Oktoba 28 ni mashindano kati ya Ukweli na Ubatili. Wanaojielewa, kujitambua na kutaka maendeleo ya kweli, watachagua ukweli. Wewe upo kundi gani?

Mkuu Invigilator , huu ndio uzuri wa demokrasia, rukhsa kumchagua yoyote, hivyo kuchagua ubatili pia ni haki yako ya kidemokrasia.
P
Nakutuma Mkuu Pascal Mayalla kwa Mgombea wako! Mwambie hana haki ya kuwaamulia Watanzania kumchagua Mgombea wampendaye!

Lakini pia umwambie hayo maendeleo anayotuhubiria sasa, yalishafanywa na watangulizi wake kitambo tu, hivyo yeye si mtu wa kwanza kununua ndege au kujenga bwawa la kuzalisha umeme!

By the way, hizo hela zinazotumika kujengea hiyo miundombinu, hazitoki mfukoni mwake! Ni kodi za Watanzania wote! Wafuasi wa vyama mbalimbali vya kisiasa, na wale wengi tusio na vyama. Yaani kwa sababu chungu kamkabidhi mpwa basi anajiona yeye ndiye mmiliki!

Na usisahau kumwambia aachane na hii tabia yake sugu ya KUTUFOKEA na KUTUPANGIA Watanzania nini cha kufanya! This is a Democratic State! It is NOT a DICTATORSHIP Country like Rwanda, North Korea, etc.
 
Tuchague mtu asiye na kashfa Wala si
. Dikteta
. Fisadi
.Mwizi
.Muongo
.mbaguzi
.Mdini
. Mkabila
.Mkanda
. Katili
. Muuaji
. Visasi
.Mpenda bifu na ligi
. Zulumati
.Asiyejiamini
.Muoga
. Mwenye uwezo wa kureasoning na sio claiming
. Matured, educated and civilized
.Mtesaji
Viongozi wenye sifa hizi piga kura za hapana kubwa.
 
Wewe pascal, Siku ile ulimuuliza magufuli kuhusu uvunjifu wa katiba ..vipi Leo kuita upande wake ukweli? Au nikweli mayala inamanisha njaa?
 
Ndugu yangu umejitahidi sana kupambanua hoja yako lakini jambo moja umesahau, uwezo na mamlaka ya kuamua kipi ni ukweli na kipi ni ubatili kila mmoja wetu anao na anaweza kufanya hivyo kwa kadri ya mtazamo wake.

Umeichukua kauli ya mgombea wa chama kimoja kuuelezea ubatili na ukweli, mambo hayaendi hivyo.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ambao ni mashindano kati ya ukweli vs ubatili, Je, wewe utachagua nini? Utachagua ukweli au ubatili? The choice is yours!

Declaration of Interest
Japo mimi Pascal Mayalla ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM ila mimi ni Kada Mzalendo ambae ninatanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa mkweli daima, na siku zote huwa nausema ukweli halisi jinsi ukweli huo jinsi ulivyo, bila kujali ukweli huo kama ni ukweli wa haki, ni mchungu vipi au unauma vipi, as long as ni ukweli nitausema.

Sisi Watanzania tuko watu wa aina mbili:
1. Kundi la kwanza ni la Watanzania Wakweli, the realists wanaoukubali ukweli halisi jinsi ile ulivyo, hawa ni watu walio jitambua na wanao jielewa hivyo tarehe 28, October, watachagua ukweli.

2. Kundi la pili, ni kundi la ubatili, hawa ni wishful thinkers and day dreamers, hawa ni Watanzania wenzetu, wasiojielewa na wasio jitambua ambao wanaishi kwenye Tanzania ya kusadikika, utopian society, hawa tarehe 28 October, watachagua ubatili.

Je, wewe uko kundi gani?Je, uko kundi la ukweli au ubatili? Tarehe 28 October, utachagua kweli au utachagua ubatili?

Maendeleo ya Kweli vs Ubatili
Tanzania tulitawaliwa wakoloni Wajerumani kisha Waingereza, walituachia baadhi ya misemo ya kizungu ambayo ni ya ukweli mtupi japo ukweli mwingine ni ukweli mchungu kumeza lakini ndio ukweli wenyewe halisi!.

Moja ya misemo hii ya wazungu, ni msemo huu " The Boss is Always Right" yaani anachosema mkubwa, ndicho kitu cha ukweli, mkubwa huwa hakosei, na hata akikosea, kosa hilo hugeuka ndio kitu sahihi na ndio ukweli wenyewe!.

Kwa sasa, kwa nchi yetu Tanzania, the top boss ni rais wa JMT, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, katika kampeni zake, rais Magufuli ameomba, ili kutuletea maendeleo ya kweli, rais Magufuli ameomba tumchagulie rais, wabunge na madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi, CCM, mkichagua upinzani, mtakuwa mmechagua ubatili, sahauni maendeleo!.

Kauli hiyo ndio ukweli wenyewe halisi uliopo kwenye uchaguzi huu, kama wewe ni Mtanzania, ni mkweli, ni mtu anaejitambua na unaejielewa na then tarehe 28 October, utachagua ukweli.

NB: Ukweli sio lazima uwe the right thing, yaani ukweli halisi sio lazima uwe ni wa haki, hata kama ukweli huo sio ukweli wa haki, lakini ndio kitu halisi kilichopo. Kauli ya rais Magufuli kuwa usipochagua CCM, hataleta maendeleo, kwa vile maendeleo hayana chama, hivyo kauli hiyo sio kauli ya haki, lakini ndio kauli ya ukweli wenyewe uliopo!

