Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,314
- 24,173
Hukumu iliyotolewa jana kwa Ole Sabaya, kuwa alikuwa jambazi la kutumia silaha kupora mali za wananchi, vile vile limeupaka matope utawala wa Magufuli.
Kwamba mteule wa Rais, akafanya mambo kinyume na utawala wa sheria na mbaya zaidi ujambazi, ni vigumu kueleweka kirahisi kwa nini haya yaliruhusiwa kutokea.
Utawala wa Magufuli mara kadhaa umelaumiwa kutoheshimu haki za binadamu na mali zao, huu mfano wa Sabaya umejitokeza kukubaliana na hoja hizo.
Kwamba kulikuwepo na wasiojulikana, watu kutekwa na baadaye aidha kupotea au kurudishwa na wasiongee yaliyowasibu, hili la Sabaya linathibitisha uhusika wa viongozi fulani, ndani ya Dola, wakiwa na baraka " kutoka juu".
Kwa vyovyote vile Ole Sabaya ni doa jeusi na ambalo si zuri kwa utawala wa Magufuli.