Ole Sendeka,mbunge wa Simanjiro na Eng Chambiri,mbunge wa Babati 215 siombali sana na mtajuta

Mtoto wa tembo

Senior Member
Oct 4, 2012
198
30
nianze na huyu mbunge wa Babati mjini hajawahi sisikika wala kuonekana bungeni kwa muda mrefu sana.
jimboni kwake pia mpaka wamemsahau na wanajuta kumpa nafasi ya uwakilishi.
watu wanadhulumiwa Babati mjini kwenye suala la ardhi ,huduma za hospitali mbaya sana ,jeshi la polisi kunyanyasa raia,miundo mbinu mibovu sijui upo kwa viigezo vipi hapo njengoni.
kweli utakuja kwa sera zipi next time kuwaomba kura watu wako??

nimetoka mererani kikazi huwezi amini maji ya kuoga ilibidi mmiliki wa hiyo hoteli apigiwe simu kutoka mjini ndipo atoe agizo kua maji yakanunuliwe KIA ambapo ni umbali wa kilomita kama ishirini na tano.
mji wa mererani ni maarufu kwa madini aina ya Tanzanite ambayo hayapatikani sehemu yoyote hapa duniani zaidi ya hapo mererani.
tatizo la maji ni kubwa sana,kwa ujumla hata mabomba hayapo ardhini,inamaana toka MUNGU aumbe dunia wananchi wa kule hawajawahi ona maji ya bomba.
Ole Sendeka una laana ya watu wa mererani na sijui utakuja kwa staili gani kuomba kura.

wana wa MTWARA msikubali gesi kutoka huko mpaka mpewe uhakika wa nyie kufaidi kwanza.
mfano mwingine mzuri ni machimbo ya dhahabu na almasi kule shinyanga na mkoa wa Mara kwa ujumla,wameachiwa mahandaki hata mchanga wawekezaji wameondoka nao.
MTWARA komaeni mpaka mwisho.
 
afadhali ya Sendeka,huyo wa Babati ndio ziro kabisa.hajawahi onekana bungeni na jimboni kwake.
kweli ccm ni majanga kwa Tanganyika.
 
ha ha mlikurupuka mngeuliza tarime aliko tokea baada ya kupigwa chini na chacha wangwe eti nyie mkaenda kumpa ubunge kisyeri ni mbumbu sana uwezo wake ni mdogo sana
 
Cha2 alikimbizwa kwao Tarime nyie mkamchagua, tulieni mpaka 2015 mtakuwa mpepata akili.
 
ila mbuge wa babati nilimsikia akiongea bungeni week jana ni mhindi fulani hivi, akitoa dongo tu kwa ccm utasikia huyo si mtanzania.
 
namwona mbunge wenu anafuatilia hapo chini "kishili" .

wana babati imekula kwenu,kwa nini mlikulupuka kumchagua chambili?alikuwa mbunge wa tarime kwa miaka 15(1990-2005)hadi anashindwa na chacha wangwe alichangia bungeni mara moja tu,tena kuhusu kupanda kwa bei ya nyama dar es salaam,.
 
mbunge aina ya chambiri tunamshangaa kwa nini anahitaji kuwakilisha watu? maana hata ukimuuliza maana ya uwakilishi hajui!!!!!! sasa jamani si kama mtu anatafuta biashara yake si afanye siasa kwa nini iwe ndio biashara?
halafu huyu sendeka naye alikuwaga na akili lakini tangu aanze kula rushwa za lowassa hana mwelekeo
 
Baadhi ya Wadanganyika sasa waanza kuumizwa na mfumo ulijikita nchini Danganyika.. Wakati wa chaguzi tunabaguana kwa kanga za mkopo wa maisha ya miaka mitano(5) na kofia na vilemba.. Sasa hivi twalia wote.. Fanya kosa tena 2015...!!!!!!!
 
mbunge aina ya chambiri tunamshangaa kwa nini anahitaji kuwakilisha watu? maana hata ukimuuliza maana ya uwakilishi hajui!!!!!! sasa jamani si kama mtu anatafuta biashara yake si afanye siasa kwa nini iwe ndio biashara?
halafu huyu sendeka naye alikuwaga na akili lakini tangu aanze kula rushwa za lowassa hana mwelekeo
Watajiju. 2015 is just around the corner.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
wana babati imekula kwenu,kwa nini mlikulupuka kumchagua chambili?alikuwa mbunge wa tarime kwa miaka 15(1990-2005)hadi anashindwa na chacha wangwe alichangia bungeni mara moja tu,tena kuhusu kupanda kwa bei ya nyama dar es salaam,.

Kama sikosei,huyu Chambiri wa Babati mjini,ni kaka wa yule aliyekuwa mbunge wa Tarime,..Huyu kaka mtu, alikuwa Mwenyekiti wa CCM,mkoa,kabla ya Bwana Makongoro Nyerere..Baada ya jina lake kutokurudi kwenye nafasi ya Uwenyekiti mkoa,mwaka 2010 ndipo akaamua kwenda kugombea Babati mjini,akamshinda Mwl Omar Kwaang kwenye kura za maoni za CCM,na kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu..ila ni kweli huwa simsikii kabisa bungeni,hana tofauti kabisa na yule mbunge wa Mikumi..Hapo Babati Mjini,inahitajijika M4c kidoogo tu!
 
Hiyo Katiba mpya ije itatuondolea watu kama hawa kwenye nafasi za ubunge...wapo wapo tu utadhani wapo dukani
 
Kama sikosei,huyu Chambiri wa Babati mjini,ni kaka wa yule aliyekuwa mbunge wa Tarime,..Huyu kaka mtu, alikuwa Mwenyekiti wa CCM,mkoa,kabla ya Bwana Makongoro Nyerere..Baada ya jina lake kutokurudi kwenye nafasi ya Uwenyekiti mkoa,mwaka 2010 ndipo akaamua kwenda kugombea Babati mjini,akamshinda Mwl Omar Kwaang kwenye kura za maoni za CCM,na kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu..ila ni kweli huwa simsikii kabisa bungeni,hana tofauti kabisa na yule mbunge wa Mikumi..Hapo Babati Mjini,inahitajijika M4c kidoogo tu!

Chambiri huyo wa babati,ndo huyo huyo aliyekuwa mbunge wa Tarime.
 
Back
Top Bottom