Ole Sabaya kaa kimya uchunguzwe, acha kuchonganisha mamlaka za nchi. Utaingia matatizoni

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
268
1,000
Wakuu amani iwe juu yenu,

Hili naomba niliseme wazi na Sabaya mwenyewe najua yupo humu asome na asikie ujumbe impate. Kama hataki aache lakini matokeo atayapata muda sio mrefu. Hii ni tahadhari kwake kama ana masikio asikie, kama ana ubongo aelewe.

Kuna kundi la vijana wa CCM ambalo hata mimi nikiri mimi kwenye makundi hayo, wanafanya kazi kumsema Vibaya Mhe Rais wetu chini ya uamuzi wake wa kumsimashia Sabaya nafasi ya ukuu wa wilaya, makundi haya yanamtetea Sabaya kwa hali na mali akiyaandaa yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya sana kazi wanayofanya ni kudhihaki mamlaka za nchi. Wamesahau kuwa aliyemsimamisha kazi Sabaya si Samia Suluhu Hassan bali ni Rais Samia Suluhu Hassan. Urais ni taasisi kubwa ina macho yake ya kila aina na ni mengi.

Sabaya badala ya kutulia achunguzwe tuhuma dhidi yake ili ma majibu yajulikane na badala yake anatumia vijana kumsafisha aonekane kua hana hatia. Sabaya unataka kujihami na nini? What if matokeo ya uchunguzi yakasema aliharibu pakubwa na aende jela, wasafishaji wake watenda wapi hali ikiwa hivyo. Wewe wenzako wanatulia hata ili hata kama kuna makosa yatadhihiri hata busara inaweza kutumika kumuadhibu, leo wewe unaona umeonewa na kutuma vijana kumsema vibaya Mama?

Matukio yote unayotuhumiwa nayo Sabaya ni makubwa sana ni bora kukaa kimya. Muungwa huchutama pale akoseapo. Wajanja hukaa kimya ili hata kama kuna makosa waonewe huruma lakini wewe kichwa ngumu.

Hivi wewe unafikiri Mama hana faili lako? Unafikiri hakujui vizuri? Endelea kujiona unaonewa utapata mtu wa kukurudisha kwenye nafasi yako kama si jela.
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,953
2,000
Huyu Sabaya ni mjinga sana, amewatengeneza mamluki wa kumtetea, na yeye mwenyewe kwa kupitia accounts zake za JF, amekuwa akipost kila mara mada ya kuonesha kuwa yeye ni mtu safi bali alikuwa anafanya uovu kwa sababu ya maelekezo toka kwa marehemu.

Lakini kwa hakika jibu atalipata. Rais Samia siyo mjinga. Unadhani kwa nini Hapi na Chalamila, licha ya kusemwa sana, hawajasimamishwa? Hapi na Chalamila, ni mdomoni tu, lakini hawajaua mtu wala hawajapora mali ya mtu, tofauti na Sabaya ambaye ametenda grave crimes ambazo ni lazima uwe hayawani kukubali kuwa ni mambo ya kawaida.

Vyombo vinavyochunguza, vimalize kazi haraka, Sabaya asimamishwe mahakamani, na aende wanakoishi waovu kama yeye.
 
Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
15,045
2,000
Uyo jambazi Ole Sabaya ningekuwa mchawi ningeila nyama yake uku tunaisimanga

Halafu eti ni Ukuu wa Wilaya nafasi ambayo ukiniteua mimi naikataa lakini si kwa kiburi la hasha.

Nitamshukuru mteuzi lakini nitamwambia samahani naomba mteule mtanzania mwingine kwa nafasi hiyo.

Nashangaa nafasi ndogo kama hiyo mtu mzima unalia lia kama mtoto mdogo.

Namshukuru Mungu hizi teuzi hazijawahi kukatisha udi hizi wangu.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,353
2,000
CCM mnalea haya matatizo mwishowe yanaanza kuwatafuna wenyewe, tabia yenu ya kuwapa madaraka wanaowapiga wapinzani au kuwatukana wazee wenu wastaafu mlianza toka enzi za JK, hamfai tena kuongoza hii nchi, mmeshindwa kuliondoa taifa kwenye umasikini zaidi ya miaka 60 baada ya uhuru bado watu hawana maji safi na salama mpaka leo, sasa mnaanza kuporomosha mpaka maadili ya jamii yetu, nyie ni failures.
 
Black belts

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,423
2,000
Huyu Sabaya ni mjinga sana, amewatengeneza mamluki wa kumtetea, na yeye mwenyewe kwa kuoitia accounts zake za JF, amekuwa akipost kila mara mada ya kuonesha kuwa yeye ni mtu safi bali alikuwa anafanya uovu kwa sababu ya maelekezo toka kwa marehemu...
Dunia itamshangaa madam president Samia Kama uyu Sabaya hatoshtakiwa kwa ujambazi aliokuwa anaufanya
 
Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
268
1,000
Usitishe watu mjinga wewe,eti taasisi ya Raisi ina macho mengi,danganya wajinga,acha watu waongee wanachoamini,kamtishe mkweo huko
Kwahiyo unabisha kua Ofisi ya Rais ina macho mapana? Sasa endeleeni kutumiwa na sabaya wajinga nyie. Mama ndio Rais na ni mwenyekiti wa Chama tuone mtafanya nini?

