Ole Milya amlipua Mnyeti, asema kuna genge la wahuni lilikuwa likimshauri Hayati Dkt. Magufuli vibaya

James ole Milya ni kijana makini na mkweli sina hofu kuhusu msimamo wako kwenye mambo ya msingi
Toka aunge mkono juhudi Hana tofauti na Polepole tu mchumia tumbo. Ye avumilie tu huko alipo kila mtu acheze kwake
 
Mbunge wa zamani wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara ameibuka na kusema kuwa kuna genge la baadhi ya wanasiasa nchini walikuwa wanamshauri vibaya hayati Rais Magufuli vibaya kwa maslahi yao binafsi.

Ole Milya ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia hatua ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa fedha za serikali (CAG) kulitaja shirika la ndege la ATCL kupata hasara ya kiasi cha sh,60 bilioni katika ripoti yake ya ukaguzi wa mwaka 2019/20.

Akizungumza na wanahabari Ole Milya alisema kwamba wanasiasa hao waliunda genge ambalo lilikuwa likimshauri hayati Rais Magufuli mambo ya hovyo kwa ajili ya matumbo yao.

Alimtaja mmoja wa wanasiasa hao ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza,Alexander Mnyeti kwamba mwanasiasa huyu alikuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa maslahi binafsi.

Mnyeti,aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru na kisha kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara ambapo Mara kwa Mara alitajwa kukwaruzana na Ole Milya kuhusu msimamo wake wa eneo la mgodi wa machimbo ya madini ya Vito ya Tanzanite One uliopo Mererani mkoani Manyara.

Ole Milya alisema kwamba Mara kwa Mara akiwa bungeni alilalamikia shirika la ATCL kuendeshwa kwa hasara lakini alionekana kichaa.

"Kuna genge la wahuni akiwemo Mnyeti hawa walikuwa wanamshauri Rais Magufuli vibaya sisi tulikuwa tukiongea tunaonekana wabaya" alisema Ole Milya

Ole Milya alidai kwamba hata wakati akiwa Mbunge akipigania haki za wachimbaji wadogo katika mgodi wa madini wa Tanzanite One ,Mnyeti aliwahi kumtakia kwamba asahau habari ya ubunge na atahakikisha apiti kwenye kura za maoni za Ccm.

"Huyu Mnyeti wakati tunavutana kuhusu Tanzanite One yeye alikuwa hataki wachimbaji wadogo alinitamkia nisahau habari ya ubunge na akaniapia atahakikisha jina langu linakatwa kwenye kura za maoni" aliongeza Ole Milya

Ole Milya alidai kwamba uamuzi wa hayati Rais Magufuli kufufua shirika la ndege la ATCL sanjari na ununuzi wa ndege hizo haukuwa mbaya tatizo lilikuwa ni kupotoshwa kwa genge hilo namna ya kuliendesha shirika.

"Mimi nilisema hata kwenye bunge lililopita tatizo halikuwa Rais Magufuli kununua ndege shida ilikuwa ni upande wa washauri wake walikuwa wanampotosha mambo mengi tu hata namna ya kuliendesha shirika" alisema Ole Milya

Ole Milya, alipongeza hatua zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kupambana na rushwa na ufisadi na kuwataka watanzania wamuombee na kumuunga mkono.

"Huyu Rais Samia amenyooka na kama atasimama bila kusikiliza wapambe atafika mbali ninamshauri ajiepushe na wanafiki tu atafika mbali sana" alisisitiza Ole Milya

Mwisho.View attachment 1737940View attachment 1737942View attachment 1737943
Ole Millya nakushauri uache siasa za CCM. Ziliishakushinda kitambo tangu ukiwa Mwnyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.
 
Vita imeanza ya wao kwa wao sasa. Ila hao wanao laumiwa na kuitwa genge la wahuni waliokua wanamshauri vubaya Rais, nao watajitetea Mwendazake aliwahi kunena "MIMI SIPANGIWI, MIMI NI KICHAA KWELI KWELI INHIIIIII!!! HAYA!!!".

Cha msingi Rais Samia Suluhu acheze na waliothubutu kutudanganya kwamba mashirika ya ATCL na TTCL yalikua yanaendeshwa kwa faida kufikia hatua yaligawa gawio kwa serikali.

Watueleze hilo gawio walilopewa serikali ni gawio la hio hasara ya Billioni 60 au vipi??? Au gawio la kuifisadi hazina yetu???

Huenda hata habari ya gawio ni propaganda - hakuna pesa iliyohama! Tuliishia tu kwenye picha ya hundi, sherehe na makofi.

Tumechezewa sana watanzania!!
 
Ndege Moja unaweza kusema ni kosa.., ila unaongeza ya pili na ya tatu (je kulikuwa na uhitaji wa ndege zote hizo) kwanini kwanza usichukue moja na kuona muelekeo ?

Haya tuseme ni huduma hata tukipata hasara tunatoa huduma..., lakini huduma gani hio ambayo bei zimepanda baada ya kununua ndege badala ya kushuka ?

Kila nijaribu kutete huu uozo nashindwa pa kuanzia
 
Sio kwamba walikuwa wanamshauri vibaya,tuseme Ukweli Magufuli alikuwa HASHAURIKI.Hali hii ilifanya wengi wawe watu wa ndio ili kulinda vyeo vyao. Tuache kuficha wakati ukweli unajulikana.
 
Huyo Ole Millya akae kimya, yeye alienda kuunga juhudi kwa maslahi yake binafsi, kisha anamshangaa Mnyeti kupigania maslahi yake binafsi!Uamuzi wa kununua ndege ulikuwa makosa kwa sasa, hivyo apambane na wabaya wake asitake kuleta lugha za kitapeli.
Ana engineer bifu lake na Bwana Mnyeti kisayansi
 
Back
Top Bottom