Sasa kama wewe ni mkweli na unachotaka ni maendeleo ya kweli, then ili kuyapata hayo maendeleo, maadam the boss is always right, na the boss ameisha sema tumchagulie nani, ili atuletee maendeleo, then wakweli wote wanajua tarehe 28 October watachagua nini, nani na chama gani!.

Ukweli ni upi?
Ukweli ni kauli ya rais Magufuli, kuwa ili kupata maendeleo, tumchagulie viongozi wa kutoka CCM, mkichagua upinzani, maendeleo utaishia kuyasikia.

Ubatili ni upi?
Baada ya kusikia kuwa usipoichagua CCM hutapatiwa maendeleo, utaishia kuyasikia tuu hayo maendeleo, hii maana yake, ukiamua kuuchagua upinzani, maana yake ni umechagua ubatili. Je, wewe utachagua nini kati ya ukweli na ubatili?

Kwa vile uchaguzi wa mwaka huu ni mashindano kati ya ukweli na ubatili, Watanzania wanaojielewa, kujitambua na kutaka maendeleo ya kweli, Tarehe 28 October, hawa watachagua ukweli, lakini kuna Watanzania wenzetu ambao hawajielewi, na hawajitambui, hawa tarehe 28 October, watachagua ubatili. Je, wewe mwenzangu na mimi, uko kundi gani?

Nakutakia Uchaguzi Mwema.
Paskali
"Njaa"
 
usipoichagua CCM hutapatiwa maendeleo, utaishia kuyasikia tuu hayo maendeleo,
Mkuu Pascal Mayalla nilitegemea utumie kipawa na taaluma yako ya uandishi kukemea ubaguzi huu wa kisiasa unaohubiriwa na mgombea urais wa chama chako.

Kuchagua upinzani siyo kosa linalostahili mwananchi kunyimwa Maendeleo kwasabb upinzani upo kwa mujibu wa sheria. Lkn pia wananchi waliochagua upinzani wanalipa kodi na tozo nyingine zote sawa na wale waliochagua ccm.

Tutofautiane kiitikadi lkn tuungane kukemea uovu.

Sote tunakumbuka siku Ile pale ikulu mwanzoni mwa utawala wa huyu mwenyekiti wako Pascal Mayalla ulionesha njia kwa kumpiga maswali yenye lengo la kumrudisha kwenye mstari.

Natamani kuendelea kukuona Pascal Mayalla wa enzi hizo.
 
Kwenye urais nitawapa ccm kwa sababu pamoja na madhaifu makubwa waliyonayo wapinzani bado hawajanishauri kuwapa kura yangu kwa upande wa rais kwani hawaeleweki wanasimamia maslahi ya nani.

Upande wa wabunge nitawapa upinzani kwani sikubaliani na pointi ya rais aliyepo kuwa ilikupata maendeleo tumchagulie wabunge wa ccm.

Kama tungekuwa na upinzani unaoeleweka hata mgombea wao asingepata kura yangu na anaipata si kwa sababu ni bora ila kwa aina ya mpinzani aliyenaye.
 
Mkuu Molemo , ni lini niliwahi kuleta kiapo chochote humu jukwaani? Ila pia kwani Chadema bado iko hai?. Kilichomo ni Tundu Lissu ndie anashabikiwa na sio Chadema as chama, je unamjua aliyemshauri Lissu agombee urais ni nani? Angalia tarehe ya bandiko hili
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

P
Eti aliyemshauri Lissu agombee. We jama umepoteza wengi sana waliokuwa wanakuamini kuwa "objective on issues".

Naamini kuna watu wamejifunza kito kutokana na "u turn" ulioifanya.

Ukweli wa ubatili vs ukweli wa haki na maendeleo ya watu.
 
Mkuu Molemo , ni lini niliwahi kuleta kiapo chochote humu jukwaani?. Ila pia kwani Chadema bado iko hai?. Kilichomo ni Tundu Lissu ndie anashabikiwa na sio Chadema as chama, jee unamjua aliyemshauri Lissu agombee urais ni nani?. Angalia tarehe ya bandiko hili
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

P
Mkuu Chadema bado iko hai Sana tu.... na sio ya kufa leo.... Chadema kwa Sasa ni taasisi...watabadilika watu tu....kulijua hilo angalia vigogo walioondoka na chama bado Kiko hai...mmoja wao Dk Slaa..nikweli Lissu ana mvuto....lakini Chama pia kinaongeza mvuto... Unadhani kwa mfano Lissu angegombea kupitia Chama cha Mbatia angekuwa na nguvu sawa na hii.... kwa Sasa CHADEMA Ni chama kubwa....hata mzee Wasira aliwahi kusema CHADEMA itakufa....siku hizi naona yuko kimya.
 
Mkuu Molemo , ni lini niliwahi kuleta kiapo chochote humu jukwaani? Ila pia kwani Chadema bado iko hai?. Kilichomo ni Tundu Lissu ndie anashabikiwa na sio Chadema as chama, je unamjua aliyemshauri Lissu agombee urais ni nani? Angalia tarehe ya bandiko hili
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

P
Pascal siku hizi unachanganya sana. Kwako uchaguzi ni kitu gani ?!. Ushindani katika siasa za uchaguzi ni kukichagua Ccm ?!. Basi unaamini ktk democracy ya ajabu. Yah Maghufuli ni Rais lakini lazima ashindanishwe na mwananchi mwingine mzalendo mwenye mawazo tofauti juu ya uendeshaji nchi .

Pascal tumieni usomi wenu ndani ya Ccm, kukiokoa chama hicho toka Mkononi mwa wahafidhina wa ki communist walio ndani ya chama. Kwani kwenye u communist ni kusifu na kuabudu. Na ndicho unachokifanya sasa
 
Back
Top Bottom