Dunamist
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 474
- 682
Meneja wa kampeni wa mgombea wa CCM Julius Kalanga katika uchaguzi wa marudio katika jimbo la Monduli mbunge wa Ngorongoro na naibu waziri wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema wana Monduli wamepata nafasi ya kufanya masahihisho baada ya kufelimtihani mwaka 2015.
"Sasa tumekuja kwenu mfanye marekebisho ya mtihani wa 2015, tumemleta tena Kalanga akitoka katika chama ambacho hakina ilani ya kuwaletea maendeleo, hii ni fursa ya kufanya masahihisho" Alisema Ole Nasha. Ole nasha alisema Kalanga ndiye chaguo sahihi kwa wana Monduli
Katika uchaguzi huo wa marudio,wabunge 16 wa CCM wametia kambi jimboni humo kupambana na waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya CDM bwana Edward Lowassa ambaye yuko bega kwa bega na mgombea wa CDM ndugu Yonas Laizer.
Source: Mwananchi