Ole sendeka aichana vilivyo hotuba ya bajeti ya Magufuli

Ole sendeka ana bifu na magufuli

Ni kweli nilimuona Ole Sendeka akiomba mwongozo kwa mtindo ule ule wa kutoa hotuba. Na alitumia maneno "Serikali ya ccm iko katika hatua zake mwisho....". Inawezekana Ole Sendeka ameamua kuutangazia umma 'tafsiri' sahihi ya nini kilifanyika juzi na jana kwenye kikao cha CC na pengine ameamua kutuandaa (pyschologically) sisi watanzania kwa kifo cha CCM.

Kwa upande mwingine, Ole Sendeka yeye sio CCM ni CCJ, na mgombea wao ni Mzee Sitta. Sasa inawezekana Sendeka na wenzake wanataka kumuandama Magufuli ili aonekane sio chochote na watanzania na hivyo kuimarisha nafasi ya mgombea wao yaani Sitta?

Mkuu huna akili kabisa hata ya kufikia kidogo umekosa!?
 
bandari mpya,uwanja wa kisasa,epz na lami ya gharama 1.6 bn per km bagamoyo to msata!double road moroco-bagamoyo!
 
Sielewi ni kwanini pengine Mhe. Christopher ole Sendeka ameamua kuomba mwongozo kwa kutumia lugha kali kiasi hicho, ambayo ingetumiwa na mbunge kutoka upande wa upinzani ingeweza kutafsiriwa ni kuendesha propaganda za siasa Bungeni. Ni wazi kuna jambo limejificha nyuma ya pazia!!!
 
Ole Sendeka anataka ajengewe km 5 tuu kwenda Kia kama sikosei wakati kuna mikoa ya kusini rami inapita wilayani tuu
Kutoka Arusha mjini hadi Simanjiro wilayani (Orkesumet) ni km 180 za vumbi kwa kupitia Majengo, Mbauda, Sombetini, Kwa Mromboo. na ni km 140 kutoka njia panda ya Kia kupitia Mirerani hadi simanjiro wilayani
 
Mwenye macho hambiwi tazama na mwenye masikio anasikia, SENDEKA kaanza zamani kuona alama za nyakati. CCM imafika mwisho wa kufikiri na kutenda inaenda kama boya.
NEC ilitoa siku 90 watu wapigwe chini zimepita, eti wametoa tena muda mpaka septemba.

Chama kinacho abdu watu si chama. Chama imara husimamia mamuzi yake, Sasa hivi watu wote wenye kufuatilia siasa za ccm hatuji CCM inaamini katika nini. sana sana ni mabingwa wa misamiati . sensdaka Kamunga mkono yule babu aliyedai hatakufa kabla CCM haijafa.

2012 panachimbika, kunawatu watakuja na hoja ya kumvua mwenyekiti kofia hiyo ili awe rais tu na si mwenyekiti wa chama.
 
Mimi nawapongeza sana CCM kwa kuwa kwa kipindi chote hiki kuwa madarakani it means wamekuwa wanaweza ku-manage changes... sio rahisi kwa chama cha miaka 50 and yet kiko-competitive... it is not easy... wewe angalia watu wenye umri huo leo hata makazini na sehemu zingine walivyo wagumu kubadika.
 
Jioni hii nimemsikia Mh. Ole Sendeka akisema wazi wazi kuwa sasa ni dhahiri Serikali ya CCM iko katika hatua za mwisho za kifo chake. Hilo limetokana na madai kuwa.

Bajeti ya Ujenzi imejikita maeneo ambayo wanatoka viongozi na watendaji wakuu wa serikali na kuacha maeneno mengine ya nchi. Ametoa mifano mbali mbali kuonyesha jinsi bajeti ilivyobagua ki-uwazi wazi. Ameomba muongozo wa mwenyekiti lakini mwenyekiti amesema atautoa baadae.