Hatuwezi kuacha kujenga taifa katika misingi ya amani na utulivu kwa sababu ya mjinga moja tena level ya DC. Akae asubiri uchunguzi ukikamilika kama hana hatia atakua huru, kama alidhulumu sheria itachukua mkondo wake.
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,804
2,000
Wakuu amani iwe juu yenu!

Hili naomba niliseme wazi na Sabaya mwenyewe najua yupo humu asome na asikie ujumbe impate. Kama hataki aache lakini matokeo atayapata muda sio mrefu. Hii ni tahadhari kwake kama ana masikio asikie, kama ana ubongo aelewe....
Hizo ni tabia za rika la Nyangoro kule umasaini, angekuwa real Laigwanani angechutama.

Ninachokijua kuhusu Sabaya ni kwamba uchunguzi utafanyika tuhuma zitathibitika (kwa sababu ziko wazi)na atashitakiwa ikibidi ataenda jela. Hatofautiani sana na James Kaji tuhuma ni kama zinafanana na ukwasi is like the same sema kaji alikuwa anapiga kimya kimya.
 
Mamy K

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
610
1,000
Kwahiyo unabisha kua Ofisi ya Rais ina macho mapana? Sasa endeleeni kutumiwa na sabaya wajinga nyie. Mama ndio Rais na ni mwenyekiti wa Chama tuone mtafanya nini?

Hatuwezi kuacha kujenga taifa katika misingi ya amani na utulivu kwa sababu ya mjinga moja tena level ya DC. Akae asubiri uchunguzi ukikamilika kama hana hatia atakua huru, kama alidhulumu sheria itachukua mkondo wake.
Hawaamini kama zama zimebadilika. Zama za ushamba wa kutekana zimeisha. Na kama wanaona hawatendewi haki watoke huko UVCCM na wengine tuingie.
Mtu analilia ukuu wa wilaya kama kazaliwa nao!
 
Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
137
1,000
Wakuu amani iwe juu yenu!

Hili naomba niliseme wazi na Sabaya mwenyewe najua yupo humu asome na asikie ujumbe impate. Kama hataki aache lakini matokeo atayapata muda sio mrefu. Hii ni tahadhari kwake kama ana masikio asikie, kama ana ubongo aelewe....
Na wewe ukae kimya uziachie relevant authorities zifanye kazi zao.
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,753
2,000
Wakuu amani iwe juu yenu!

Hili naomba niliseme wazi na Sabaya mwenyewe najua yupo humu asome na asikie ujumbe impate. Kama hataki aache lakini matokeo atayapata muda sio mrefu. Hii ni tahadhari kwake kama ana masikio asikie, kama ana ubongo aelewe.

Kuna kundi la vijana wa CCM ambalo hata mimi nikiri mimi kwenye makundi hayo, wanafanya kazi kumsema Vibaya Mhe Rais wetu chini ya uamuzi wake wa kumsimashia Sabaya nafasi ya ukuu wa wilaya, makundi haya yanamtetea Sabaya kwa hali na mali akiyaandaa yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya sana kazi wanayofanya ni kudhihaki mamlaka za nchi. Wamesahau kuwa aliyemsimamisha kazi Sabaya si Samia Suluhu Hassan bali ni Rais Samia Suluhu Hassan. Urais ni taasisi kubwa ina macho yake ya kila aina na ni mengi.

Sabaya badala ya kutulia achunguzwe tuhuma dhidi yake ili ma majibu yajulikane na badala yake anatumia vijana kumsafisha aonekane kua hana hatia. Sabaya unataka kujihami na nini? What if matokeo ya uchunguzi yakasema aliharibu pakubwa na aende jela, wasafishaji wake watenda wapi hali ikiwa hivyo. Wewe wenzako wanatulia hata ili hata kama kuna makosa yatadhihiri hata busara inaweza kutumika kumuadhibu, leo wewe unaona umeonewa na kutuma vijana kumsema vibaya Mama?

Matukio yote unayotuhumiwa nayo Sabaya ni makubwa sana ni bora kukaa kimya. Muungwa huchutama pale akoseapo. Wajanja hukaa kimya ili hata kama kuna makosa waonewe huruma lakini wewe kichwa ngumu.

Hivi wewe unafikiri Mama hana faili lako? Unafikiri hakujui vizuri? Endelea kujiona unaonewa utapata mtu wa kukurudisha kwenye nafasi yako kama si jela.
Asahau. Imetoka hiyo. Ataendelea kuuota tu u-DC akiwa huru au jela.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom