Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 667
- 1,467
Usiku wa kuamkia leo angani kulikuwa na kitu mfano wa nyota yenye muonekano wa mwanga mkali sana katika upande wa mashariki kuja katikati mwa anga kama utakuwa unaangalia juu wengi wamepata maswali na kujiuliza kuwa ni nini?
Kwa majibu ya haraka haraka ile ilikuwa ni sayari ya Saturn ambayo kwa siku ya jana ilikuwa inaelekea kuwa karibu na mwezi wetu, ukaribu ambao ulionekana katika nyakati za usiku wa manane au usiku ule mnene zaidi.
Katika mfumo wa jua Saturn ni sayari ya pili kwa ukubwa baada ya sayari ya Jupiter, ambapo Saturn kwa upande wa ikweta ina mzunguko wa ukubwa wa Km 119,300 ambapo kwa ukubwa huu ni sawa na ukubwa wa mzunguko wa dunia yetu kwa upande wa ikweta mara 9 zaidi
Kwa wale wafuatiliaji matukio ya angani kwa karibu zaidi, siku ya jana na leo ndio siku nzuri ya kufanya tafiti katika sayari hii kwakuwa ipo katika eneo ambalo ni rahisi kupata muonekano wake kama utatumia professional telescope.
#Source By, Moudyswema #Tanzaniascienceyetu #Elimuyaangazambali