Ole Sendeka: Marufuku vyama vya upinzani kufanya vikao mkoani kwangu

Mimi nafikiri viongozi wawe makini na matamko yao. Vyama vingi au wapinzani wapo kisheria katika nchi hii. Sasa kama hawatakiwi cha kwanza ni kuwafuta katika katiba ba sheria za vyama vya siasa lakini siyo kutoa matamko ya aina hii.

Wawe makini! You must be joking. Wewe unaamini mtu anayetoa kauli kama hii anao uwezo wa kuwa makini kweli?
 
Hii ni awamu ya kukanyaga sheria, maana haina makali kwa watawala hasa wateule wa rais. Wamemsoma rais anafurahia sana ukandamizaji wa vyama vya siasa ila Mwenyezi Mungu tu hayupo upande wao.
 
Tatizo ni mikutano ya hadhara yenye kukusanya wananchi hiyo aiwezi kubalika baada ya uchaguzi; lakini kama majuzi Salum Mwalimu kaenda kwenye mikutano yao ya ndani kwa wanachama wao hizo ni haki zao za msingi.

Hivyo ya hadhara imekatazwa na sheria gani?
 
"Nikikukuta nitakushukia kama mwewe" alisema Ole Sendeka.

Source: TBC1 Dira ya mchana.

My take.
Viongozi wetu ni bora wawe wazi kama hawataki uwepo wa vyama vingi.
Mengine maneno tu mbona Salum Mwalimu ametoka hapa na kafanya kikao akaenda kukamatiwa Iringa

Sema Chadema akili kama mapunguani kila neno kila nukta mnaichukulia jumla jumla
 
Mimi nafikiri viongozi wawe makini na matamko yao. Vyama vingi au wapinzani wapo kisheria katika nchi hii. Sasa kama hawatakiwi cha kwanza ni kuwafuta katika katiba ba sheria za vyama vya siasa lakini siyo kutoa matamko ya aina hii.
Kwa bahati mbaya hata vyombo vyetu vya habari havihoji haya
 
..mbona Mwenyekiti wa CCM anafanya ziara nchi nzima, anasimama barabarani na kuhutubia, na muda mwingi hushutumu na kudhalilisha vyama vya upinzani?

..tumeshuhudia mara kadhaa CCM wakifanya vikao vyao IKULU, lakini kuna wana CDM wamezuiwa kufanya mikutano kwenye majengo ya shule za msingi au kumbi binafsi.

..Kuna wana CDM zaidi ya 40 waliwekwa mahabusu kwa zaidi ya miezi mitatu mkoani Geita na kosa lao lilikuwa kufanya kikao cha ndani. Mahakama iliwaachia huru lakini kuna taarifa baadhi yao walikamatwa tena hapohapo mahakamani.

..kuna UKATILI na UDHALILISHAJI mkubwa dhidi ya wafuasi wa vyama vya siasa hapa nchini.
Huu ndio unyanyasaji
 
There is 'state capture' tofauti na Afrika kusini, ours has been captured by idiotic and fat pigs with very big stomachs. Inakera sana.
 
"Nikikukuta nitakushukia kama mwewe" alisema Ole Sendeka.

Source: TBC1 Dira ya mchana.

My take.
Viongozi wetu ni bora wawe wazi kama hawataki uwepo wa vyama vingi.
Akikataa tusifanye shughuli zetu kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, basi tutafanyia juu ya kichwa chake
 
Back
Top Bottom