Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Wakuu amani iwe juu yenu,
Hili naomba niliseme wazi na Sabaya mwenyewe najua yupo humu asome na asikie ujumbe impate. Kama hataki aache lakini matokeo atayapata muda sio mrefu. Hii ni tahadhari kwake kama ana masikio asikie, kama ana ubongo aelewe.
Kuna kundi la vijana wa CCM ambalo hata mimi nikiri mimi kwenye makundi hayo, wanafanya kazi kumsema Vibaya Mhe Rais wetu chini ya uamuzi wake wa kumsimashia Sabaya nafasi ya ukuu wa wilaya, makundi haya yanamtetea Sabaya kwa hali na mali akiyaandaa yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya sana kazi wanayofanya ni kudhihaki mamlaka za nchi. Wamesahau kuwa aliyemsimamisha kazi Sabaya si Samia Suluhu Hassan bali ni Rais Samia Suluhu Hassan. Urais ni taasisi kubwa ina macho yake ya kila aina na ni mengi.
Sabaya badala ya kutulia achunguzwe tuhuma dhidi yake ili ma majibu yajulikane na badala yake anatumia vijana kumsafisha aonekane kua hana hatia. Sabaya unataka kujihami na nini? What if matokeo ya uchunguzi yakasema aliharibu pakubwa na aende jela, wasafishaji wake watenda wapi hali ikiwa hivyo. Wewe wenzako wanatulia hata ili hata kama kuna makosa yatadhihiri hata busara inaweza kutumika kumuadhibu, leo wewe unaona umeonewa na kutuma vijana kumsema vibaya Mama?
Matukio yote unayotuhumiwa nayo Sabaya ni makubwa sana ni bora kukaa kimya. Muungwa huchutama pale akoseapo. Wajanja hukaa kimya ili hata kama kuna makosa waonewe huruma lakini wewe kichwa ngumu.
Hivi wewe unafikiri Mama hana faili lako? Unafikiri hakujui vizuri? Endelea kujiona unaonewa utapata mtu wa kukurudisha kwenye nafasi yako kama si jela.