Ole Mushi: Kutojaliwa upinzani kuanzia Serikali, taasisi za dini nk kuna dalili kutengeneza uasi na kujitoa muhanga. Ugaidi unatengenezwa na Serikali

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
KUNA JAMBO LA KUONGEA KAMA TAIFA HAPA.

Na Thadei Ole Mushi.

Niliwahi kuandika Mara Moja tu kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Niliandika Sababu ya watu kutokutaka kujiandikisha. Leo naomba niandike tena kidogo kuhusu uchaguzi huu.

Naandika haya nikiwa ni mwanaccm, naandika haya nikiwa ni Mtanzania. Kama kuna atakayesema Mimi sio ccm au sio mtanzania kwa nitakachoandika namruhusu tu kusema kwa kuwa ndio Uhuru wenyewe wa kujadiliana kwa mustakabali mpana wa Nchi yetu Mimi na wewe.

Naona kila siku wapinzani wanalalamika kuhusu kuonewa, kutokutendewa haki nk. Sijui ni kwa kiasi gani hawajatendewa haki lakini hebu tujadiliane kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Kuna ujumbe nimeuona wa Askofu Bagonza, sijui chama chake lakini nimeona kama ana Mantiki katika alichokiongea.

Askofu Bagonza kuna jambo ambalo ameligusa kuwa Upinzani umesusiwa na kila Mtu, waandishi, viongozi wa dini, asasi za kiraia, Serikali yaani kila mtu kawasusia. Askofu Bagonza katumia neno "stigmatization" (the act of treating someone or something unfairly by publicly disapproving of them) kwa Lugha ya Kikwere ni hali ya kutomtendea haki tena na hadhara yaani kila mtu anakudharau.

HILI KWANGU NI LOGIC.

Hivi mnafikiri kwa nini Watu hujinyonga? mnafikiri kwa nn watu hujitoa mhanga? Chukulia mfano huu Binti aliyekuwa anasoma anapata ujauzito, nyumbani kila mtu akamtenga kuanzia baba, mama, ndugu zake nk. Akienda shuleni hadi marafiki wanamtenga kwa kifupi huyu anapata shambulio la kisaikolojia na kitakachotokea aidha atajidhuru au atadhuru wengine.

LOGIC

Najua kuna wana CCM hawatanielewa, anyway Mwanamikakati wa Jeshi la China Sun Tzu katika kitabu chake cha art of war aliwahi kusema " To a surrounded enemy, you must leave a way of escape" akiwa na maana kuwa usimbane adui kila pembe mpe nafasi ya kutoroka. Ukimbana kila pembe hatakubali kufa kirahisi atapambana kujiokoa na anaweza kukuletea madhara. Wakati mwingine hata kama adui una uhakika wa kumpiga mwachie nafasi ya kutoroka utakuwa umepata ushindi mkubwa bila kutumia nguvu.

SIKIA.

Sikuwahi kusoma Falsafa au Saikolojia kwa kiwango kikubwa sana, nilisoma katika ngazi za awali nikachepukia kwenye masomo ya ujalalani huku kwenye chaki na madaftari aliyokimbia Prof Kabudi ila nitawaambia kitu kidogo sana kwa mustakabali wa taifa hili Siku za usoni.

Kuna faida Kubwa sana ya wapinzani kutokuwatenga na kila kitu, wanapatwa ugonjwa wa Sonoma, Sijui ni kwa kiasi gani wametendwa kama wanasingizia au kweli wamefanya makosa ila kuna kila sababu ya kuwasikiliza, kuna kila sababu asasi za kiraia kuwasemea, kuna kila sababu ya viongozi wa dini kuwasemea nk.

Hii itatusaidia sisi CCM kushusha msononeko huo walionao, hili litasaidia kutokujidhuru au kudhuru wengine, hili litatuleta pamoja zaidi kama taifa, hili litatusaidia kutokuzaa vikundi vya uhalifu nchini, vikundi vya kujitoa mhanga, hili litatusaidia kuwachelewesha kwenye uasi kama watapata mtu wa kuwasemea.

