Ole Sosopi ahojiwa polisi

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa(BAVICHA), Patric Ole Sosopi leo amehojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma ya kutoa lugha chafu inayotishia uvunjifu wa amani.

Sosopi alifika kituoni hapo saa 4.10 asubuhi huku ameambatana na wakili wake Frederick Kikwelo huku wakisindikizwa na wafuasi watano wa chama hicho.

Akizungumzia suala hilo baada ya kutoka polisi mwanasheria wake alisema mwenyemkiti huyo alihojiwa kwa nusu saa na alipewa dhamana na jeshi la polisi huku wakiendelea na upelelezi wao ambapo ukikamilika watakabidhi kwa mwendesha mashtaka kwa ajili ya kupitia ushahidi.

Sosopi alisema baada ya kuhojiwa alielezwa na jeshi la polisi kuwa arudi Julai 18 mwaka huu lakini hawajampa sababu ya msingi ya kurudi siku hiyo.

“Polisi hawajanipa sababu ya msingi ya kurudi Julai 18 mwaka huu,”alisema Sosopi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu alichohojiwa Sosopi, alisema hana taarifa hizo hivyo atafuatiulia
Wanadhani ndio watapunguza spidi ya bavicha kwenda dodoma?
 
siku hizi unashinda mitandaoni ili na wewe uchaguliwe kama wenzako lakini wewe elimu yako ni form 4 pale mazengo laki unaweza pata bahati maana magu uchagua watu wasio na vision kama wewe jitahidi

swissme
Hivi alimaliza kweli hata hiyo form 4?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom