Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai lengai ole sabaya amekana kumtambua mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyemwapisha baada ya kuteuliwa Kwa kuieleza mahakama kwamba kesho yake ndo alijua kuwa aliyemwapisha alikuwa ni mkuu wa Mkoa.
Akihojiwa na Wakili mkuu wa serikali , Tumaini Kweka,Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,katika Kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha na Kumpora Mali na fedha inayomkabili ,Sabaya na wenzake wawili ,alisema siku iliyofuata ndio alitambua kuwa aliyemwapisha ni Marehemu Anne Mghwira aliyekuwa mkuu wake wa Mkoa wa Kilimanjaro
WAKILI Kweka anasema Lengai Ole Sabaya alihojiwa na Tume ya Binadamu na Utawala bora Mei 6 mwaka huu juu ya vijana wanne aliokuwa akiwatumia ofisni kwake wakati sio waajiriwa wa umma.
Kweka aliyasema hayo wakati akimuhoji shahidi huyo (Sabaya) baada ya kumaliza utetezi wake katika kesi inayomkabili yeye na wenzake wawili ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Alidai kuwa siku hiyo (Sabaya) akiwa ofisini kwake alipata ugeni huo ambao ulifanya mahojiano naye.
“Katika mahojiano hayo uliulizwa kwanini unatumia vijana ambao sio watumishi wa umma katika ofisi yako,”alidai Kweka.
Sehemu ya mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo:
Wakili:Ebu shahidi eleza mahakama kuwa 9/2/2021 ukiwa katika kikao chako ofisini kwako baada ya saa 9:00 kumaliza kazi zako ulipokea simu kwa mamlaka ya juu ya uteuzi iliyokuteua
Shahidi:Ndio
Wakili:Majukumu,cheo vipo kisheria na majukumu yake yameanishwakisheria unakubaliana na mimi
Shahidi:Nakubaliana na wewe
Wakili:Utakubaliana na mimi majukumu yalioainishwa kisheria sipo siri
Shahidi:Siyo
Wakili:9?2/2021 umeeleza ulifika majira ya saa 11:45 jioni Arusha na timu yako?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Ulisema mlienda kwenye duka la Mohamed Saad kw amaelekezo uliyopewa
Shahidi:Sijasema
Wakili:Ulisema ulipofika dukani hapo mlikuta vijana wawili wanauza je walikuwa wnauza sehemu gani wewe kama msomi mwenye digrii?
Shahidi: Nilisema tulikuta vijana wawili sijasema eneo gani
Wakili:unajua asili yao
Shahidi:Sijuwi
Wakili:Je Bakari Msangi unamfahamu aliyekuja mahakamani hapa kutoa ushahidi na ulimfahamu lini?
Shahidi:Namfahamu tangu mwaka lipogombea nafasi ya mwenyekiti Umoja wa Vijana CCM (UVCCM)
Wakili:Unakumbuka 6 Mei mwaka 2021 ulipata ugeni wa Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa mahojiano na walifanya mahojiano yakawaida na wewe
Shahidi:Sijuwi
Wakili:Hiyo 9/2/2021 maelekezo uliyopewa na mamlaka ya juu ya uteuzi walikueleza nini ukahoji kwenye duka la Mohamed Saad
Shahidi:Niliseleza tulipotoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na hao watu niliokuw anao walikuwa na maelekezo yao
Wakili:Kati ya hao mlioenda nao kama timu walikuambia bila shaka kuwa mchukue mtakaowakuta
Shahidi: haikuwa maelekezo yoyote
Wakili:upo mahakamani unadaiwa ulitenda nini 9?2/2021
Shahidi:Sijatenda
Wakili:SWali moja wapo uliloulizwa na tume iliyokutembelea ofisini kwako ya Haki za Binadamu na Utawala bora walikuuliza kwa nini unatumia vijana wanne kwenye ofisi za umma wakati sio watumishi
Shahidi:Sikuulizwa swali hilo wala sikumbuki
Wakili:Unaweza kueleza aliyekuapisha anaitw anani
Shahidi:Simjuwi
Baada ya Shahidi kujibu jibu hilo Hakimu Odira alilazimika kuingilia kati na kuwaomba mawakili wake wa utetezi kumwelekeza shahidi wao (Sabaya) kujibu maswali anayoulizw akw aufasaha, sababu hawezi kushindwa kumfahamu aliyemuapisha kuwa Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo baada ya mahojiano hayo kufika muda waliokubaliana kumaliza saa 10:00, Wakili Kweka aliomba kuahirisha kesi hiyo hadi kesho atakapoendelea na mahojiano yake na shahidi huyo.
Kesi imeahirishwa hadi leo itakapoendelea na mahojiano kati ya shahidi huyo na Wakili Kweka na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu katika Gereza kuu Kisongo Arusha.
Awali Sabaya katika utetezi wake alidai kwenda kwenye duka la Mohamed Saad ambako kumetokea wizi wa fedha anazodaiwa kuiba katika kesi hiyo kwa maelekzo ya mamlaka ya uteuzi juu
Ole Sabaya, ambaye ni mshatikwa wa kwanza katika kesi ya jinai namba 105, yenye mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha, alidai aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk.John Magufuli, alimpa agizo la kwenda kufanya opareshi maalumu katika duka la Mohamed Saad.
Alidai aliyekuwa Rais hayati Dk.John Magufuli, alinipa agizo la kwenda kufanya kazi maalumu katika duka Mohamed Saad, lililopo eneo la soko kuu jijini Arusha, akiwa ameambatana na watu wanne ambao walitumwa kujiunga naye kutekeleza agizo la Mamlaka yake ya uteuzi.
Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine katika shauri hilo, la jinai ni Silvester Nyegu(26) na Daniel Mbura (38), wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.