio maana hakuna anayemjaribu na wote tunamwogopa ili tusije ziamsha hasira zake na kuchanganyikiwa pia tusijejuta. Kwa mfano mpaka sasa uhakiki imekua danadana hata aliowapa mamlaka hawana majibu mpaka aseme yeye coz yeye ni one man show na pia one man army. Hata ndugu yangu Lissu pamoja na kuzijua sheria naye amenyuti kimya. Brother Lema alimjaribu kidogo tu mpaka sasa ni historia. Wafanyakazi wananyimwa haki na stahiki zao ila viongozi wa vyama vya wafanyakazi wako kimya wanaogopa kupasuliwa kama jipu. Sio kituo cha haki za binadamu, sijui jukwaa la katiba, wala wanaharati na pia yoyote aliyeweza kujibu shambulizi la NAINYOSHA NCHI KWANZA, SITAKI MAMBO YA VIKATIBAKATIBA MIMI KWENYE UTAWALA WANGU
>To make them do something extreme eg drive somebody crazy/mad/insane ikimaanisha kumfanya mtu afanye kitu kwa kupitiliza mfano awe juha au punguani wa kupitiliza. Sidhani kama wanafunzi wa elimu ya juu walifikia huko. Kwa hili huyu mheshimiwa ameamua kuwa mbogo kwa sababu hataki kushughulikia kero za watu wake hivyo sasa anakereka kuona wanadai haki ili hali yeye anataka waishi kama mashetani kwa wakati huohuo walimie meno. Kweli yeye ni msema kweli na maneno yake yameumba kwa kuwalk the talk na talk the walk. Shikamoo J. L. Austin wewe ni noma sana uliposema HOW TO DO THINGS WITH WORDS.

Namaliza kwa kusema ole wenu watanzania, hawa jamaa wanaposema huwa wanamaanisha kweli kweli kwa kuwa wao wakisema ni mungu amesema na pia ni Mungu kasimama wao walipo. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

.
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,842
2,000
Hawa hawashauriki mwisho utaishia kuambiwa kuwa hawa ndio vichaa tunaopambana nao.
 
kyte

Senior Member
Sep 8, 2013
164
225
Aisee hata ww una moyo wa mwendawazimu,,huoni hata hapo ulikuwa unatoa somo na ushauri usiotakiwa. Kifupi hata siku moja huwezi kuzuia au kuzifunga akili na ufahamu wa watu,utawatisha nao watanyamaza sababu hawataki madhara ktk miili yao,lkn kwa kuwanyamazisha hivyo je,akili na ufahamu wao. Kiongozi anaetawala kwa mkono wa chuma tumeshuhudia na kusoma siku zote hawajawahi kutoa majibu muafaka kwa mustakabali wa anaowaongoza,. Kama anaweza kuongea yy utawala wake sio wa kile kitabu cha makubaliano na wananchi ambacho aliapa kukilinda,.!! Kazi bado sana
 
Mkuu kwa hyo ktk hlo mm nina moyo wa mwendawazimu!!!!!
 
treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,634
2,000
Mleta hoja, ni kweli kama ulivyoanza hapo juu, Mungu anatupenda sana watanzania. Lakini pia mweleze Mungu vizuri katika hizi situations. Mungu anatupenda sana watanzania, lakini bila shaka anatushangaa sana pia kwa sababu ya mambo yetu ya ovyo ovyo na unafiki unafiki. Hivyo ameamua kuendelea kutuacha kuogelee kwenye umaskini wa kutupwa pamoja na kuwa na raslimali nyingi ili akili itukae vizuri. Kwenye hilo, tusidanganyike, Mungu anasikia sala zetu lakini hawezi kutusaidia kwa lolote. Haiwezekani tuwe masikini miaka nenda rudi na kisha tuendelee kuchagua chama hichocho kila baada ya miaka mitano (na tumekuwa tukifanya hivyo kwa zaidi ya miaka 50 sasa) kisha tumlalamikie Mungu. Hapo Mungu ataendelea kutuvunisha tunachopanda, na hiyo ndiyo haki yake.
 
JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,939
2,000
Kati ya viongozi watakao jilaumu sana wakimaliza muda wao na kustaafu ni JPM na makonda. katika uongozi kuthubutu ni jambo jema ila kuwa too ambitious ni hatari.Ni hatari kwasababu hutaki kukutana na kikwazo wakati unataka kufikia malengo yako, na unaweza kudhuru kuangamiza kabisa mtu yeyote unae dhani kwako ni kikwazo. kutofautiana kinadharia na kiitikadi katika zama za vyama vingi ni jambo la kawaida na uvumilivu wa kihoja unahitajika.walio jiona miungu watu wote wamepotea wameiacha dunia ikiendelea.
 
Kweli kabisa ktk hilo Mungu lazima anatushangaa sana kwa kuwachagua watu walewale na wenye akili zilezile pia na malengo yaleyale. PIA VIONGOZ I HOPE MUNGU ANAWAONA KWA KUTUMIA MAMLAKA WALIZONAZO KUBAK MADARAKAN
 
DUBULIHASA

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
1,853
2,000
Kati ya viongozi watakao jilaumu sana wakimaliza muda wao na kustaafu ni JPM na makonda. katika uongozi kuthubutu ni jambo jema ila kuwa too ambitious ni hatari.Ni hatari kwasababu hutaki kukutana na kikwazo wakati unataka kufikia malengo yako, na unaweza kudhuru kuangamiza kabisa mtu yeyote unae dhani kwako ni kikwazo. kutofautiana kinadharia na kiitikadi katika zama za vyama vingi ni jambo la kawaida na uvumilivu wa kihoja unahitajika.walio jiona miungu watu wote wamepotea wameiacha dunia ikiendelea.
Wanajifanya wazalendo kumbe wanafki sana.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,174
2,000
Mwisho wa siku inafahamika kwamba hicho ni kiburi cha madaraka tu , hakuna mwanadamu mwenye uwezo kushinda Mungu .
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,174
2,000
Kati ya viongozi watakao jilaumu sana wakimaliza muda wao na kustaafu ni JPM na makonda. katika uongozi kuthubutu ni jambo jema ila kuwa too ambitious ni hatari.Ni hatari kwasababu hutaki kukutana na kikwazo wakati unataka kufikia malengo yako, na unaweza kudhuru kuangamiza kabisa mtu yeyote unae dhani kwako ni kikwazo. kutofautiana kinadharia na kiitikadi katika zama za vyama vingi ni jambo la kawaida na uvumilivu wa kihoja unahitajika.walio jiona miungu watu wote wamepotea wameiacha dunia ikiendelea.
Na historia inaonyesha kwamba kila utendayo yatakurudia .
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,425
2,000
Kwangu nakubaliana n.a. wewe aslimia zote lkn ili sio la kuwaraum wanao toa hizo kauli au matendo bali kujiraum sisi kama watanzania ambao tunakubari n.a. kuruhusu haya mambo wanayofanya kabisa.
Ebu angalia mifano mingine ya wabunge ambao ndio mamlaka ya kumuwajibisha rais moja kwa moja kisheria lkn wamekaa kimya huku katiba ikiendelea kuvunjwa na hakuna mwenye kukemea angalau..Bila shaka wote ni washirika wa haya maovu wawe wapinzani au ccm
Siku ambayo rais alivunja katiba in public n.a. pia kwenda kinyume n.a. maadili ya uongozi wa umma ni siku aliposema serikali yake haiwezi kushirikiana n.a. upinzani ..hii kauli nchi nyingine watu wataingia mtaani n.a. lazma utaondoka
 
Hiyo ni kwel na wapinzan nao sasa wanamwogopa coz huyu mtu amegeuka ye ndo mungu full kuleta ubabe, I think kuna umuhimu wa kubadil methodology ya kuweka mambo sawa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom