Ole Sendeka: Kama kweli Shigongo anaidai CCM afike ofisini, sio kulalamika mitandaoni

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Salaam wanajamvi,

Nimezipata fununu kuwa, Shigongo kaahidiwa kulipwa na CCM.

Shigongo ambaye aliahidi katika andiko lake la jana kwenye gazeti la Wikienda kuwa, leo angekitaja kiwango anachowadai CCM, ameahidiwa kulipwa hivyo atapiga kimya na hatotaja anadai shilingi ngapi

Nimepata fununu kuwa gazeti la Mwananchi ndiyo limeripoti habari hii.

Kwa mliolisoma gazeti hilo, kuna ukweli?

========

Dar es Salaam. Mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Eric Shigongo na CCM wamefikia makubaliano ya malipo ya deni analokidai chama hicho tawala baada ya awali kuilalamikia sekretarieti kuwa inampuuza.

Shigongo, anayemiliki magazeti na hoteli alilalamika kwenye ukurasa wake wa facebook na malalamiko hayo kuchapishwa kwenye gazeti moja la kila wiki kuwa aliingia mkataba wa biashara na CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini chama hicho kimeshindwa kutekeleza wajibu wake na anapowatafuta wajumbe wa sekretarieti wamekuwa wakimzungusha.

Hata hivyo, Shigongo hakutaja kiasi cha fedha anachoidai CCM wala aina ya biashara aliyofanya nayo, zaidi ya kueleza kuwa makala hiyo ingekuwa na mwendelezo.

Lakini jana alifikia makubaliano na CCM. “Nimeitwa na viongozi wa CCM na tumekubaliana jinsi ya kumaliza tatizo hili,” alisema Shigongo kwa ufupi alipotafutwa na Mwananchi jana jioni.

Awali jana mchana akizungumza kuhusu malalamiko hayo, msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema chama chake hakijapokea barua yoyote kutoka kwa Shigongo na akamtaka awasilishe nyaraka zake iwapo alifanya kazi na chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema utaratibu wa kudaiana uko wazi na anayedai, hupaswa kukutana na anayemdai na akasisitiza kuwa endapo Shigongo anakidai chama hicho, awasilishe madai yake sambamba na mikataba aliyoingia badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari.

“Sitegemei alalamike kwenye mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo vyake vya habari. Kama kweli anatudai, taratibu za kudaiana zipo wazi. Afike ofisi zetu akiwa na barua yake ya madai, mikataba ya makubaliano ya kufanya kazi na kiasi cha fedha anazotudai,” alisema.

Katika madai yake, Shigongo alisema juhudi za kumpata Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ziligonga mwamba, wakati mtu pekee aliyekuwa akimkuta ofisi ndogo za chama hicho, Zakhia Meghji, ambaye ni mweka hazina aliyekuwa akimtuliza kwa maneno.

Kinana alipopigiwa simu yake ya mkononi kwa nyakati tofauti, hakupatikana na pia hakujibu ujumbe mfupi wa simu aliotumiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
sasa napata akili kwa nini MULAA hajashikwa kwa tuhuma za mauaji yale, huenda nae alikopesha chama akaambiwe ajilipe kwa kumaliza tembo wetu, haijapata kutokea kesi ya meno ya tembo ikalipwa kwa fidia, na kesi ya mauaji polisi wapige kimya kweli? kuna deni linafidiwa hapa si bure.
 
Dar es Salaam. Mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Eric Shigongo na CCM wamefikia makubaliano ya malipo ya deni analokidai chama hicho tawala baada ya awali kuilalamikia sekretarieti kuwa inampuuza.

Shigongo, anayemiliki magazeti na hoteli alilalamika kwenye ukurasa wake wa facebook na malalamiko hayo kuchapishwa kwenye gazeti moja la kila wiki kuwa aliingia mkataba wa biashara na CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini chama hicho kimeshindwa kutekeleza wajibu wake na anapowatafuta wajumbe wa sekretarieti wamekuwa wakimzungusha.

Hata hivyo, Shigongo hakutaja kiasi cha fedha anachoidai CCM wala aina ya biashara aliyofanya nayo, zaidi ya kueleza kuwa makala hiyo ingekuwa na mwendelezo.

Lakini jana alifikia makubaliano na CCM. “Nimeitwa na viongozi wa CCM na tumekubaliana jinsi ya kumaliza tatizo hili,” alisema Shigongo kwa ufupi alipotafutwa na Mwananchi jana jioni.

Awali jana mchana akizungumza kuhusu malalamiko hayo, msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema chama chake hakijapokea barua yoyote kutoka kwa Shigongo na akamtaka awasilishe nyaraka zake iwapo alifanya kazi na chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema utaratibu wa kudaiana uko wazi na anayedai, hupaswa kukutana na anayemdai na akasisitiza kuwa endapo Shigongo anakidai chama hicho, awasilishe madai yake sambamba na mikataba aliyoingia badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari.

“Sitegemei alalamike kwenye mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo vyake vya habari. Kama kweli anatudai, taratibu za kudaiana zipo wazi. Afike ofisi zetu akiwa na barua yake ya madai, mikataba ya makubaliano ya kufanya kazi na kiasi cha fedha anazotudai,” alisema.

Katika madai yake, Shigongo alisema juhudi za kumpata Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ziligonga mwamba, wakati mtu pekee aliyekuwa akimkuta ofisi ndogo za chama hicho, Zakhia Meghji, ambaye ni mweka hazina aliyekuwa akimtuliza kwa maneno.

Kinana alipopigiwa simu yake ya mkononi kwa nyakati tofauti, hakupatikana na pia hakujibu ujumbe mfupi wa simu aliotumiwa.

Chanzo:Mwananchi
 
Deni la Shigongo inawezekana lilikuwa halijulikani na Chama.Sasa aende kuonana na mtaalamu wa Propaganda.
 
Hivi ukipewa pesa za 'kazi maalumu' kama zile za kubrashia viatu unadhani accountability yake itaonekana popote!?
Ndio maana wazungu wanapinga sana rushwa na hao wachina wanakupiga risasi kabisa kwa kujihusisha nayo.
 
Malalamiko yake yamesikika kupitia vyombo vyake vya habari na mitandao. Wengine waige mfano huo wa kudai
 
Alafu mwenyekiti wao anavyodhalilisha wengine kwa madeni kumbe yeye na chama chake nao wamejaa madeni tu!
 
Back
Top Bottom