Ole Sabaya: Doa jeusi kwa utawala wa Hayati Magufuli

Wahenga walisema kuwa kila masika na mbu wake.

Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha hapa duniani.

Tazameni jinsi vijana hawa walivyo kuwa wanakula nchi na majivuno kibao.

Leo hii mida hii anagombea kupanga foreni na bakuli la ammonium akapate ugali. View attachment 1980933
Naona wameimerge humu ndani mkuu wangu.....

2969622_images_9.jpeg
 
Yeye akijisafisha basi serikali itakuwa imepakwa kinyesi, Wananchi tutaamini alichokisema Sabaya kwamba alikuwa anatumwa na mamlaka iliyo juu yake.
Sasa sijui Kama hiyo serikali itakuwa na uhalali wa kuendelea kuwepo hata ikiwepo sijui Kama Kuna mwananchi atakuwa na imani nayo.
Kitu cha kushangaza wengi wanao mponda Sabaya ni walewale wanao mshabikia Hangaya.
Yaani wanasahau Hangaya ni moja ya serikali iliyokuwepo kipindi cha Sabaya.
 
Kitu cha kushangaza wengi wanao mponda Sabaya ni walewale wanao mshabikia Hangaya.
Yaani wanasahau Hangaya ni moja ya serikali iliyokuwepo kipindi cha Sabaya.
Tumnyonge mnyonge ila haki yake tumpe,unadhani angekuwepo naniii yule hii kesi ya Sabaya ingekuwepo?
 
Mleta mada usisahau kuwa 90% ya top Govt Officials wa sasa ni wateule wa our beloved The Late Magufuli kuanzia Rais Mamá Samia, Dr Mpango, PM Majaliwa, Jaji Mkuu Prof Ibrahim, DG Tiss, CDF, IGP na wengine wengi

Maamuzi ya kesi ya Sabaya isiihusianishe na mkuu wa Serikali iliyopita ilhali watendaji wakuu wengi kama nilivyowataja wenye influence bado ni wale wale toka awamu iliyopita na ni wenye kiwango kizuri cha kukubalika kwa maana ya utendaji wao ktk nchi yetu

Kama Sabaya alifanya makosa basi acha hukumu imuhusu yeye kama yeye

..swali nj kwamba ilikuwaje Sabaya akafanya mambo yote hayo bila wakubwa zake kumchukulia hatua?

..utakumbuka kwamba kipindi cha Magufuli wateule mbalimbali walikuwa wanafuatiliwa kwa karibu, na hata mawasiliano yao kudukuliwa.

..Mara kwa mara Magufuli alinukuliwa akisema anajua kila wanachofanya wateule wake.

..Na zipo kumbukumbu za DC aliyetumbuliwa kwa sababu ya tabia mbaya ya ugoni. Sasa ilikuwaje DC mgoni atumbuliwe, halafu DC jambazi aachwe atambe anavyotaka?
 
Tumnyonge mnyonge ila haki yake tumpe,unadhani angekuwepo naniii yule hii kesi ya Sabaya ingekuwepo?
Sawa isingekuwepo ila mpo tayari mumkingia kifua Hangaya asihusike?
Na mnakumbuka Sabaya alivyo mtaja Mpango na yule wa sijui wa BoT
 
Sawa isingekuwepo ila mpo tayari mumkingia kifua Hangaya asihusike?
Na mnakumbuka Sabaya alivyo mtaja Mpango na yule wa sijui wa BoT
Tupo tayari na nani? Mimi simuwakilishi mtu yeyote nasema hivyo kwa utashi wangu,sipo tayari kumkingia kifua Ila angalau kaonyesha hakuridhishwa na maaamuzi ya Boss wake, sio yeye tu wapo wengi.
 
Mbowe yeye anatuhumiwa kupanga mipango miovu ya kuvuruga AMANI YA nchi. Sasa wewe jiulize mtu anaye taka kuvuruga amani ya nchi unajua madhara yake ni makubwa kiasi gani?! Ni hatari kubwa sana na kama akikutwa na hatia anastahili adhabu kali zaidi ili iwe fundisho kwa wanasiasa wengine wanao jaribu kuchezea amani ya nchi.

Yaani huwezi kulinganisha makosa ya unyanganyi, n.kna makosa ya Mbowe ya kupanga njama za kuvuruga amani ya nchi, Amani ya nchi ndio inayotufanya leo tunafurahia haki kutendeka, amani ya nchi ndio mpango mzima, leo hii Mbowe na Genge lake la kihalifu wanadaiwa kupanga njama za kuvuruga amani ya nchi iliyo tengenezwa na kulindwa kwa zaidi ya miaka 60!!

Amani ya nchi yetu ni ya thamani kubwa sana kuliko mbowe au mtu yeyote yule, atakaye bainika kuchezea amani yetu atashughulikiwa bila huruma.
Naunga mkono hoja. MBOWE alitaka kuiteka nchi kwa kutumia silaha kali sana aina ya Lugar yenye risasi tatu
 
Hukumu iliyotolewa jana kwa Ole Sabaya, kuwa alikuwa jambazi la kutumia silaha kupora mali za wananchi, vile vile limeupaka matope utawala wa Magufuli.

Kwamba mteule wa Rais, akafanya mambo kinyume na utawala wa sheria na mbaya zaidi ujambazi, ni vigumu kueleweka kirahisi kwa nini haya yaliruhusiwa kutokea.

Utawala wa Magufuli mara kadhaa umelaumiwa kutoheshimu haki za binadamu na mali zao, huu mfano wa Sabaya umejitokeza kukubaliana na hoja hizo.

Kwamba kulikuwepo na wasiojulikana, watu kutekwa na baadaye aidha kupotea au kurudishwa na wasiongee yaliyowasibu, hili la Sabaya linathibitisha uhusika wa viongozi fulani, ndani ya Dola, wakiwa na baraka " kutoka juu".

Kwa vyovyote vile Ole Sabaya ni doa jeusi na ambalo si zuri kwa utawala wa Magufuli.
Hizo baraka za kutoka juu ndio haswa doa jeusi linalozungumziwa. Penye ukweli hatuna budi kusema.
 
Back
Top Bottom