Magufuli ni bomu sana..................na sijui kwa nini watu wengi hawalioni hili..........................katika ccm kujivua gamba naye alipaswa kuwa mmoja wao...................he is very corrupt but smart enough not to twitch other corruptible colleagues.........................lest he be twitched too..........
 
anakumbuka shuka wakati asubuhi ndo inafika

Nami nimesema usemi huu, aache unafiki wa kuwasema wenzie kuwa wamefanya vibaya, kwani yeye kalifanyia nini hili Taifa. Uhodari wake wa kuongea anautumia kuwachafua wenzie. Hili nalo ni Gamba la CCM.
 
Magufuli ni bomu sana..................na sijui kwa nini watu wengi hawalioni hili..........................katika ccm kujivua gamba naye alipaswa kuwa mmoja wao...................he is very corrupt but smart enough not to twitch other corruptible colleagues.........................lest he be twitched too..........


Mkuu hizi ni tuhuma nzito!! Waweza kututhibitishia Mkuu?.
 
Kubwabwaja kwa ole sendeka wakati kapitisha na kuiunga mkono budget 100% maana yake nini!? Wamdanganya nani wewe? Nawe ni gamba tu, wapaswa uvuliwe mara moja, mnafiki mkubwa.
 
Olesendeka alipaswa kuwa muwazi kidogo siyo kusema maeneo yamepangwa kwa upendeleo ni bora angeitaja Kilimanjaro moja kwa moja ni kweli barabara nyingi za lami zipo kule,hata kama kuna M.Pinda kule Rukwa' bado ni mkoa upo nyuma sana kwa barabara za lami ikiwemo mikoa ya kigoma, Tabora, Lindi na Mtwara ambayo kwayo ndio barabara nyingi zitajengwa kwenye bajeti hii.

Hata kama angekuwa anatoka raisi kwenye mikoa hii hauwezi kusema imependelewa. AKOMAE NA MKOA WA KILIMANJARO AMBAO KIMSINGI UMEKUWA UKIPENDELEWA SANA siyo kusema bajeti nzima ina upendeleo!
 
alicho ongea Ole Sendeka ni ukweli mtupu lakini kwa kuwa ccm inaona kama inaonewa utaona watamwita Gamba
 
Sasa kupeleka barabara Butiama sio upendeleo, wakati kuna mikoa haina kabisa barabara, kama Rukwa?
Ameongea ukweli lakini hajajenga hoja vizuri

Kila barabara itaonekana imependelewa kama tutajudge anavyotaka... nadhani ingekua bora iwapo angekuja na cost benefit analysis ya choices za barabara anazotaka yeye... na pia auonyeshe hasara ya barabara asizotaka yeye
 
Ni kweli nilimuona Ole Sendeka akiomba mwongozo kwa mtindo ule ule wa kutoa hotuba. Na alitumia maneno &quot;Serikali ya ccm iko katika hatua zake mwisho....&quot;. Inawezekana Ole Sendeka ameamua kuutangazia umma 'tafsiri' sahihi ya nini kilifanyika juzi na jana kwenye kikao cha CC na pengine ameamua kutuandaa (pyschologically) sisi watanzania kwa kifo cha CCM. <br />
<br />
Kwa upande mwingine, Ole Sendeka yeye sio CCM ni CCJ, na mgombea wao ni Mzee Sitta. Sasa inawezekana Sendeka na wenzake wanataka kumuandama Magufuli ili aonekane sio chochote na watanzania na hivyo kuimarisha nafasi ya mgombea wao yaani Sitta?
<br />
<br />
Mkuu umeongea ukweli mtupu hata mimi nililiona hilo. Nilimuona Magufuli na Mwakyembe walicheka sana kisha wakateta kitu mara tu Sendeka alivyomaliza kutoa mwongozo wake.
 
huyu magufuli aliisha jenga nyumba za serikali za gharama kubwa na kuwauzia vigogo wenzake bei ya chee.so he iz always gambaz.
 
Back
Top Bottom