Ole Sabaya hata kama alikuwa na hatia lakini sio ya unyag'anyi wa kutumia silaha. Hakimu aliyehukumu hana weledi

Kila siku mahakimu kama hawa wanaumbuka High Court.
Ni uwendawazimu kufanya jambo kwa dhamira eti ya kumwua mtu. Kama anadhani ana haki ambayo haikuzingatiwa, akate rufaa kwa dhamira ya kuitafuta haki yake.

Akikata rufaa kwa dhamira ya kumwumbua hakimu, ataishia kuumbuka yeye kama ulivyoumbuka wewe uliyekuwa kila siku unapiga porojo za kumtetea mtu mwovu hapa JF.

Sabaya ni mtu mwovu, jambazi, mtesaji na muuaji. Asubiria kesi nyingine ambazo zitazidi kumpa makazi yake ya kudumu gerezani. Hili jitu ni shetani. Mtu mwenye Roho wa Mungu, kamwe hawezi kuwapigilia misumari miguuni binafamu wenzake au kuwakata masikio, kama hili jambazi lilivyokuwa likiwafanyia watu.

Uraiani ni kwa watu wema hata kama siyo watakatifu, jambazi kama Sabaya, mahali pake sahihi ni gerezani,
 
Nimesoma baadhi ya nukuu za hakimu Amworo anakiri kuwa Sabaya alikuwa na siraha eneo la tukio . Lakini hii sio sababu ya kudai kuwa alitenda unyang'anyi wa kutumia siraha.

Ili unyang'anyi wa kutumia siraha utimie lazima mtuhumiwa atishie kwa siraha, kutumia siraha na kisha kupora mali. Ukifuatilia kesi ya Sabaya utaona kuwa hakuna mahala hili linasithibitishwa.

Lakini hata mashahhidi wa mashitaka wanakiri kuwa Sababya na wenzake walikwenda na magari ya serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. Hapa ndipo utaona kama kuna walakini, maana hata mkuu wa wilaya ya Arusha wakati huo alifahamu.

My take; Mahakimu wanaofanya kazi kwa kukariri hawafai.
Basi hapo mwenyewe umejiona nooooooooooooma
 
Hakimu hajafanya kazi kwa kukariri. amefanya kazi kwa kuzingatia gap zilizokuwepo kwenye ushahidi wa Sabaya na tafsiri yake kisheria.

Kitendo cha Sabaya kukiri kumiliki silaha, hata kama ni kwa ulinzi wake binafsi, na kuwa nayo siku ya tukio alipoingia ofisini kwa watu bila kibali kinachotambulika kisheria, hapa ndipo alipoharibu. Mahakama ilitafsiri hili amefanya uvamizi wa kutumia silaha.

Kwasababu unapoingia ofisini kwa mtu na silaha, hata kama huja point kwa muhusika, lakini psychologically unakuwa na advantage mbele ya muhusika, anaingiwa hofu kwa kuiona ile silaha uliyonayo, so unaweza muamrisha chochote na akatii kwa hofu ya silaha uliyonayo usije kumdhuru.

Silaha kuwa ndio "ingredient" muhimu kwenye kesi yake, alitakiwa kwenye utetezi wake either;

1. Akatae kabisa kumiliki silaha yoyote ya moto.

au

2. Akubali kumiliki silaha LAKINI hakuwa nayo siku ya tukio.

Huo utetezi wa pili ungesaidia kumsogeza mbele kwa kuisumbua mahakama itafute mashahidi wa ku-prove kwamba siku ya tukio kweli alikuwa na silaha.

Ili mahakama iamue jambo, lazima kuwe na ushahidi usioacha shaka, na huu ushahidi mostly ungetakiwa uje toka kwa third parties, hapa wangeweza kuwahonga mashahidi kama walikuwepo na kesi ingeishia hapo, au angepewa hukumu ndogo kama ingethibitika aliingia kwa watu bila kibali ila hakuwa na silaha.

Lakini kwa kukiri kwake kuwa na silaha eneo la tukio bila kibali alijimaliza mwenyewe, alimpunguzia hakimu kazi kwa kiasi kikubwa sana, mawakili wake hawakum "coach" vizuri kwenye hili.
Kiburi chake hapa kwenye silaha, kilichangia kummaliza. Alijiona akisema aliingia na silaha "kwake" siyo shida. Amekua akiingia mahakamani akiwa bado ana ile "image ya mtoto wa baba"
 
Sasa hiyo silaha aliyo kuwa nayo eneo la tukio, ilikuwa ni kwa ajili ya nini? Kuwalingishia hao wafanyabiashara?

Halafu unakili mwenyewe 'hata kama Sabaya ana hatia......!! Sasa si ndiyo hiyo ya unyang'anyi wa kutumia silaha!!

Hata kama alitishia tu, bado sheria iko pale pale! Miaka 30 jela, na viboko juu.
Hili jambazi lilistahili na lenyewr kupigiliwa misumari kama lilivyowatendea wengine.

Na bado kuna kesi nyingine nyingi zitakuja. Hili kwa kushirikiana na akina Kingai ndio waliomwua Lijenje.
 