Naandika haya kwa maslahi ya taifa sio chama wala mtu. CCM Msinichukie tujadili hii hoja kwenye vichwa vyetu.... Nishukuru maeneo ambayo yameanza kusikiliza baadhi ya malalamiko yao.

Karibu jalalani

Ole Mushi
0712702602
 
Ushauri wako mzuri, ila unaowashauri vichaa. CCM siyo chama tena, CCM kabakia jiwe. Yote unayoona siyo mpango wa CCM. Afadhali ungekuwa mpango wa CCM usingeona uvundo wote huu. Nafananisha hizi mbinu na ushamba wa madaraka walionao mliowakabidhi chama. Poleni sana CCM.
 
Heti kuwajali wapinzani! Kuwajali kivipi? Upinzani ni siasa! Na siasa in hoja! Na hoja zinapambanishwa hili mshindi apatikane ashike dola! Sasa kama wameshindwa hoja hata katika chama lao la CHADEMA wamweshindwa democrasia ya ukomo wa Mbowe na wameshindwa kumuondoa ndo waote ndoto za mchana kukiondoa CCM madarakani?
 
Ili taifa lipone, inapaswa busara itumike ili mtu ampishe mwingine ktk ofisi, ili makovu na maumivu yakapate kusahaulika ili kuinusuru hatma ya umoja wetu wa kitaifa ambao uliasisiwa na Baba wa Taifa letu.
 
Wengine tulishasusia maswala ya kisiasa tangia yule bwana ashambuliwe kwa risasi mchana kweupe tena mbele ya cctv camera na wasiojulikana,uamuzi wa sasahivi wa Mbowe na Zitto kuviondoa vyama vyao ni wa busara sana ila umechelewa walitakiwa wasusie hizi shughuli tangu kipindi kile yule mtu alipopiga marufuku mikutano ya siasa kwa wenzake ila sio kwa chama chake! kama mazingira ya kufanya siasa ni kuhatarisha maisha ya wanachama wako huitaji kuwaburuza huko wakabambikiwe kesi zisizokwisha mahakamani,wangejitoa moja kwa moja hata uchaguzi wa mwakani wamuachie abaki mwenyewe awe anajitekenya na kucheka pekeyake!
 
Dunia ya sasa kuvuruga watu kwa kutegemea vyombo vya dola yafaa upimwe akili.Always jeshi usimama na wananchi kuepukwa kutengwa kimataifa pale nguvu ya umma inaposimama pamoja.Ndo madhara ya kutokusoma somo la history kule unajifunza kutorudia makosa yaliyopelekea kuanguka kwa tawala mfano ottoman,timbuktu,songhai,Mali,Mongolia,French revolution,mapinduzi ya romania,nk.Ajuaye history atembei gizani kamwe.
 
Wengine tulishasusia maswala ya kisiasa tangia yule bwana ashambuliwe kwa risasi mchana kweupe tena mbele ya cctv camera na wasiojulikana,uamuzi wa sasahivi wa Mbowe na Zitto kuviondoa vyama vyao ni wa busara sana ila umechelewa walitakiwa wasusie hizi shughuli tangu kipindi kile yule mtu alipopiga marufuku mikutano ya siasa kwa wenzake ila sio kwa chama chake! kama mazingira ya kufanya siasa ni kuhatarisha maisha ya wanachama wako huitaji kuwaburuza huko wakabambikiwe kesi zisizokwisha mahakamani,wangejitoa moja kwa moja hata uchaguzi wa mwakani wamuachie abaki mwenyewe awe anajitekenya na kucheka pekeyake!
Vipi ukimsusia fisi bucha ni kumsaidia au kumkomoa,aibu kaumbiwa aliyestaarabika na kuelimika
 
Heti kuwajali wapinzani! Kuwajali kivipi? Upinzani ni siasa! Na siasa in hoja! Na hoja zinapambanishwa hili mshindi apatikane ashike dola! Sasa kama wameshindwa hoja hata katika chama lao la CHADEMA wamweshindwa democrasia ya ukomo wa Mbowe na wameshindwa kumuondoa ndo waote ndoto za mchana kukiondoa CCM madarakani?

Hoja zipi sasa hali mnakimbia na mpira
 
Back
Top Bottom