Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,333
Habari Leo
MKURUGENZI wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Emanuel Ole Naiko, ameituhumu Kamati Teule ya Bunge kwa kumhusisha na kashfa ya Richmond huku akisema anaamini ilifanya hivyo kwa nia ya kumkomoa kwa vile yeye ni mzaliwa wa Monduli.
Akizungumza jana, Ole Naiko alisema kulikuwa na njama za makusudi zilizokuwa zinafanywa na Kamati hiyo ya Bunge kumhusisha yeye, TIC na mkataba uliofanywa kati ya Serikali na kampuni hiyo ya kuzalisha umeme wa dharura ambao umelisababishia Taifa hasara ya mabilioni.
Katika mapendekezo yake yaliyowasilishwa bungeni mapema mwezi huu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema Mkurugenzi wa TIC na maofisa wengine walioshiriki katika kuipa upendeleo Richmond wawajibishwe kwani walitenda hivyo kinyume cha sheria.
Akizungumzia suala hilo jana, Ole Naiko alisema yeye binafsi alianza kuhisi kwamba kamati hiyo ilikuwa inamtafuta kumhusisha yeye na TIC katika sakata hilo baada ya kupokea barua ya pili ya kamati iliyomtaka awasilishe vitabu vyote vya wageni tangu mwaka 2006 hadi 2007.
Barua hii ilinifanya nihisi kwamba kulikuwa na hila za kutuhusisha na sakata hilo, alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa Nililazimika kumwandikia Katibu wa Bunge kulalamikia summons za namna hiyo ambazo zilikuwa zinaonyesha nia mbaya ya kunitafutia kosa sikujibiwa.
Akichambua kile alichokiita nia mbaya ya kamati; Ole Naiko alisema alishtuka baada ya kamati hiyo kumwita ofisa mmoja wa kituo hicho kwa sharti kuwa asiijulishe menejimenti juu ya kuitwa kwake.Sisi hatukuwa na la kuficha mimi namwachia Mwenyezi Mungu suala hili. Katika mazungumzo yake, Mkurugenzi huyo alirejea kauli iliyotolewa na Kiongozi mmoja wa Kanisa mjini Monduli mwishoni mwa wiki akitahadharisha kuwa Watanzania wasihusishe suala la Richmond na watu wanaotoka Wilaya ya Monduli.
Alisema hatari hiyo ni kujenga chuki kwa watu kutoka Monduli na nchi inaweza kutumbukia kwenye migogoro ya kikabila. Alisema kumhusisha Mmasai ama watu wa Monduli na Richmond itaifanya jamii ichukie baadhi ya wananchi kwa sababu tu wanatoka sehemu fulani ya nchi.
Huku akimnukuu Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere, Ole naiko alisema chuki za namna hiyo ni sawa na mtu kula nyama ya mtu haishii hapo. Kama nia ni kuondoa watu wa sehemu fulani ya nchi serikalini, tufanye hivyo kwa kuwatendea haki na siyo kuwajengea mazingira ya namna hii.
Mkurugenzi huyo alisema shutuma kwamba TIC iliwapa upendeleo Richmond zimejengeka katika maswali ambayo mmoja wa wakurugenzi wa Richmond Naeem Gire, alipohojiwa na Kamati ya Bunge. Alisema maswali hayo yalilenga kudhihirisha kwamba Richmond ilipewa umuhimu pekee kuliko wawekezaji wengine jambo ambalo sio la kweli.
Hata hivyo aliongeza kuwa hakuna dhambi kwa kituo hicho kumpokea mwekezaji kama mfalme; Sisi kwetu wawekezaji ni wafalme awe Richmond ndio sababu tulipata tuzo ya dunia 2007 kwa kuwakaribisha wawekezaji.
Ole Naiko alisema kituo chake kimesikitishwa na taarifa ambayo ilijaribu kuifanya jamii iamini kuwa kilipinda taratibu kuipa cheti cha uwekezaji kampuni ya Richmond. Alisema hakuna kosa lolote lile kwani wawekezaji hao walikwenda wakiwa wametimiza masharti yote yanayotajwa na sheria.
Vielelezo hivyo ni cheti cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni (BRELA) cha Julai 12 2006, leseni ya biashara iliyotolewa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, mpango wa biashara ulionyesha mchanganuo wa mradi, hati ya TRA inayoonyesha ilisajili kulipa kodi, fomu ya maombi yenye kiapo na barua ya benki na ushahidi kwamba wana fedha za kutekeleza mradi huo.
Alihoji, baada ya mwekezaji huyo kusajiliwa na vyombo vingine vya serikali, TIC ingelikuwa na kigezo gani kuwachelewesha ama kuwafanyia due diligence kuna tofauti gani kati ya TIC na hivyo vyombo vingine vilivyo wasajili? Mbona vyenyewe havilaumiwi?
Akionyeshwa kukerwa na shutuma za kamati kwa TIC, Ole Naiko alisema Mkataba wa Serikali na Richmond haujawahi kupokewa TIC wala hakukuwa na haja ya kituo hicho kupata mkataba huo kwani suala la mkataba linashughulikiwa na mamlaka nyingine. Alisema kama ni kosa kuipa cheti cha uwekezaji Richmond, basi kosa hilo haliwezi kuisha TIC bali kosa hilo litasambazwa kwa mamlaka zote zilizoipa Richmond usajili wa namna moja ama nyingine.