Mabwanyenye wa kimachame waliyopanga kulipa kisasa kwa mwanamapinduzi sabaya kwa kazi ya kizalendo kwa taifa wajitayarishe kukosa hii raha wanaona saa hizi. Kwenye rufaa bila shaka ndio haki itatendeka.
Mjane unaweweseka.
FB_IMG_1634450109028.jpg
 
Nimesoma baadhi ya nukuu za hakimu Amworo anakiri kuwa Sabaya alikuwa na siraha eneo la tukio . Lakini hii sio sababu ya kudai kuwa alitenda unyang'anyi wa kutumia siraha.

Ili unyang'anyi wa kutumia siraha utimie lazima mtuhumiwa atishie kwa siraha, kutumia siraha na kisha kupora mali. Ukifuatilia kesi ya Sabaya utaona kuwa hakuna mahala hili linasithibitishwa.

Lakini hata mashahhidi wa mashitaka wanakiri kuwa Sababya na wenzake walikwenda na magari ya serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. Hapa ndipo utaona kama kuna walakini, maana hata mkuu wa wilaya ya Arusha wakati huo alifahamu.

My take; Mahakimu wanaofanya kazi kwa kukariri hawafai.
Kitendo tu cha kuwa na silaha wakati unataka kupora tayari ni ujambazi wa kutumia silaha. Sabaya kama kiongozi (DC) angeenda pale na polisi wakiwa na silaha ingeeleweka. Lakini yeye kwenda pale na watu wengine ambao si askari na kumlazimisha mtu kutoa fedha tayari status ya tukio inabadilika.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
High Court anachomoka zote. Wakati utaprove.
Kama mahakama kuu kuna wanafiki kama wewe, basi msubirie. Anza maandalizi ya sherehe ya kumpokea.

Unahangaika na nini wakati una uhakika wa kuungana na mpendwa wako ili muendeleze unyama wenu? Tulia umsubirie, halafu uje uwalingishie JF ukiwatumia picha ya pamoja ya sherehe ya kumpokea.
 
Nimesoma baadhi ya nukuu za hakimu Amworo anakiri kuwa Sabaya alikuwa na siraha eneo la tukio . Lakini hii sio sababu ya kudai kuwa alitenda unyang'anyi wa kutumia siraha.

Ili unyang'anyi wa kutumia siraha utimie lazima mtuhumiwa atishie kwa siraha, kutumia siraha na kisha kupora mali. Ukifuatilia kesi ya Sabaya utaona kuwa hakuna mahala hili linasithibitishwa.

Lakini hata mashahhidi wa mashitaka wanakiri kuwa Sababya na wenzake walikwenda na magari ya serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. Hapa ndipo utaona kama kuna walakini, maana hata mkuu wa wilaya ya Arusha wakati huo alifahamu.

My take; Mahakimu wanaofanya kazi kwa kukariri hawafai.
Kumbuka kuwa kesho akiwa ndani ya vazi jipya la rangi ya njano atakuwa mahakamani kukabili shtaka lingine la uhujumu uchumi.
 
Kiburi chake hapa kwenye silaha, kilichangia kummaliza. Alijiona akisema akiingia na silaha "kwake" siyo shida. Amekua akiingia mahakamani akiwa bado ana ile "image ya mtoto wa baba"
Hakujua mahakama sio kanisani au msikitini ukiiambia ukweli itakusamehe, pale ukisema kweli hakimu anachofanya ni kuangalia sheria inasemaje kuhusu kosa husika na adhabu yake ni ipi, then anakutwanga miaka yako ananyanyuka anaondoka.
 
Nimesoma baadhi ya nukuu za hakimu Amworo anakiri kuwa Sabaya alikuwa na siraha eneo la tukio . Lakini hii sio sababu ya kudai kuwa alitenda unyang'anyi wa kutumia siraha.

Ili unyang'anyi wa kutumia siraha utimie lazima mtuhumiwa atishie kwa siraha, kutumia siraha na kisha kupora mali. Ukifuatilia kesi ya Sabaya utaona kuwa hakuna mahala hili linasithibitishwa.

Lakini hata mashahhidi wa mashitaka wanakiri kuwa Sababya na wenzake walikwenda na magari ya serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. Hapa ndipo utaona kama kuna walakini, maana hata mkuu wa wilaya ya Arusha wakati huo alifahamu.

My take; Mahakimu wanaofanya kazi kwa kukariri hawafai.
Bongo bana,hujui hata kuandika lkn unakosoa mahakimu walosomea!!! Ujinga wako bakinao mwenyewe jombaa...
 
High Court anachomoka zote. Wakati utaprove.
Mkuu una imani sana. Hongera..... Kwa nini huwezi kuona madudu ya Sabaya? Hayo ni ya Arusha tu, kuna ya Moshi/Hai, huyu mtu hafai kutetewa ndugu. Kuna ambao hawajaamua tu kuyafikisha mahakamani.

Kuna issue ya kuvamia Hotel ya Weruweru River Lodge ya Asante Tours inayomilikiwa na Cathbert Swai, kuna ushahidi wa CCTV cameras, hii haijafika mahakamani bado. Ni tukio la aibu. Mkuu, moyo wa kujaribu kumuona Sabaya ni msafi unatoka wapi?
 
Back
Top Bottom