Okwi Awapungia Yanga kwa Ishaya ya 5-0

IMG_1721.JPG
 
[h=1]MAKALA: OKWI NA HISIA ZA 5-0[/h]




Na Saleh Ally
MECHI ya kesho ya kirafiki ya Nani Mtani Jembe kati ya watani Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ina mambo mengi.



Burudani ya mchezo wa kesho inaonekana zaidi imetekwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba na mpya Yanga, Emmanuel Okwi ambaye anarudi tena katika mechi ya watani, akiwa upande wa Yanga.


Watakaokwenda uwanjani, wengi watataka kuwa mashahidi wa mawazo yao kwamba kweli Okwi anaweza kuichezea Yanga? Kesho atakuwa kwenye namba 25 lakini safari hii ni njano na kijani na si nyekundu na nyeupe.


Katika soka, yote yanawezekana lakini kikubwa ni kupata uhakika na kuwa shahidi wa macho, kuhakikisha kama kweli kimetokea.


Mambo mengi yanayovutia kwa Okwi hiyo kesho ni kwamba mechi yake ya mwisho ilikuwa ni Mei 6, 2012 Simba ilipoifunga Yanga kwa mabao 5-0 kwenye uwanja huohuo wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Baada ya hapo, mzunguko wa pili hakucheza kwa kuwa alikuwa na kadi nyekundu aliyoipata katika mechi dhidi ya JKT, baada ya hapo wakati Simba ikienda kupiga kambi nchini Oman kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili chini ya Patrick Liewig, yeye ‘akauzwa' Etoile du Sahel ya Tunisia.


Katika mechi ya ushindi wa mabao 5-0, Okwi alifunga mabao mawili, akasababisha mawili na sasa anarudi kuichezea Yanga. Swali, atasababisha au kufunga mangapi?


Kocha Ernie Brandts haitakuwa rahisi kumuanzisha, kwa kocha wa kiwango chake lazima ataangalia suala la ugeni wake katika kikosi, atamuanzisha benchi na kumuingiza hapo baadaye.


Akiingia atafanya nini? Ndiyo swali. Soka lina mambo mengi, huenda akaingia na kushangaza kwa kufanya makubwa kama kawaida yake, lakini inawezekana pia akadoda kwa kuwa anahitaji muda, yote yanawezekana.


Nani atamkaba?
Kama Kocha Brandts atamuingiza Okwi, mfano kuchukua nafasi ya Simon Msuva, beki yupi atakuwa na uwezo wa kutosha kumzuia? Kweli katika soka kila kitu kinawezekana.


Mfano mzuri wa makali ya Okwi, mkongwe Shadrack Nsajigwa angekuwa na jibu, lakini sasa huenda mzigo ukamuangukia Said Nassor ‘Chollo' au Issa Rashid ‘Baba Ubaya' kulingana na Zdravko Logarusic atakavyopanga kikosi. Itakuwaje? Vizuri kusubiri.


Pasi za uhakika?
Wakati Okwi aking'ara alikuwa amezungukwa na viungo mahiri wenye uwezo wa juu sana. Angalia Haruna Moshi ‘Boban', Mwinyi Kazimoto na marehemu Patrick Mutesa Mafisango. Swali, Yanga kuna watu wenye uwezo wa kazi hiyo?


Inawezekana pasi za Athumani Iddi ‘Chuji' au Frank Domayo zikawa msaada mkubwa kwake. Haruna Niyonzima pia anaweza kuwa hivyo, hasa kama ataachia mpira mapema kwa Okwi.


Anakutana nao:
Okwi anakutana tena na Juma Kaseja, Ally Mustapha ‘Barthez' (kama atakuwa katika listi) na Kelvin Yondani ambao alikuwa nao katika kikosi kile kilichoshinda 5-0.


Wao watatu au wanne wanaweza kuisaidia Yanga kulipa kisasi kesho? Majibu ya mpira ni baada ya dakika 90, kwani Simba pia inaweza kushinda na kuwashangaza ambao hawafikirii hivyo.


Berko tena?
Wakati Yanga inalala kwa mabao 5-0, Okwi alifunga bao ‘baya' la kwanza baada ya kuwapita mabeki watatu na kuingia nao kabla ya kupiga shuti lililompita kipa Mghana, Yaw Berko.


Leo Berko yuko Simba, hakuna ujanja lazima atakuwa langoni au katika benchi. Kama akianza maana yake atakuwa amekutana na Okwi tena baada ya miezi 15, ataweza kumzuia asitikise tena nyavu zake?


Hatari:
Huenda Hamis Kiiza akawa hatari zaidi kesho kwa Simba, licha ya kuwa, amekuwa akiwafunga mara nyingi lakini safari hii atasaidiana na Okwi ambaye amecheza naye mechi nyingi wakiwa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.


Okwi anajua Kiiza anataka nini, hali kadhalika Kiiza anajua Okwi anataka nini. Hivyo mabeki wa Simba wanapaswa kuwa makini na huenda Joseph Owino akawa msaada mkubwa kwa wenzake kwa kuwa pia anaijua vizuri kazi ya wawili hao wakati akiwa URA au wanapokutana The Cranes.


Mabadiliko:
Mashabiki leo wana kazi ya kubadili mambo, Mei 6, 2012, mashabiki wa Simba walimshangilia sana Okwi kuliko siku nyingine. Huenda leo wakafanya kazi kubwa ya kumzomea.


Mpira ni burudani ya aina yake, kwani hata mashabiki wa Yanga ambao walimzomea Okwi kwelikweli, nao watakuwa wakimshangilia utafikiri wanamuona kwa mara ya kwanza na hawakuwahi kumzomea hata kidogo.


Huenda ndiyo mapenzi ya dhati lakini ukweli ni kwamba wanampokea na kumsisitiza au kumshawishi kwamba na wao wanataka 5-0.


Ingawa timu hizo zilikutana mara mbili baada ya mechi hiyo, lakini bado mechi ya 5-0 ndiyo imekuwa gumzo zaidi. Kama ukiiangalia mechi hiyo, watakaokosekana leo katika kila timu ni hawa wafuatao:


Watakaokosekana Simba:


Juma Kaseja
Ally Mustapha ‘Barthez'
Amir Maftah
Shomari Kapombe
Mwinyi Kazimoto
Haruna Moshi ‘Boban'
Mutesa Mafisango (marehemu)
Felix Sunzu
Emmanuel Okwi


Watakaokosekana Yanga:
Yaw Berko
Shadrack Nsajigwa
Juma Seif ‘Kijiko'
Nurdin Bakari
Rashid Gumbo
Davis Mwape
Kenneth Asamoah


FIN
 
Back
Top Bottom