Kwani walichaguliwa na wananchi?? Sio lazima wawakilishe etiWabunge, wawakilisheni Wananchi wenu vizuri.
Asilimia kubwa ya Wabunge kule Bungeni hawatetei maslahi ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Zaidi sana wanachokifanya ni kujipendekeza na kujikomba kwa Mkubwa.
Wameacha kabisa wajibu wa msingi wa Mbunge ambao ni kuisimamia na kuishauri serikali. Wananchi wanateseka huku mtaani, wao hawana habari.
Mbaya zaidi, akitokea Mbunge mmoja akatoa hoja inayokinzana kidogo na utawala, unakuta wanamshambulia kisawa sawa huyo Mbunge kwa kuomba miongozo isiyo hata na tija kwa Taifa.
Kama Wabunge wote wangetimiza wajibu wao wa msingi, kwa hakika hata bei za vitu zisingekuwa zimepanda kwa kiasi hiki.
Ni vema kila Mbunge akakumbuka kuwa, Wananchi ndio waliompeleka pale Bungeni, na wala si huo utawala wanaoutetemeke.
Pia wakumbuke kuwa, mwaka 2025 siyo mbali sana kama wanavyofikiri, watakuja kutuambia nini 2025?
Hali kadhalika wakumbuke kuwa, Watanzania wa sasa si kama wa miaka iliyopita.
Wanajitambua sana kuliko wakati mwingine wowote ule.