Ole Naiko: Inabidi tuwasamehe kodi wachimba madini kwa sababu wanazalisha umeme!

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,592
1,599
Ole Naiko amesema kuwa wanawasamehe kodi wachimba madini kwa sababu kule porini kwenye migodi serikali haijapeleka umeme, hivyo serikali inaamua kuwasamehe kulipa kodi kwa sababu wanazalisha umeme wao wenyewe ambao wanautumia huko migodini.

Hivi kwa kuwasamehe kodi wachimba madini tutafika kwenye hayo maisha tuliyoahidwa? I mean Maisha bora kwa kila Mtz.

Source: Channel ten
 
mmmh, kuna sababu ya kuwasamehe kodi wachimba madini huku wafanyakazi wakikatwa kodi lukuki?
 
mmmh, kuna sababu ya kuwasamehe kodi wachimba madini huku wafanyakazi wakikatwa kodi lukuki?

Du hii nchi bana. Wasamehewe ya nini? Si wanakuwa wamesevu bill ya Tanesco? These people are not seriours pamoja na bei ya dhahabu kupanda sana soko la dunia. Yetu macho.
 
Ni kodi ipi kwaza wanasamehewa? Kuna kodi nyingi, iko kodi wakati unatafuta madini (Mrahaba 3%) na kodi wakati unachimba madini (Corporate tax, VAT, PAYE, SDL etc.
 
Naiko is another product of luck and default placement of staff regardless of appraisal nor qualities
 
hawa ndio viongozi wetu ..duh inasikitisha na kushangaza sana.

Kama wanazalisha umeme wao maana yake si hawalipi tanesco? kama wangekuwa wanalipa tanesco si ndio gharama hizo hizo tu wanazotumia kwa umeme wao wenyewe? hivi hawa viongozi wetu wana akili gani? au bongo zao zinafanya kazi kweli kweli.

sioni ajabu kuona ka-nchi bado ni masikini kila siku kumbe tuliowaweka ndio sababu kubwa ya yote
 
Hivi mnafahamu Ole naiko ana nyumba Botswana, Nyumba aliojengewa na muwekezaji wa Mlimani city? Huyu jamaa ni fisadi wa kutupa...!
 
hawa jamaa ndio wanazidi kuimaliza nchi..misamaha mpaka lini?
Halafu haiingii akilini kabisa eti kwa sababu hatumii umeme wa TANESCO basi asilipe kodi, kana kwamba umeme wa TANESCO ni huduma inayotolewa bure. Jamaa alisoma wapi huyu?
 
sometimes mmasai ni mmasai, alikuwa anafikiri nn hadi aseme hili? yaani wasilipe kodi? hero umejisahau Dar, u r too low, period
 
Ni lini tena amepewa kazi baric!!! Du hawa viongozi wetu wanapachikana tu kwenye ulaji!!!
 
Mbona baba yangu analipa kodi na umeme hana? Huyu jamaa ana akili timamu?
Akili timamu itoke wapi? ndio mafisadi wenyewe hao; baada ya kelele za muda mferu leo ndio wanauza sura eti wamegawa madawati ya 15m: hakuna chchote hapo amestaafu serikalini kaingia kwenye dhahabu: anyway tz zaidi ya uijuavyo.
 
Sasa ndio napata picha ya kauli hii. Tanzania ina safari ndefu.


Tulawaka wanakaribia kufunga - mashimo matupu yamebaki, kodi hakuna!. Kuna uozo wa hali ya juu TIC na kama kweli Dr Mgimwa anataka kuengeza mapato anatakiwa apitie orodha ya makampuni yote yenye certificate toka TIC. Hapa ndipo nchi inageuzwa kama shamba la bibi.

Kuteuliwa kwa huyu Ole Naiko kunaibua umuhimu wa kuwa na miiko ya uongozi. Wameuwa Azimio la Arusha lakini hawakuweka chochote.
 
Majitu mengine ni mapumbafu 2. wanazalisha umeme wapi? Huo umeme si unawanufaisha wao zaidi kwenye mitambo yao? Yaani wapore dhahabu zetu bure eti kisa wanazalisha umeme. Huo umeme unawanufaisha watanzania wangapi ukilinganisha na kiasi cha dhahabu wanacholamba? mengine ni ya kuchapa makofi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom