Ole Milya amlipua Mnyeti, asema kuna genge la wahuni lilikuwa likimshauri Hayati Dkt. Magufuli vibaya

Mbunge wa zamani wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara ameibuka na kusema kuwa kuna genge la baadhi ya wanasiasa nchini walikuwa wanamshauri vibaya hayati Rais Magufuli vibaya kwa maslahi yao binafsi.

Ole Milya ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia hatua ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa fedha za serikali (CAG) kulitaja shirika la ndege la ATCL kupata hasara ya kiasi cha sh,60 bilioni katika ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2019/20.

Akizungumza na wanahabari Ole Milya alisema kwamba wanasiasa hao waliunda genge ambalo lilikuwa likimshauri hayati Rais Magufuli mambo ya hovyo kwa ajili ya matumbo yao.

Alimtaja mmoja wa wanasiasa hao ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza,Alexander Mnyeti kwamba mwanasiasa huyu alikuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa maslahi binafsi.

Mnyeti,aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru na kisha kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara ambapo Mara kwa Mara alitajwa kukwaruzana na Ole Milya kuhusu msimamo wake wa eneo la mgodi wa machimbo ya madini ya Vito ya Tanzanite One uliopo Mererani mkoani Manyara.

Ole Milya alisema kwamba Mara kwa Mara akiwa bungeni alilalamikia shirika la ATCL kuendeshwa kwa hasara lakini alionekana kichaa.

"Kuna genge la wahuni akiwemo Mnyeti hawa walikuwa wanamshauri Rais Magufuli vibaya sisi tulikuwa tukiongea tunaonekana wabaya" alisema Ole Milya

Ole Milya alidai kwamba hata wakati akiwa Mbunge akipigania haki za wachimbaji wadogo katika mgodi wa madini wa Tanzanite One ,Mnyeti aliwahi kumtakia kwamba asahau habari ya ubunge na atahakikisha apiti kwenye kura za maoni za Ccm.

"Huyu Mnyeti wakati tunavutana kuhusu Tanzanite One yeye alikuwa hataki wachimbaji wadogo alinitamkia nisahau habari ya ubunge na akaniapia atahakikisha jina langu linakatwa kwenye kura za maoni" aliongeza Ole Milya

Ole Milya alidai kwamba uamuzi wa hayati Rais Magufuli kufufua shirika la ndege la ATCL sanjari na ununuzi wa ndege hizo haukuwa mbaya tatizo lilikuwa ni kupotoshwa kwa genge hilo namna ya kuliendesha shirika.

"Mimi nilisema hata kwenye bunge lililopita tatizo halikuwa Rais Magufuli kununua ndege shida ilikuwa ni upande wa washauri wake walikuwa wanampotosha mambo mengi tu hata namna ya kuliendesha shirika" alisema Ole Milya

Ole Milya, alipongeza hatua zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kupambana na rushwa na ufisadi na kuwataka watanzania wamuombee na kumuunga mkono.

"Huyu Rais Samia amenyooka na kama atasimama bila kusikiliza wapambe atafika mbali ninamshauri ajiepushe na wanafiki tu atafika mbali sana" alisisitiza Ole Milya

Mwisho.View attachment 1737940View attachment 1737942View attachment 1737943
Matumbo yetu fc

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Huyo Millya kachanganyikiwa
Mbona hakuongea hayo wakati Magufuli yupo hai?
 
Kifo cha Magufuli kina mafundisho mengi sana. Ukisema uyaandike yote unajaza kitabu cha kurasa 1000.

'Mwanadamu kumbuka kuwa u mavumbi, na mavumbini utarudi'.

Kuna watu walipumbazika wakasahau kabisa kuwa uhai una kikomo. Walifikiri boss ataishi milele.


RIP Magufuli.
 
Back
Top Bottom